Wazazi tubadilike; huu si muda wa kumlazimisha mtoto kusoma unachotaka wewe

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,121
5,219
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kumekuwa na ukatishaji ndoto kwa watoto na unyanyasaji mkubwa wa vipawa na machaguo ya watoto hasa pale wanapotaka kusoma au kufanya kitu ambacho mzazi anakichukulia ni duni au si kipaumbele chake.

Chukulia mfano mtoto aliyemaliza form four na akafahulu vyema katika masomo yake yote kwa div 1 na akapangiwa shule kujiunga na kidato cha sita ila akamwambia mzazi mimi na elimu ya kidato cha 6 hapana nina ndoto nyingine isiyoitaji mlolongo huo aidha nipeleke nikapate ujuzi husika au kozi fulani, tiyar mpaka hapa ni ugomvi usiyoweza hamulika.

Leo hii watoto wanasoma kwa sababu mzazi analazimisha kasome hata kama mtoto anachosoma hakipendi na kinamwathiri kitaaluma na kisaikolojia, utakuta umemkalia mtoto kooni kasome sayansi upate ajira umwoni mtoto wa fulani kafanikiwa huoni fulani ameajiriwa we unafikiri ukisoma sanaa utafika wapi kama siyo kuishia kuwa mwalimu wa art asiyeajirika au mwanasheria na suti nyeusi kutwa kiguu na njia ila hana pa kulala.

Yawezekana ushauri wako ni mzuri na muhimu na kile ukisemacho ni kweli kulingana na mazingira ya ajira nchini na pia ni kweli kuwa hayupo mzazi hata mmoja atakaye mwanaye asome vitu ambavyo baadae havitompa manufaa na hadhi nzuri kwenye jamii inayomzunguka.

Lakini huyu mtoto naye ana hiyari yake ebu msikilize najaribu kuvivaa viatu vyake, yeye kama yeye anasababu gani kuchagua hicho alichochagua na je wahisi kwa ufahamu halio nao na msimamo wake ni thabiti kiasi kwamba atojilaumu kwa maamuzi yake ya sasa na ya kwamba uamuzi huo umetoka moyoni mwake na si kwa kushawishiwa au kupotoka.

Ikiwa maamuzi haya ya mtoto huyu kukataa kujiunga na elimu ya sekondari, vyuo vya afya, uaskari au ualimu na chuo kikuu na badala yake anataka kujiunga na kampuni ya ulinzi,ususi, ujasiriamali au anataka umpeleke gereji nakadhalika, tofauti na matarajio yako ya mwanzo na ni kweli amedhamiria kwa dhati tafadhali mwache na usimpangie hata ikiwa wewe ndiye umsomeshaye unachotakiwa kufanya ni kutoa carrier guidance and counselling (CGC) upande wa maamuzi muachie mwenyewe.

Usianze zile kauli za mimi sikusomeshi kama umechagua hilo tafuta wakukusomesha mie nimechoka mizigo na wewe unataka hurudi kuwa mzigo tena kwangu kama umegoma kufanya hivyo tafuta pa kwenda kuishi na siyo kwangu.

Huu ni unyanyasaji, ukatili na ukale uliopitiliza kama mzazi wa kisasa tambua kuwa sasa hivi ajira ni mbinde kotekote awe amesoma au hajasomea hicho unachoshinikiza asome, hivyo ni heri asome kile akipendacho itamfanya awe na juhudi binafsi maishani katika kile alichokichagua

hata kama hatopata kazi haitomwia vigumu sana kukopi na mazingira ya fani au kazi aliyoichagua na vile vile hatokuwa na haki ya kumlahumu mtu yeyote kuwa ndiye sehemu ya anguko lake kwa kumpangia future isiyo yake, naomba niishie hapa kazi kwenu wazazi wa sasa na watarajiwa.
 
Sometimes sisi kama wazazi tumeona mengi sana acha tuwapangie vya kusoma
Akizaliwa tu asome,bila hivi silipi ada
1.Udaktari
2.Engineering
3.Biashara
 
Law vipi?
Hiyo muda sana watoto wa maskini wanalala njaa na degree za hiyo kozi,hiyo kozi ni kama una network au ndugu anamiliki law firm yake ndo unasoma ili mkafanye kazi but ni kozi nzuri hata mtoto mmoja kwenye familia asome ili awalinde
 
Back
Top Bottom