jje's
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 10,798
- 16,462
Kuna story moja ya kweli kabisa binti wa kazi/beki tatu alikuwa anamnywesha mtoto wa bosi wake viroba. Ni hivi mabosi ni wafanyakazi hivyo binti alikuwa akibaki home na mtoto peke yake.
Baada ya muda alipata rafiki wa kiume na wakaanza relationship. Kwa kuwa mtoto alikuwa ni kikwazo aliamua awe ananunua viroba (pombe) ili awe anachanganya na maziwa mtoto anywe alewe alale.
Majirani waligunduga tabia aya binti huyo ya kumuacha mtoto ndani kila siku na kwenda kwa wanaume wakaamua kumweleza mama wa mtoto ambaye aliamua kuweka mtego.
Aliaga kama kawaida anaenda kazini na baada ya muda alirudi na kukuta binti akimpa maziwa mtoto aliomba amsaidie kumnywesha mtoto maziwa ndipo alipogundua kuwa kuna tofauti kwani kila akimnywesha maziwa mtoto anakunja uso, akacheki ka yana moto sana lakini wapi ile aliposogolea kidogo akakutana na harufu ya viroba.
Ilibidi achukue hatua ya kumpiga sana binti ndipo alipotoa siri kuwa huwa hufanya hivyo ili mtoto alale naye afanye mambo yake na alielekezwa na mpenzi wake. Cha kusikitisha hapa sio kiroba bali alipojaribu kumpeleka mtoto hospitali kucheki afya yake aliaambiwa ubongo wa mtoto umeshaharibika.
Hivyo nawasihi wazazi wote kike/kiume tuwe makini sana na beki tatu na tupende kufuatilia maendeleo ya watoto wetu.
Tumefika mahali tunajisahau kabisa majukumu yetu na kuwaachia mabeki tatu bila kujua madhara yake.
Wote kwa pamoja tuchukue hatua na tutekeleze haya.