Wazazi tuendelee kuchangia elimu ya watoto wetu

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,527
Kumekuwapo na matamko ya kuzuia michango shuleni lakini ukweli ni kwamba hawa wanaotoa matamko haya watoto wao hawasomi shule hizi za kata na ajenda yao ni kuwafanya Watanzania tuendelee kuwa wajinga na wapumbavu.

Kikawaida fidia ya elimu bure ni Tsh 20000 kwa kila mwanafunzi, kiasi hiki cha pesa ndo hutumika kuendesha shughuli zote za shule kuanzia mitihani,ukarabati, vifaa vya kufundishia, umitashumta/umisseta na wakati mwingine kulipia walinzi wa shule n.k.

Ukweli ni kwamba kwa shule nyingi kiasi hiki hakitoshi, mathalani shule zinahitaji kuwa na mitihani ya mara kwa mara kuwapima wanafunzi wake na kuandaa kwa ajili ya mitihani ya mwisho, Kuna shule hazina miundombinu kama madawati, viti na meza, Kuna shule hazijitoshelezi kwa walimu hivyo inabidi waajiri walimu wa ziada kufundisha.

Vitu vyote hivyo vinahitaji nguvu ya wazazi kuchangia na kuhakikisha inatolewa elimu nzuri, tukiendelea kuwasikiliza hawa wanasiasa tutakaopoteza ni sisi wazazi maana wao watoto wao wanasoma shule nzuri na za gharama, tujiulize kama elimu bure ni nzuri mbona hawapeleki watoto wao, mbona watoto wao wanasoma shule za gharama zinazofanya mitihani mara kwa mara na zenye mazingira rafiki ya kujifunzia.

Hawa wanasiasa hawana urafiki na sisi wanatudanganya elimu bure mtoto akimaliza kidato cha nne wanampanga chuo cha kati chenye ada zaidi ya 1M, hivi kama wana huruma kweli na sisi wananchi kwanini isiwe elimu bure toka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu, halafu watoe pesa za kutosha kuendesha shule zetu hizi.

Lengo lao ni kutengeneza kizazi cha wajinga wasio weza kuhoji, wasioweza kuchukua nafasi zao na za watoto wao.

Watanzania tugutuke.
 
Back
Top Bottom