Wazazi jikiteni katika malezi ya watoto

Mbaga Lazaro

Senior Member
Aug 9, 2020
132
107
Wanajamvi habarini na poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa.

Nianze kwa kuwapa kongole wazazi wote wanaotambua wajibu wao wa malezi kwa watoto wao mungu awabariki. Pili nijikite katika mada kwa kuwanyooshea kidole baadhi ya wazazi ambao wamewatelekeza watoto wao bila kuwapa mahitaji yao ya msingi. Unakuta inafika mahali mtoto anakosa support ya wazazi kiasi cha kumfanya ajiongeze kwa kuanza kujiingiza katika shughuli za utaftaji kiasi cha kushindwa kubase kwenye masomo.

Pia wapo wengine ambao wamejikuta wameingia vishawishini kwa kukosa msaada wa wazazi na hivyo kusaidiwa na watu ambao baadhi yao hutumia mwanya huo kuwarubuni. Baadhi ya watoto kwa kukosa mahitaji yao kutoka vyanzo sahihi hususan wazazi wamejiingiza kwenye mambo maovu ikiwamo makundi mabaya yenye lengo Ia kupora na maovu mengine.

Tumeshuhudia vikundi vinavyojiita watoto wa ibilisi,watoto wa mbwa , boko haramu nk.

Jambo la kushangaza baadhi ya wazazi ambao watoto wao wanapitia madhila hayo wapo ila hawajishughulishi na wengine unakuta wamejikita katika ulevi kupindukia.

Ufikapo maeneo ya mijini hususan jiji letu la Dar es salaam utashuhudia watoto wengi wapo mitaani na wakijishughulisha katika shughuli mbalimbali zisizo rasmi.Wengine wakiomba omba mitaani na jamii inashuhudia
Unajiuliza watoto hawa wanasoma sa ngapi.Watoto hawa wawapo mtaani wanajifunza mambo mengi ambayo mengine hayana afya kwao na kwa jamii.

Wapo wanaoanza hata matumizi dawa za kulevya,na pia wapo wanaofanyiwa hata vitendo vya kikatili wawapo huko mitaani.Unajiuliza huko wanapotoka jamii si inawaona,kwanini wasifanye jambo kuwaokoa watoto hawa.Watoto hawa nao wana ndoto kwanini wasisimamiwe kuzifikia.
Kwa ujumla watoto hawa hupitia magumu mengi ikiwa ni pamoja na (i)Matatizo ya kisaikolojia.
(ii)Kuporomoka kitaaluma au kuacha shule kabisa.
(iii)Mimba zisizotarajiwa/za utotoni.
(iv)Kupata magonjwa hasa STD's
(v)Kuwa na tabia zisizofaa.
(vi)Kukosa msingi mzuri kielimu kutokana na utoro au kuacha masomo.




Rai yangu

(i) serikali hasa serikali za mitaa, iwatafute na kuwakumbusha wazazi waliotelekeza watoto wajibu wao ikishindikana wachukua hatua zaidi

(ii)Jamii itoe taarifa kwa vyombo husika juu ya wazazi walio kwenye maeneo yao wanaowapitisha watoto wao katika madhila haya.
(iii)Viongozi wa dini watilie mkazo malezi kwa watoto na kukemea wazazi wenye tabia za namna hii.
(iv)Ndugu wa karibu wajitolee kuwalea watoto wanaopitia masaibu haya endapo jitihada kadha zilizotumika ziligonga mwamba.

Mwisho kabisa "mtoto ni wa jamii tushirikiane kumlea''
 
Back
Top Bottom