Wazazi ndio chanzo cha wake wabovu katika jamii

Nsam

JF-Expert Member
Oct 25, 2018
212
286
Nimeenda somewhere kumtembelea ndugu yangu nimegundua wao ndio hutengeneza wanawake wa baadae wabovu pasua kichwa na wa kututesa baadae

Yaani watoto wanalelewa ovyo ovyo ovyo sana

Mtoto hajui neno hamna! Hakuna

Chakula kinapikwa mtoto hataki kula kisa tu ni ugali au chakula kingine asichotaka

Mtoto yupo radhi alale njaa kisa hajapata chakula anachota, anataka chips mtoto wa darasa la tatu au nne anata kupasua kichwa unasema mtoto amenishinda?

Mzazi mwenyewe anajua mtoto wake atampa shida mumewe! Mtoto anakosa kitu analia hadi anaanguka chini anapewa!

Jf jamani sisi ndio wazazi tuache ukisasa wa kifala tunapoteza watoto na kuwapa kazi wanaume kulea hao watoto wenu
 
ASILIMIA KUBWA SANA YA MALEZI YA SASA KWA WATOTO NI MABOVU MNOOOO,WAZAZI,JAMII,WALEZI,SERIKALI NA WADAU WOTE TUNA HATIA JUU YA HILI

Nimeshangaa nimeshangaa ovyo sana
 
Sio wazazi wote, ila wapo ambao huharibu watoto wao kutokana na malezi ya nyumbani, kifupi kunakuwa hakuna maandalizi ili kumuandaa mtoto wa kike kuja kuwa mke mwema...
 
Hizo tabia za hao watoto zinafanywa na watoto wa kike tu au hata wa kiume?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom