Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,323
- 40,172
Wazazi msiwapangie au kuwatafutia wachumba watoto wenu.
Kuna rafiki yangu mmoja tumeshibana sana.Tangu shule ya msingi mpaka sasa hivi nywele zinakaribia kubadilika rangi. Baada tu ya kuhitimu chuo kwa upande wangu nilitafuta mke anayeendana na mahitaji yangu,kuanzia muonekano n.k na kuishi naye. Rafiki yangu akawa bado anajipanga ili aweze kuja kupata mtu sahihi. Baada ya kama miaka 2 nilisafiri mimi na mke wangu kwenda mkoa fulani ambapo rafiki yangu kwa kipindi kile ndipo alipokuwa anafanya kazi. Baada ya kumaliza shughuli zilizonipeleka,nilimtafuta rafiki yangu ili tuweze kubadilishana mawazo. Tukapanga sehemu ya kukutana na kweli tukafika katika ilo eneo,tukapata chakula cha jioni;mimi nikiwa na mrs na yeye akiwa na mchumba wake mtarajiwa. Tukatambulishana pale,nami nikampongeza kwa kuwa na mpenzi mwenye mvuto.
Baada ya kama mwaka mmoja akanijulisha anataka kufunga ndoa,lakini si na yule mchumba wake wa mwanzo....bali kuna mwingine ametafutiwa na wazazi;mi nikamuuliza imekuwaje mkuu mpaka umetafutiwa,akasema yule wa mwanzo alikataa kubadili dini na pia wazazi wameona atakuja kunisumbua huko mbeleni.
Changamoto zilizopo kwa sasa, rafiki yangu hana utulivu na familia yake na ukimtazama unajua kweli mtu huyu ana mawazo tele.Mwezi uliopita niliweza kumtembelea kutokana na majukumu yangu ya kikazi...ndipo nilipogundua ana mawazo tele.Nahisi..anajutia kufanya makosa katika uoaji,kwani mke ana sura ya kiume..na watoto wamechukua upande wa mama.Ingawa ndoa yake haina migogoro kwa sababu 'no competition' ila kwake utulivu wa nafsi ni sifuri.
Kwa hli hiyo,wale mnaotaka kuoa/kuolewa msipende kutafutiwa wachumba....ingia mwenyewe mbugani na winda mnyama mzuri aliyenona anayetuliza kiu yako.....vinginevyo utaletewa nyama ya fisi;ingawa unaweza kujifariji tutazoeana tu huko mbeleni