Wazawa zaidi ya 1000 wanufaishwa na mradi wa uboreshaji wa reli ya kati

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
https://www.trc.co.tz/news/pageUrl


Mradi wa uboreshaji wa Reli ya Kati wawanufaisha vijana zaidi ya 1000 wanaofanya kazi katika mradi huo unaohusisha ukarabati wa reli kuanzia Dar es Salaa – Isaka.

Mradi huo ambapo ulianza utekelezaji wake Mwezi Juni 2018, umezalisha ajira za moja kwa moja kwa vijana wa kitanzania zaidi ya 1000 pamoja na ajira zisizo za moja kwa moja kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa mradi huo sambamba na kutengeneza fursa za biashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwemo mama lishe.

Aidha, mbali na fursa za ajira na biashara zilizopatikana kupitia mradi huo wafanyakazi wanaoshiriki katika mradi wamepata fursa ya kuongeza ujuzi na utaalamu kuhusu teknolojia za kisasa zinazotumika katika ujenzi wa reli ambapo itakuwa chachu kwa taifa katika kuongeza ujuzi kwa wataalamu ambao wataendeleza ujuzi huo pindi wakandarasi watakapomaliza kazi nchini.

Mhandisi Felician Hechei ni Msimamizi wa Mradi wa TIRP Ngerengere – Kilosa amesema kuwa kazi kubwa inayoendelea katika eneo hilo ni utandikaji wa reli mpya yenye uzito wa ratili 80, urekebishaji wa mitaro makalavati na madaraja.“ Tuna takribani vijana 280 ambao wameajiriwa katika kipande hiki, kazi inaenza vizuri na kasi inazidi kuongezeka” alisema Mhandisi Hechei

Ally Ramadhani Amawe ambaye ni Msimamizi wa wafanyakazi katika Kundi la Mkata mkoani Morogoro anaeleza kuwa anapata kipato cha kuendesha familia yake kupitia kazi hiyo sambamba na kujitolea katika kulijenga taifa halikadhalika ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada za kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo inawapatia fursa za ajira watanzania.

“Kiukweli wakati naanza kazi hii sikuwa na utaalamu wowote nilianza kama kibarua wa kawaida lakini sasa hivi nimepambana katika kuhakikisha majukumu ninayopewa nayafanyia kazi kwa usahihi mpaka nimekuwa kiongozi, serikali iko vizuri na Rais Magufuli yuko vizuri” alismea Ally Ramadhani

Naye Mashaka Hamis ameeleza namna ambavyo mradi huu umemuwezesha kuendesha familia yake pamoja na kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo tangu ameanza kushiriki katika mradi huo, Hamisi amesema kuwa kupitia kazi hii ameweza kuongeza kipato na kununua kiwanja kwa ajili makazi
“Katika Mradi huu nimefanya kazi kwa muda wa mwaka na mieni minne, mambo sio mabaya nimenunua uwanja nina watoto watatu na wote wanaishi vizuri kwa kutegemea kazi hii” alisema Bwana Mashaka

Hakika Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano imelenga kuwanufaisha watanzania moja kwa moja kupitia sera na vipaumbele vya mikataba vinavyowekwa katika miradi hii katika kuwanufaisha wazawa ambapo katika mradi huu wazawa zaidi ya 1000 wamenufaika na mradi huu huku wageni wakiwa 160 kwa idadi, jambo ambalo linawatia moyo watanzania kuendelea kuchapa kazi na kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Namba ya Bure
0800110042

Tovuti
trc.co.tz

Barua pepe
info@trc.co.tz

Mitandao ya Kijamii
Twitter:
twitter.com/tzrailways

Facebook:
facebook.com/tzrailways

Instagram:
instagram.com/tzrailways

Linkedin:
linkedin.com/tzrailways

You Tube
TRC Reli TV

Chukua Tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona, Jikinge, Wakinge wengine

Ulinzi wa Miundombinu ya Reli ni Jukumu letu sote, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayehujumu

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO TRC #RELI YETU, MAENDELEO YETU, TAIFA LETU #TRCMpya
IMG-20200611-WA0027.jpeg
IMG-20200609-WA0000.jpeg
IMG-20200612-WA0003.jpeg
 
Back
Top Bottom