Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,317
- 14,233
Poleni na majukumu yenu ya kulijenga Taifa Wazazi wenzangu!
Kama mada inavyojieleza, kuna huu utaratibu wa Wazazi kuwatumia Boda boda kuwapeleka Watoto wenu shule asubuhi na kisha jioni kuwarudisha nyumbani. Ndugu zangu muwe makini nao katika suala zima la usalama hasa namna ya uendeshaji wa pikipiki hata kama mnawaamini lkn chunguzeni spidi yao.
Leo asubuhi nimeona jamaa wawili Bodaboda wakiwapeleka Watoto shule kwa spidi kali, huyu wa kwanza amembeba mtoto wa kike, umri kama miaka mitano amevaa hijabu amempakiza nyuma, spidi anayoenda nayo kwakweli sijapendezewa nayo. Wa pili amebeba mtoto wa kiume, huyu amempakia mtoto kwenye mbele ya tanki la pikipiki na anakimbia sana hivyo anaua Mapafu ya yule mtoto. Kwakweli nimemhurumia sana yule mtoto.
Kwahiyo wazazi wenzangu kazi kwenu, usipomlinda mtoto wako nani wa kumthamini??.