Wazazi msiwalazimishe Watoto kusoma vitu wasivyovipenda

Rosemary Stephen

New Member
Oct 22, 2019
3
5
Wazazi wengi mmekuwa kikwazo cha watoto wenu katika kufikia ndoto zao na malengo yao. wazazi wengi mnawalazimisha watoto wenu kufanya vitu mnavyovitaka nyie na sio wanavyovipenda wao .

Mnawanyanyasa watoto na kuwafanya waishi maisha ya kulazimisha sana katika jamii zao. Unakuta mzazi anamlazimisha mtoto asome ili awe daktari na fimbo kabisa anachapwa akisema anataka kuwa mwalimu.

Ni kweli ni wazazi lakini hamna nafasi ya kuamua ubadae wa mtoto wako hasa katika ndoto zake.Kama mzazi unatakiwa kuwa kipaumbele kwa mwanao kujua kipaji chake na kumkuza katika hiko.

Mmetuletea sana wanasheria feki na madaktari feki mitaani kwa sababu ya kutimiza matakwa yenu tu. Bado mmetuletea walimu wasiowafundisha wanafunzi kwa moyo badala yake ni kuishia kuharibu watoto wetu , kuwatia mimba na kuwapa adhabu kali.

Nchi za wenzetu moja ya jambo ambalo wamelipa kipaumbele katika makuzi na malezi ya mtoto,ni kujua kipaji chake na ndoto zake na kumsaidia kuzifikia. Ndio maana Tanzania yetu haina maendeleo kwa sababu bado watu wanalazimsihwa kusoma vitu wasivyovipenda na bado wanalazimishwa kufanya kazi wasizozipenda. Hivi sasa kweli tutakuwa nchi ya namna gani? maana ubora wa mtu UNAONEAKANA PALE ANAPOFANYA KITU ANACHOKIPENDA sasa .

-Tunatakaje madaktari bora kama wanalazimishwa kuwa madaktari?kwanini wasisahau mikasi tumboni?kwanini huduma ziwe bora?kwanini watu wapatiwe huduma za haraka ?

Unaenda hospitali unakuta daktari kajifungia mlango anangalia movie kwenye pc yake na kuna foleni ya wagonjwa nje. Je unafikiri ni kwanini? Ni lwa sababu sio kitu wanachokipenda na ndio maana hayo yanayokea.

Wazazi tuwasaidie watoto wetu kujua vipaji vyako na kuwasaidia katika hivyo, bila hvyo tutaendelea kufuga ujinga na upumbavu na nchi yetu itazidi kuwa nchi ya watu wasiojitambua.
feature.jpg
 
No comment.

Na ukiangalia kwa makini utagundua wanafanya ili wapate sifa kwamba mwanangu ni mwalimu nk.

Wazazi wameupata ujumbe ndio maana wamepiga kimya.
 
Mzazi wako anaupeo kuliko wewe,anachofanya Ni kukushauri usiaome course ambazo ukimaliza unarudi kuwa mzigo kwa wazazi.
 
Mzazi wako anaupeo kuliko wewe,anachofanya Ni kukushauri usiaome course ambazo ukimaliza unarudi kuwa mzigo kwa wazazi.
Unadhani mzazi wako atakuwepo milele ili akushauri wewe?

Mtoto anatakiwa ajitambue na ajue kumake choices zake mwenyewe bila ya mtu yoyote na mzazi anatakiwa kuwa guider na sio commander.
Au huyo mzazi amefail kwenye malezi.

Matokeo yake mtoto anakuwa mtu mzima bado anashindwa kumake necessarily hard decisions sababu anaamini upeo wake hautoshi kufanya maamuzi magumu tena mengine ni binafsi.
Ataomba ushauri mpaka kwa watu ambao sio sahihi mwishowe anapotea.
Wengine utawakuta humu wakishauriwa pumba mara nyingi.

Now prove me wrong if you can.
 
Wewe kasome hayo macourse yako yasiyo na future,utakapomaliza chuo na kurudi nyumbani uwe furushi kwa wazazi,Siku ukifukuzwa nyumbani ukajitegemee usije tena kulia Lia hapa jf eti unaomba ushauri.
 
Back
Top Bottom