Wazazi: Kugombana kwenye mitandao ya kijamii sio jambo jema kwa mtoto wenu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
Binadamu tupo tofauti kutokana na malezi tofauti ambayo kila mmoja amekulia. Watu wawili wanapoamua kuwa na familia ni vizuri kila mmoja akawa tayari kumchukulia mwenzie kwa upole kutokana na tofauti zilizopo kati yao.

Kitendo cha mzazi mwenzie na nay wa mitego kuandika mitandaoni na kumtukana nay kwa kutotoa huduma za malezi ya mtoto hakikuwa kizuri kwa yeye kama mzazi. Hata kama wana matatizo wao kama wazazi halikuwa jambo la busara kuutangazia umma kuhusu matatizo yao kwa faida yake yeye na kwa faida ya mtoto wake.

Siku moja huenda mtoto huyo atakuja kuziona post hizo na huenda ikasababisha mtoto kujenga chuki dhidi ya baba na kuharibu mahusiano mazima ya huyo mtoto na baba yake. Mimi ni mmoja wa watu waliolelewa na mzazi mmoja lakini mzazi wangu hakunieleza wala kutangaza matatizo ya mzazi wangu mwingine kitu kilichopelekea mpaka leo mimi kuwa na mahusiano mazuri na wazazi wangu wote japokuwa hawako pamoja.

Jamani wazazi tuchague ni mambo gani yanafaa kuwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu familia zetu na ni mambo gani gani ambayo hayafai kuwatangazia wanajamii. Unapoona hupati msaada kutoka kwa mwenzako simama wewe kwa nafasi yako katika kuleta maendeleo ya familia yako hakuna haja ya kuanza kutukanana na mwenzio mpaka kufanya ulimwengu ujue ni kitu gani kinaendelea kati yenu.

Mwisho wa siku kinachotokea ni kuumizana kihisia au mwenzio kukufanyia dharau mbele ya jamii.

Maneno ya mzazi mwezie Nay wa mitego kwenye istagram

"Thats Face You Make When You See Your Ddy Jinaaaa Anakufanyia Promotions Na Kudanganya Watanzania Kama Oooh My Twiiin Sijui Nanunua Pisto https://jamii.app/JFUserGuide Off Hata Chupi Unayovaa Hajui Thamani Yake Maskeen [HASHTAG]#Yamoyoni[/HASHTAG] Nimevumilia Sana Its 5 Years Now Nimejiskia Kutapikaaa Na Nimetapikaa Am Done Mungu Wambinguni Nakuomba Unijaalie Maisha Marefu Uwezo Nizidishie Rizki..... Uzima Wa Afya Nikuleee Mwanangu Ajeee Akuone Baadae Inshallah Umekuja Kuwa Waziri Wa Nchi & Raisi Wa Nchi Then Alete Pua Yake Mamaeeee Sijui Hata Itakuwaje Mungu Akueke Uje Uone Mafanikio Ya Mwanangu Kwa Nguvu Zangu Inshallah 1 day Yes Endelea Na Drama Zako ila Plsss Shobo Na Mwanangu Sitakiiiii ( Tusi) Plssss Unapost Picha Za Mtoto Wangu Zanini (Tusi Kubwa )Shobo Dundo Zanini??? Sitaki Shobo Na Mwanangu Komaaaa Kama Ulivyo Komaaa ( TusiZito) Jeee Wababa Wanaojisifu Kama Wanapenda Watoto Wao Then Hata Hawajui Mtoto Anakula Nini Anasoma Wapi Anavaaa Nini Wapooooooo?????? Drama Nying Sana Mtandaoni Halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am Done Nilikuwa Na Dukuduku Kutoka Moyoni Ndani Ya 5Years Nimeongea Na Limetoka Ukweli Humueka Mtu Huruuu Kutwa Kucha Kuzalilisha Wenzio Yakwako Yanakushinda Fakeeeeeen Usiwafunze Wenzio Jifunze Kwanza Kwako... ( TusiZitoMpakaNashindwaKulitamka) [HASHTAG]#PlsssDonJudgeMe[/HASHTAG] - by [HASHTAG]#skynerhuni[/HASHTAG]

Majibu ya Nay wa mitego kwa mzazi mwenzie
nay wa.png

 
Kwanza kitendo cha huyo mwanamama kukubali kumvulia nguo huyo ney ambaye tayari ana watoto wengine siikumbuki idadi yake ila ni zaidi ya wawili{nilimsikia akihojiwa}wanawake tofauti kinaakisi uwezo wake wa kufikiri,aliyoyaandika hapo hayana tofauti na kilichopo kichwani mwake...mtu ana watoto wengine na wanawake wengine hujiulizi mbona hawa kawazalisha kawaacha wewe unaenda kummanulia mapaja akuzalishe.idiot!!!
 
Hao wadada wanaomzalia Nay jamn...bora wakae kimyaa maana wanajiaibisha..

Ila Nay atalipa kwa kila chozi linalowaanguka watu,,anafanya mambo utadhani hakuzaliwa na mwanamke..I bel he was raised by a single parent..Hana utu,adabu wala nidhamu.

Na sisi wanawake tuangalie pa kujilengesha mimba..outings na vihongo uchwara visitudanganye.

Ajabu utaskia kuna fala anampango wa kujilengesha kwa Nay azae!
 
Issue private hazitakiwi kuwa mitandaoni hata siku mmoja...

Wache watu watoe mapovu kuhusu nyinyi lakini ukweli mnaujua wenyewe...

Nyie ambianeni yale yaliyokuwa mazuri tu mitandaoni, mabaya na madhaifu yenu yote mnayamaliza kimya kimya...


Kama mimi na mahondaw wangu... Kamwe hatutaweza weka mabaya au madhaifu yetu hadharani kwenye mitandao hata siku mmoja.. Hata iweje... Ni kuambiana mazuri mwanzo mwisho.. Kwa ambao watakopenda kutoa povu, ruksa wacha watoe tuu, ila siyo Smart911 na mahondaw kuanza kuanika vibaya...

Love you sana mahondaw wangu...



Cc: mahondaw
 
Ila huyu Ney acha achambwee amezid kuwa sperm donor! Shenzzy kabsa kuhudumia halijui.
 
Uyo demu skyner kibongee anatukana sana ndo lugha yake,,,tho ni mtu poa,,lakin sio busara kutukana mitandaoni maana huyo mtoto hawakumpatia mitandaoni...fakeeeeeni
 
Ikifikia kwenye hatua km hii huwa naona km drama tu. Enzi hizo, babe, sweetheart, i love u n.k hazikatiki. Simu kila muda hazikatiki
lkn leo is vice versa. MAMBO HUWA NAYAOGOPA SANA
 
Huyu skyner aliolewa huku akiwa na mimba ya Nay, ndoa ilidumu siku mbili baada ya muoaji kugundua kuwa skyner ana mimba ya mtu mwingine, kabla hujamjudge Nay na mapungufu yake jiulizeni huyu mwanamke wa namna gani
 
Huyu skyner aliolewa huku akiwa na mimba ya Nay, ndoa ilidumu siku mbili baada ya muoaji kugundua kuwa skyner ana mimba ya mtu mwingine, kabla hujamjudge Nay na mapungufu yake jiulizeni huyu mwanamke wa namna gani
Ndio ujue huyo ney naye boya tu anazaa hata na yeyote bila mipango
 
Sio tu macelebrity hao,kuna watu wengi sana

Ukitaka kujua kimenuka. . Angalia status whatsapp, caption zake instagram na Facebook
 
Back
Top Bottom