Wazanzibari wameamka?

Mzee wetu unaamini tukio linaloitwa Mapinduzi kwenye makala yako linapaswa kuitwa sherehe au kumbukumbu.

Je tukio hilo ni la kishujaa au ni tukio la udhalimu.... Na je linapaswa ulitumie kama mfano wa kuonyesha waznz wameondoa tofauti zao.

Je waznz wameondoa tofauti au ni Maalim ndiye aliyeondoa tofauti alizokuwa yy na CCM.

Bila shaka kesho Maalim akijiunga na ccm. Utakuja na mapambio zaidi ya haya...
Sheikh Mohamed,
Umekuja na hoja nzuri.

Umeharibu mwisho kwa kunikejeli.
Neno "pambio," halikustahili.
 
Mohamed Said,

..Nashukuru hoja yako umeiwakilisha kama swali.

..Mwenendo wa Uchaguzi mkuu wa 2025 utatupa majibu kama kweli Waznz wameamka au la.

..Vilevile najiuliza kuhusu suala la kuwatoa kifungoni Masheikh wa Uamsho kama bado lipo, au limezimwa na ushiriki wa ACT ktk serikali ya umoja wa kitaifa.

..Zaidi, najiuliza kama ukweli kuhusu Wazanzibar waliopotezwa baada ya mapinduzi utakuja kujulikana, na familia zao kuombwa msamaha kwa yaliyowakuta wapendwa wao.
 
Ni kweli jeshi limetoka Tanganyika na vifaru, na wengine wamekodiwa kitoka Rwanda au Burundi wakapelekwa Pemba.

Wameuwa bila hata kifikiri kuwa hawa ni ndugu zetu, wameuwa kama vile wanauwa nyumbu.

Ipo siku ina mwisho

Niko naponys nchi-Maalim Seif
 
Ni kweli jeshi limetoka Tanganyika na vifaru, na wengine wamekodiwa kitoka Rwanda au Burundi wakapelekwa Pemba.

Wameuwa bila hata kifikiri kuwa hawa ni ndugu zetu, wameuwa kama vile wanauwa nyumbu.

Ipo siku ina mwisho
Acha upuuzi na habari za kuokoteza mitandaoni!
 
Usiwaamini ccm
1. Subiri uchaguzi mwingine uje utaona rangi halisi za jinamizi ccm na najisi iliyopakwa rangi ya amani kwa ghiliba.

2. SUK sio mara ya kwanza, ni ainaflani ya ufedhuli inayotumika na ccm kwa maalim na wazanzibar wanaoamini katika haki, ukweli na demokrasia halisi.

3. Kunamifano mingi sana ya udhalili wa ccm kwa wapinzani
A. CUF
B. ACT

Lakini ccm inafahamika tangu enzi zile za mwalimu
Maalimu Seif anafaham
Abdul Jumbe anafaham
Wale wa shimoni wanafahamu

Kifupi sioni jipya ila ninachhoona ni kiini macho kufubaza malengo ya kundi la maalimu Seif kuitafuta haki kamili ya mzanzibar. Kinachoonekana sasa ni ghiliba na utapeli wa kisiasa.

Ukweli utajulikana uchaguzi mkuu ujao 2025
Kabisa hapo 2025 ndo ukweli utajulikana. It's being naive believing that there will be ever a free and a fair election. Pathetic to see Seif as they say being the brides maid or playing the second fiddle, but what else can he do, umri umekwenda na ndo ya if you can't beat them join them. Inasikitisha
 
Wameamka wenyewe au wameamshwa? Kama wameamshwa, aliyewaamsha ajiandae kulala kama bado hajalala!
 
WAZANZIBARI WAMEAMKA?

Toka ilipoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ghafla Zanzibar imebadilika na kuwatia matumaini makubwa Wazanzibari.

Yanayoonekana katika mitandao ya kijamii katika maandishi, picha na sauti yalikuwa tabu hata kufikirika kwa mbali majuma machache yaliyopita.

Waliokuwa wakitazamana kama maadui kiasi cha kufikia kusababisha watu kuteswa na kuuliwa sasa wamekuwa ndugu wanaonekana pamoja wakiwa na tabasamu huku wakipeana mikono.

Hii ni faraja kubwa kwa Wazanzibari wengi ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar.

Dr. Martin Luther King katika hotuba yake ya mwisho kabla hajauawa alisema maneno haya, ''I've been to the Moutaintop and I've seen the promises land.''

Martin Luther King anasema amefika juu ya kilima na ameiona nchi ya ahadi akiwa na maana kuwa kwa yale aliyokuwa anashuhudia juu kilimani, basi huko waendako kutakuwa na nema.

Jana katika kusherehekea mapinduzi bendera za ACT Wazalendo na bendera za CCM zimeonekana katika viwanja zikipepea bega kwa bega.

Lakini binafsi lililokamata fikra yangu zaidi ni kuona video ya wanafunzi wa Muslim University of Morogoro (MUM) Chuo Cha Kiislam Morogoro wamekusanyika katika ukumbi wakisheherekea mapinduzi kwa kuimba nyimbo maarufu inayoimbwa sana katika sherehe za CCM Zanzibar.

Nyimbo hii ina umri sawa na mapinduzi yenyewe.
Haya yote yanaashiria kitu gani?

Haya yanaashiria kuwa Wazanzibari wameamua kusonga mbele katika udugu wao kwa maslahi ya nchi yao.
Ikiwa Wazanzibari wameamua kuwa kitu kimoja hii nini maana yake?

Maana yake ni kuwa Wazanzibari wameondoa uhasama baina yao.
Ikiwa uhasama umeondoka Wazanzibari wategemee nini?

Kubwa ni kuwa utakapofika In Shaa Allah uchaguzi mwaka wa 2025 halitaingia jeshi Zanzibar kutoka Tanganyika kama ilivyokuwa kawaida miaka yote wakati wa uchaguzi.

Ulazima huu hautakuwapo.

Hili nalo nini maana yake?
Hili likipatikana maana yake ni kuwa Zanzibar itakuwa imekomboka na Wazanzibari watafanya uchaguzi huru na wa haki.

Vikosi vya kukamata Wazanzibari kuwapiga na kuwatesa katika kila uchaguzi itakuwa ni ndoto mbaya ya jinamizi.
Hili likipatikana kura itapoteza thamani ya damu ya Mzanzibari.

Katika utulivu na amani visiwani nini hali ya baadae ya Ubao wa Kisonge na waandishi wake?
Labda tulitengeneze vyema zaidi swali hili.

Hii hali ya utengamano inayoshuhudiwa hivi sasa Zanzibar imewafurahisha Wazanzibari wote?
WanaKisonge na Mazombi wamefurahi?

Wapo ambao walikuwa wananufaika sana na uadui baina ya Wazanzibari na wamenufaika kwa miaka mingi kiasi jambo hili likawa kwao wao ni ajira ya kudumu.

Wakilala wanawaza Ubao Mweusi wa Kisonge wakiamka wanawaza kazi na shughuli za Uzombi.

Hawa ghafla wamejikuta hawana tena ajira iliyokuwa ikiwaingizia kipato.
Hawa ghafla wamejikuta hawa kazi ya kufanya.

Huenda, haijulikani, huenda hawa waandishi wa Ubao wa Kisonge wakatungua ubao wao na kugawa chaki zao kwa waalimu wa madrasa.
Huenda pia na Mazombi wakatupa nondo na marungu yao kwani hakuna wa kupiga wala kutesa.

Dr. Martin Luther King alisema amefika juu ya kilima na kaiona nchi waliyoahidiwa na Mungu.
Maalim Seif wanahistoria watakapokuja kumuandika watakuwa na mengi sana ya kumuelezea.

Maalim wasaidie wanahistoria kwa wewe mwenyewe kunyanyua kalamu na kuandika kumbukumbu zako kwani jina lako limetawala Zanzibar katika kipindi kirefu na muhimu sana cha historia yake.

Walter Cronkite anasifika kuwa yeye ndiye mtangazaji wa televisheni pekee ambae amepata kuwahoji marais wa Marekani wengi kupita mtangazaji yeyote wa wakati wake.

Maalim umesimama kulikabili sanduku la kura na kila rais aliyetawala Zanzibar.
Hii ni rekodi tabu kuvunjwa.

Ulimwengu ungependa kuisikia historia hii kutoka kinywani kwako.

=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']0:00 / 0:40

 
Mmeanza upumbavu wenu, kwani koo zingine hazina uwezo wa kutowa Marais?

Upuuzi mtupu na kujipendekeza.
Nisamehe ndugu yangu.Ila tunataka rais wa kuleta umoja wa kitaifa, kuzingatia maendeleo ya watu na kuheshimu katiba.
 
Back
Top Bottom