Wazazi mmejipanga vipi kukabiliana na athari za utajiri na umaskini katika familia zenu ikiwa watoto ndio wahanga wakuu?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,190
56,793
Ni dhahiri nje na tabia za kurithi, mtoto hutohoa tabia kutoka katika jamii inayomzunguka hasa katika ngazi ya familia.
Utajiri na umaskini ni hali zinazopatikana katika familia hasa umaskini katika bara la Afrika!.

Mambo haya mawili yamekuwa na athari kwa watoto na kupelekea uchanya ama uhasi katika tabia za watoto. Mfano familia maskini mtoto anaweza jishusha thamani kutokana na kujiona si lolote katika jamii hivyo kujidharau na jamii kumdharau pia na hii hupelekea kiumbe hichi kutenda uovu katika namna yoyote.

Vivyohivyo katika upande wa familia tajiri mtoto huweza kujiamini kupitiliza na hata kuona wengine takataka si lolote mbele yake. Kwake mali ndio lugha ya kila kitu! Hana thamani ya utu n.k

Na si hivyo tu baadhi yao katika familia hizi tajiri huwa legelege na hii humkosesha utendaji imara akikutana na mazingira tofauti.

Hayo ni machache tu katika upande hasi nafahamu upo upande chanya, lakini si wakuuzungumzia kwani hata Daktari huacha kilicho kizuri na hutibu kilichoharibika.

Nafahamu wapo wenye uwezo wao kama wao kwa kukabiliana na changamoto hizi kitabia,hivyo kwa wale walioshindwa tunawasaidiaje?

Mzazi ni kivipi unakabiliana na athari za umaskini na utajiri katika familia yako hasa watoto?
 
Back
Top Bottom