Wazazi, mimba ni aibu ila kifo cha mtoto akijaribu kutoa mimba ni aibu zaidi

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,743
4,269
Nimesikitishwa na habari ya mtoto wa miaka 13 wa Kisumu Kenya aliyefariki akijaribu kutoa ujauzito wa wiki nne. Binti huyo alitumia kining'iniza nguo (Hanger) kujaribu kutoa mimba yake na kupelekea mfuko wa uzazi kuharibika vibaya iliyopelekea kuvuja damu nyingi na mwisho kusababisha kifo kwa binti.

Kifo cha huyu binti kimeniuma sana hasa niliposoma na kugundua kuwa chanzo cha kadhia yote hiyo ni uoga tu kwa wazazi wake. Wazazi walishamuonya binti kuwa akipata ujauzito ni bora autoe na si kwenda nao nyumbani kwani wangemchuna ngozi akiwa hai.

Maneno hayo ya wazazi yanaweza kuchukuliwa kwa wepesi, au kuonwa ni vitisho tu vya kawaida ili mtoto asikosee lakini ni mazito na naamini yalimuingia akilini vilivyo binti hadi kupelekea kutumia njia katili kwake yeye na kwa kiumbe chake ili tu kujinusuru.

Wazazi, mimba yaweza kuwa ni aibu kwenu lakini mtoto akishazaliwa hakuna atakayekumbuka tena ile aibu. Mtoto wako akijiua kwa jaribio la kutoa ujauzito itakusumbua maisha yako yote, itakuwa ni aibu ya milele kwako na kumbukumbu ya mwanao itakuwa imeharibika kwani atakumbukwa kama "yule binti aliyefariki akijaribu kutoa mimba".

Sisemi tusiwaonye watoto wetu kuhusu suala hilo ila tuwe na uchaguzi mzuri wa maneno tuongeapo na watoto kwani akili zao haziwezi kuchanganua vizuri kauli kama watu wazima. Tuwaambie faida watakazopata kwa kujitunza kwao na thamani yao na maisha yao. Tuepuke kauli za vitisho vilivyopitiliza kwa watoto yasije tukuta makubwa tukajuta.

Ni hayo tu.
 
ila watoto wa siku hizi waanaanza kupigwa miti mapema jamani? miaka 13 ndo mtu unamaliza la saba hapa bongo
sasa hapo binti keshaanza kukipanua akifika 30 inakuaje hata utamu hasikii tena ndo haya ya kuita wakaka vibamia vibamia
mabinti wafundioshwe tu kujisitiri pia hata hilo tendo halina raha yoyote unatumika tu
 
Sio siku hizi tu hata zamani....na binti kuanza hayo mambo pia ina maana kuna kitu kinalack kwa wazazi...
 
Asante sana mpendwa kwa maelezo yako mazuri, ni vyema wazazi kufahamu namna ya kuwaonya watoto wao pasipo kutumia lugha kali km hiyo iliyopelekea huyo binti kujiumiza vile na mwishowe kupoteza maisha.

R.I.P
 
Wazazi wawafundishe watoto jinsi ya kuwa na responsible relationships'.
Watoto wanatakiwa wajitambue na kujielewa toka wakiwa wadogo.
Haya mambo wanaelekezwa toka wakiwa wadogo, ili wakikua waone kila kitu ni ubatili tu.
 
mbona unajibu sana na kama vile unatetea ni kweli ni vibaya kuanza mchezo huo ila haitakiwi kutetea lakini hukumu zingine zinatokea ili iwe fundisho kwa wengine..... RI.P.
 
Sio siku hizi tu hata zamani....na binti kuanza hayo mambo pia ina maana kuna kitu kinalack kwa wazazi ...
Sifikiri kama hiyo ni sababu kwa walio wengi, watoto wengi wa kike wanarubuniwa na mabarobaro kufanya ngono hata kama wanatimiziwa kila kitu na wazazi wao, wengine wanaharibiwa na media zisizo na maadili na hivyo kutaka ku practice kila wanaachoona, wengine wanadanganywa na houseboys na shamba boys kwa tamaa zao za kingono, wengine wanadanganyana wenyewe kwa wenyewe huko shuleni na hatimaye kufanya majaribio ya yale waliyosikia kwa wenzao.

Muhimu ni wazazi kuzungumza na watoto wao friendly kuwapa faida watakazopata kwa kutojihususha na ngono mapema, na hasara watakazopata endapo watafanya ngono mapema. Ila wasitishwe mpaka wakaharibiwa kisaikolojia.
 
Si rahisi kama usemavyo. Na si kila mtoto ana akili ya kuchanguanua mambo. Hapo ndipo umuhimu wa ukaribu wa mzazi kwa mtoto unapoonekana.
kweli kabisa na wazazi nao waangalie maneno wanayotoa midmon mwao ya kuonya....eti bora uitoe..maneno ndi yameua......yule bado mtoto tu na mwiliu nachange so wangetumia mbinu nyigineukali uiolzidi sio solution..huwa watu wanafail kisaikolojia kwa approach za wazazi wao
 
Sio siku hizi tu hata zamani....na binti kuanza hayo mambo pia ina maana kuna kitu kinalack kwa wazazi...
Yawezekana lakini mimi dadangu mmoja alikuwa kicheche tangu umri wa miaka 10 kila kitu alikuwa anapata alichokihitaji lakini kwake ngono ilikuwa kama kifungua kinywa kuliko hata majirani ambao walikuwa hawajiwezi kwa milo, mapene, imani n,k
 
Sifikiri kama hiyo ni sababu kwa walio wengi, watoto wengi wa kike wanarubuniwa na mabarobaro kufanya ngono hata kama wanatimiziwa kila kitu na wazazi wao, wengine wanaharibiwa na media zisizo na maadili na hivyo kutaka ku practice kila wanaachoona, wengine wanadanganywa na houseboys na shamba boys kwa tamaa zao za kingono, wengine wanadanganyana wenyewe kwa wenyewe huko shuleni na hatimaye kufanya majaribio ya yale waliyosikia kwa wenzao.

Muhimu ni wazazi kuzungumza na watoto wao friendly kuwapa faida watakazopata kwa kutojihususha na ngono mapema, na hasara watakazopata endapo watafanya ngono mapema. Ila wasitishwe mpaka wakaharibiwa kisaikolojia.
Kwani kukosa kitu kwa mzazi ina maana pesa tu au material things?...Upendo ni kitu kikubwa sana kwa mtoto pamoja na kumjali. Unaweza kudhani unampenda mtoto kwa kumpa pesa, mavazi na kila kitu lakini kumbe humsikilizi, akipata wa kumsikiliza huko kichochoroni lazma amvue nguo.
 
Yawezekana lakini mimi dadangu mmoja alikuwa kicheche tangu umri wa miaka 10 kila kitu alikuwa anapata alichokihitaji lakini kwake ngono ilikuwa kama kifungua kinywa kuliko hata majirani ambao walikuwa hawajiwezi kwa milo, mapene, imani n,k
Una uhakika alipata kila alichohitaji? Au alipata kila mlichodhani anakihitaji...Mtoto anakuja mtupu duniani, kila tabia inatokana na malezi.
 
Asante sana mpendwa kwa maelezo yako mazuri, ni vyema wazazi kufahamu namna ya kuwaonya watoto wao pasipo kutumia lugha kali km hiyo iliyopelekea huyo binti kujiumiza vile na mwishowe kupoteza maisha.

R.I.P
Halafu nimekumiss...
 
Una uhakika alipata kila alichohitaji? Au alipata kila mlichodhani anakihitaji...Mtoto anakuja mtupu duniani, kila tabia inatokana na malezi.
Upo sahihi sana maana nakumbuka kulikuwa na jirani yetu alikuwa mkali sana kwa binti yake na akatangaza kuwa anatembea na bastola asimkute kijana yeyote amesimama na binti yake lkn haikuwa sababu ya binti kutomegwa, aliendelea kugawa kwa siri kwa kwenda mbele, wazazi wanapaswa kuwatreat watoto wao friendly ukitumia nguvu ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom