Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 36,655
- 83,584
Siombaya nikiweka wazi kwamba sasa ninaendelea vizuri baada ya kupigwa na dhoruba kali siku kadhaa silizo pita.
Back to the point..
Baada ya serikali kuamuru watoto wetu warudi majumbani toka mashuleni ili kupisha janga hili la COVID19, kuna mambo kadhaa nimeyaona huku mitaani.
Kwasasa ni jukumu la wazazi kuwalinda watoto wetu ili wawe watulivu majumbani.
Huku mitaani kuna ombwe na vijana wanazagaa kitaa, pia vijana hawa wamekuwa na matembezi mengi yasio ya msingi kabisa. Hali hii imenipelekea mimi kama mzazi kuamua niwakumbushe wazazi wenzangu wawe makini na watoto wao.
Na kwakuwa sasa watoto Wapo mikononi mwa wazazi/walezi basi nijukumu sasa kwetu sisi kuwa thibiti watoto hawa ambao ninaona kabisa pasipo udhibiti watoto wengi wataanza kujiingiza kwenye matendo yasio mema na wakike watajikuta wana tiwa mimba za utotoni, na hata kujiweka kwenye mazingira hatarishi kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, milipuko nk.
Nashauri wazazi na walezi kuliangalia hili kwa upana na hasa wajitahidi kila mmoja kumdhibiti watoto wake, maana bila hivyo tutajikuta baada ya kumaliza janga la COVID19 tutajikuta tumezalisha janga lingine jipya la watoto kupata mimba za utotoni na vijana kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu.
Mwenye sikio na asikie.
Naomba kuwasilisha........
Sent using Jamii Forums mobile app