Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 1,743
- 4,270
Nimesikitishwa na habari ya mtoto wa miaka 13 wa Kisumu Kenya aliyefariki akijaribu kutoa ujauzito wa wiki nne. Binti huyo alitumia kining'iniza nguo (Hanger) kujaribu kutoa mimba yake na kupelekea mfuko wa uzazi kuharibika vibaya iliyopelekea kuvuja damu nyingi na mwisho kusababisha kifo kwa binti.
Kifo cha huyu binti kimeniuma sana hasa niliposoma na kugundua kuwa chanzo cha kadhia yote hiyo ni uoga tu kwa wazazi wake. Wazazi walishamuonya binti kuwa akipata ujauzito ni bora autoe na si kwenda nao nyumbani kwani wangemchuna ngozi akiwa hai.
Maneno hayo ya wazazi yanaweza kuchukuliwa kwa wepesi, au kuonwa ni vitisho tu vya kawaida ili mtoto asikosee lakini ni mazito na naamini yalimuingia akilini vilivyo binti hadi kupelekea kutumia njia katili kwake yeye na kwa kiumbe chake ili tu kujinusuru.
Wazazi, mimba yaweza kuwa ni aibu kwenu lakini mtoto akishazaliwa hakuna atakayekumbuka tena ile aibu. Mtoto wako akijiua kwa jaribio la kutoa ujauzito itakusumbua maisha yako yote, itakuwa ni aibu ya milele kwako na kumbukumbu ya mwanao itakuwa imeharibika kwani atakumbukwa kama "yule binti aliyefariki akijaribu kutoa mimba".
Sisemi tusiwaonye watoto wetu kuhusu suala hilo ila tuwe na uchaguzi mzuri wa maneno tuongeapo na watoto kwani akili zao haziwezi kuchanganua vizuri kauli kama watu wazima. Tuwaambie faida watakazopata kwa kujitunza kwao na thamani yao na maisha yao. Tuepuke kauli za vitisho vilivyopitiliza kwa watoto yasije tukuta makubwa tukajuta.
Ni hayo tu.