Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,808
- 59,317
Lizzy, mimi naona wakati mwingi hii mbinu ya Mtorii inasaidia. Kuna dada namfahamu, pamoja na kuolewa, lakini hataki baba mtoto wake (ambaye ameshaoa) amchukue mtoto si kwa kusalimia wala nini. Na madai yake hataki mtoto wake akaishi na mama wa kambo. SIna tatizo na argument yake, lakini anafikia to the extent ya kumwambia baba mtoto kama anamtaka mtoto kumsalimia basi amchukue azunguke naye tuu, na siyo kumpeleka kwake jioni arudishwe. Watu wakamshika masikio mwanaume wakamwambia mtoto hagombaniwi, muda muafaka ukifika atakutafuta tu, cha msingi wewe kama ni ada lipa shuleni na achana na kukimbizana na mambo ya mtoto. Na kweli, imemletea amani mwanaume coz sasa hivi yeye ndiye anatumiwa ujumbe kuwa mtoto aje likizo? Kwa sababu hamna mtu wa kuendekeza drama alizokuwa anaziibua pale linapogusiwa suala la mtoto.
Kwa mtazamo wangu mie, hizi purukushani za wazazi wenza mwisho wake ni watoto ndio wanaoumia, coz ukimkuta baba kichaa anasusa kabisa hata kuhudumia huyo mtoto. Labda ukikuta na mama mtu anaweza kumhudumia mwenyewe.
Alitumia akili kwa kutotaka mashindano na mama mtu....ila hiyo ya kukataa mtoto alelewe na mama wa kambo hata mimi naisupport sana.Mtu uko hai mwanao analelewa na mtu mwingine...na ukifa je?!