beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Serikali ya Mkoa wa Mtwara imesema itaanza kuwasaka wazazi ambao watoto wao wameshindwa kuripoti shuleni kuanza kidato cha kwanza mwaka huu.
Wanafunzi hao wa kidato cha kwanza wameshindwa kuripoti shuleni, huku idadi ya waliofaulu ni zaidi ya 20,000, hivyo serikali kuagiza wazazi wote waliogoma kupeleka watoto shuleni kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kukuta wanafunzi wa kidato cha kwanza zaidi ya 3,000 hawajaripoti shuleni.
Amesema matarajio ya mkoa ni watoto 20,400 na ndiyo waliyofaulu mtihani wa darasa la saba na kutakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.
Alisema hali hiyo haiwezi kuvumiliwa na kusisitiza kuwa tangu shule zifunguliwe zaidi ya wiki tatu, lakini wanafunzi wa kidato cha kwanza walioripoti shule maudhurio hayaridhishi.
Alisema asilimia 75 ya wanafunzi hao hawajaripoti shule na kusisitiza ifikapo Jumatatu ijayo, wazazi wote waliogoma kupeleka watoto shule sheria ichukue mkondo wake dhidi yao, huku akisisitiza nia ya serikali ya kutoa elimu bure ni kuona kila Mtanzania anapata elimu ya msingi na sekondari.
Byakanwa ameshawaagiza wa vijiji, vitongoji na mitaa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wazazi hao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mtwara, Germana Mng’aho, alisema takwimu zilizokusanywa na ofisi ya elimu mkoa inaonyesha kuwa hadi Januari 17, mwaka huu watoto walioripoti shule hasa sekondari ni wachache.
Alisema ofisi yake imejipanga kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mchakato wa kuwafatilia watoto wote waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza, lakini hawajaripoti unafanikiwa.
Chanzo: IPP Media