Wazanzibari wapenda mabadiliko kutoka utawala wa dhulma kuelekea katika uongozi wa haki na heshima, tutoke tupambane, muda ni sasa!

Hili la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalikuwa na baraka za UK, US na Israel, mimi siliafiki, kwasababu Mapinduzi Matukufu yale yalikuwa ni surprise, na yamefanywa kwa ambush, Waingereza wakaleta manowari zao mbio mbio, lakini kabla hazijafika Zanzibar, tukaungana, hivyo zikaishia Mombasa.

Why Waingereza wayatake Mapinduzi ya Zanzibar na halafu wasitake Mapinduzi ya Tannganyika wakati Nyerere alikuwa ni mcommunist wa Pan Africanism?.
P

Nyerere alikua ni mbabaishaji tu nawala hakua na madhara kwa mabeberu Zaidi ya kuwa na faida nae, Tazama yaliyomkuta Lumumba huyo ndie aliyewasumbua mabeberu.
 
Hili la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalikuwa na baraka za UK, US na Israel, mimi siliafiki, kwasababu Mapinduzi Matukufu yale yalikuwa ni surprise, na yamefanywa kwa ambush, Waingereza wakaleta manowari zao mbio mbio, lakini kabla hazijafika Zanzibar, tukaungana, hivyo zikaishia Mombasa.

P

mkuu umewahi kumsikia David Kimche?
 
mkuu umewahi kumsikia David Kimche?
Yes nimemsikia ni Mossad posing as journalist na diplomat, ameandika vitabu vingi, na alikuwepo Zanzibar siku ya Mapinduzi. Hizi ni conspiracy theories only, ma diplomats karibu wote ni hao hao, hata wa kwetu!. Ma journalists wengi pia ni hao hao!. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalipangwa na kutekelezwa na wenyewe wenye Zanzibar yao, hivyo Zanzibar ni nchi ya Kimapinduzi, ukombozi wake umepatikana kwa watu kumwaga machozi, jasho na damu, hivyo usitegemee watu waliojikomboa kwa namna hii, halafu waje wakabidhi nchi kwa "wale wale" kwa kutumia kipande cha karatasi!.

P
 
Kama unadhani sababu za viongozi wa uamsho kushikiliwa ni kuusema vibaya muungano, pole!. Naomba niishie hapa.
P


Msikilize Imani Petro , alifanywa nini Zanzibar , baada ya kufanya mihadhara ? Pengo kaja juu akatoa amri ashughulikiwe

Isikilize mpaka mwisho utaelewa hii nchi ni ya nani ?

 
Leo ni ujumbe mahsusi kwa Wazanzibari wapenda mabadiliko hususan vijana. Napenda nichukue fursa hii kuwaambia kwamba mabadiliko hayaji ghafla na hayaji katika sahanini. Mabadiliko yanapiganiwa, kwa gharama kubwa na mara nyengine kwa muda mrefu.

Ukoloni wa Kireno Zanzibar ulidumu kwa takriban karne mbili. Katika kipindi chote hicho Wazanzibari hawakuwa wamefunga mikono. Walikuwa wakipambana, wakidhalilishwa na wakiuwawa. Jambo la kutupa somo ni kwamba wazee wetu hao hawakuwa na nia ya kurudi nyuma na kusaliti mapambano ya kuung'oa utawala dhalimu uliokuwa ukiwaonea. Waliendelea kupambana hadi pale Mreno alipong'olewa kwa panga na magobore, yeye na mizizi yake kutoka katika ardhi ya Zanzibar.

Baada ya muda mkoloni mwengine Muingereza alikuja na kuviweka tena visiwa vya Zanzibar katika makucha yake kwa takriban miaka 70. Wazee wetu hawakusita, hawakuchoka, hawakurudi nyuma hawakusaliti mapambano eti kwa sababu mkoloni nguvu yake imekuwa kubwa na wao watawaliwa ni wanyonge na dhaifu. Hawakuchoka kwa sababu walikuwa na ghera ya nchi yao, thamani yao, heshima ya nchi yao. Kinyume chake wameendelea kupambana kizazi baada ya kizazi hadi pale Muingereza nae alipong'olewa.

Ujio wa Uhuru na baadae Mapinduzi ulitazamiwa kuwa na faraja kwa Wazanzibari walionyanyasika kwa miaka mingi. Hata hivyo warithi wa madaraka na utamu ulipiganiwa na Wapigania Uhuru na Wanamapinduzi walibadili kila dhamira njema ya Uhuru na Mapinduzi. Wameendeleza uonevu, ubaguzi, mateso na mauwaji kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wazanzibari bado wangali wanaishi maisha ya unyonge na kudhalikika mno.

Wanamageuzi wa zama hizi wakiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad bado hawajachoka wanaendelea na mapambano. Ni kweli nguvu ya watawala madhalimu na watesi wetu Hawa wa zama hizi ni kubwa sana ila vijana wafahamu kuwa hakuna mtawala dhalimu asie na nguvu kubwa kiasi cha kufanya atakavyo kwa manufaa yake utawalani.

Matokeo ya dhulma ya Uchaguzi wa Zanzibar wa 1995, baadae 2000, baadae 2005, baadae 2010 na hatimae 2015 ambayo ni kuporwa ushindi wetu wapinzani si kiashiria kwamba mapambano yametushinda, laa hasha! mapambano hayajatushinda kama ambavyo hayakuwashinda wazee wetu walipigana kwa zaidi ya miaka mia mbili. Hayajatushinda eti kwa sababu watawala madhalimu wamezidisha nguvu yao ya udhalimu na kubadili silaha kali na mpya kila kukicha. Hayajatushinda eti kwa sababu muda wa kuwashinda watesi na madhalimu wetu umepindukia miaka 25.

Ni kweli Viongozi wetu wa mapambano haya wamekua wakitutia moyo kwamba tuko karibu kushinda dhulma hii. Hii ndio spirit ya mapambano. Ni lazima tupeane moyo wa kushinda maana hatujalala tunapambana hivyo tunatarajia kuishinda dhulma kesho au kesho kutwa kwa uwezo wa Allah. Kwa kuwa kila Uchaguzi ni sisi Wapigania Mageuzi ndio tinaoshinda pamoja na matumizi ya Dola, hila, mbinu chafu na nguvu zote za kimamluki ni ushahidi wa wazi na sisi pia ni wabunifu wa kukabili hujuma na mikakati miovu ya dola.

Kwa wale wenye macho yanayoona vyema na aliki inayowaza kwa murua tathmini ya kila Uchaguzi Mkuu mpya kuna hatua kubwa moja au zaidi ya moja ambayo sisi tumepiga kulinganishwa na Uchaguzi uliopita. Matokeo ya 1995 na yale ya 2015 ni tofauti kabisa. Ule wa 2015 tulikuwa mbele zaidi ya hatua 100. Hivyo Uchaguzi wa 2020 unahitaji hatua za ziada kuliko pale tulipoishia 2015 ili tumalize kazi. Viongozi wetu hawana dola hawana bunduki wanatumia zaidi sayansi ya siasa na uchaguzi, mikakati na akili ya mapambano. Kwa 2015 mikakati ilisema tuishie pale. Kwa 2020 inaanzia pale inasonga katika hatua mpya za kumaliza kazi.

Vijana waliorudi nyuma katika mapambano haya eti kwa kuwa hawaoni yakifikia mafanikio wajiangalie tena kama wako sahihi. Wajiangalie inawezekana kumbe sababu hasa ya kuchelewa kufika ni nguvu yao na mchango wao katika mapambano haya umekuwa haba hivyo wanapaswa kujitutumua zaidi. Vijana waliorudi nyuma eti Viongozi wetu waliahidi hivi lakini ikawa vyengine nao wajitazame tena na wajifikirie upya kama wapo sahihi. Kiongozi wa vita hawezi kuliambia jeshi tunauliwa tunashindwa lazima atoe maneno ya kuwatia moyo wapiganaji wenzake.

Usalama wa Taifa baada ya kuona wimbi la vijana waliovunjika moyo eti kwa hoja ya kwamba waliahidiwa ushindi limekuwa kubwa nao walijipanga kuitumia fursa hiyo. Sasa kuna maandiko, kuna mijadala, kuna clips nk mitandaoni na kwengineno katika kukoleza na kudhihaki hoja hii ya kijinga eti "ahadi ya ushindi" iliyotolewa na viongozi wetu haikutimia. Wapo vijana wapenda Mageuzi walioghilibika na propaganda hii na kuivaa vifuani mwao barabara.

Ushindi wa kupiganiwa hauna ahadi, hauahidiwi bali unapiganiwa. Hizo zilizotolewa na viongozi wetu sio ahadi. Ahadi anatoa mwenye fursa mkononi. Viongozi wetu hawajashika hatamu wapo katika mapambano magumu sana hivyo hawatoi ahadi yoyote ya kutuhakikishia ushindi. Wanachofanya ni kututia moyo tuendelee kupambana bila kuchoka, hivyo tuendelee kupambana.

Uchaguzi wa Oktoba 2020 umefika. Wapambanaji ni mimi na ww sio viongozi pekee. Viongozi ni wasimamiaji na waelekezaji tu. Hivyo tutoke tupambane. Tusisubiri kuja kulaumu kauli za viongozi za kututia moyo kwa kuziita ni ahadi za ushindi. Ushindi ni matokeo ya mapambano sio ahadi.

Zanzibar bado dhulma imetamalaki. Vijana tukaze buti tupambane. Viongozi wetu wamevinjari, hawajachoka, hawachoki wapo mstari wa mbele.

2020 Zanzibar bila CCM inawezekana!

Hivi muarabu hakuwa mkoroni?
 
Back
Top Bottom