Wazanzibari wamebobea kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza. Wabara mhh!!!

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
216
500
Natanguliza shukrani zangu kwa JamiiForums kwa kazi nzuri mnayoifanya. Yaani mpaka nje ya nchi Watanzania na wasiokuwa utawakuta wanasoma na kutoa maoni katika mtandao huu maarufu. Hongereni sana.

Sasa nije kwenye mada yangu. Sisi Wazanzibari tupo vizuri sana tena sana katika lugha zetu mbili kuliko ndugu zetu wa bara ambao huchanganya na lafudhi ya kikwao. Kuthibitisha hayo sikiliza hotuba ya madam (mama) president (rais) Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Umoja wa Mataifa kwa lugha safi, nadhifu, matamshi sahihi kabisa ukizima tv (luninga) yako na ukamsikiliza utasema ni Muingereza halisi. Hiyo ni kwa lugha ya Kiingereza.

Ukija kwenye lugha ya Kiswahili ukamsiliza mwenyekiti wa baraza la wazee la Chadema majuzi tu alikuwa anahutubia wazee wenzie lakini Kiswahili kilikuwa safi, fasaha, sanifu na kinaeleweka kirahisi sana.

Sasa njoo kwa mheshimiwa Polepole, yeye naye alikuwa akizungumza mada zake kwa Kiswahili lakini kichekesho neno magharibi limemshinda kabisa anatamka mangaribi, isitoshe lafudhi yake imeingiliana na ya kikwao. Nawaomba wabara mjifundishe lugha hizi mbili mkishindwa muongee kikwenu.
 

Joe razinger

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
358
1,000
Zanzibar si kama mkoa mmoja wa bara,pili wasomi ni wachache wengi shule za madrasa ,sijui umefanya vipi research,kwenye kiswahili naweza kukubali
 

King Mbappe

JF-Expert Member
Jul 26, 2018
1,029
2,000
Wazanzibari hawahawa wanaosema kanekshen badala ya connection, skuli badala ya school?
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
7,679
2,000
Kwanza tu ulivyotumia maherufi makubwa yaonyesha kiwango chako cha elimu, chuo ukiandika essay, report, research, thesis, dissertation kwa maherufi hayo, wapata zero, sifuri.
 

Kilembwe

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
1,567
2,000
Karibu sana JF jukwaa la wazamivu katika fikra (the forum of Great Thinkers)! siku nyingine ulete mada ya maana.....
 

Latebloomer

New Member
Oct 6, 2021
4
45
Niliifuatilia kwa makini ile hotuba ya raisi Samia Suluhu katika umoja wa mataifa. Binafsi kilicho nivutia si umahiri wa lugha alio nao bali ni namna alivo mudu kuiweka tone (upole, utulivu n.k). Kumbuka huwezi kupima competency ya mtu kwa hotuba ambayo tayari imeandaliwa na kufanyiwa mazoezi mara kadhaa.

Hotuba ya Samia sio perfect reflection ya wazanzibari wote vinginevo tuamue kutanguliza mapenzi. Kwa upande wa umahiri na umilisi wa kiswahili ni sawa Wazanzibari kuwa makungwi (masters) sababu kuanzia utotoni wao ni monoligual, akati bara asilimia kubwa watu ni bi au hata trilingual kulingana na mazingira yanavo ruhusu, hivo usitegemee mtoto aliye anzia lafudhi ya kilugha then Kiswahili akawa sawa na yule aliyeogelea bahari ya waswahili maisha yake yote, lakini hii sio hoja saana sababu kuna mutual intelligibility ambapo wewe mwenyewe ulimuelewa vizuri Polepole akimaanisha magharibi badala ya Magaribi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom