Wazanzibari waliopo nje wasaidia Mnazi mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari waliopo nje wasaidia Mnazi mmoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Feb 2, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=3][/h]

  UMOJA wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (MUWAZA) wenye makao makuu yake Denmark, umetoa vifaa mbalimbali kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja vyenye thamani ya Sh milioni 80 kusaidia sekta ya afya.


  Mwenyekiti wa umoja huo, Dk. Omar Juma Khatib alikabidhi vifaa hivyo kwa ajili ya matumizi ya wadi ya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu (ICU). Dk. Khatib alisema wameamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya afya kwa wananchi wa Zanzibar ikiwemo ICU ambayo ipo katika hali mbaya kutokana na uchakavu wa vifaa vyake.


  “Msaada huu ni kutoka kwa Wazanzibari waliopo nje ya nchi kwa ajili ya ndugu zao wa Zanzibar....baadhi ya vifaa tulivyoleta ni kwa ajili ya wadi ya wagonjwa mahututi,” alisema Dk. Khatib. Mapema akipokea msaada huo, Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Hassan Hafidh alisema msaada huo umekuja katika wakati muafaka kwani hospitali hiyo inakabiliwa na ukosefu wa vifaa mbalimbali.


  “Tunawashukuru kwa dhati umoja wa Wazanzibari waliopo nje ya nchi kwa msaada wao ambao umekuja katika wakati muafaka huku hospitali ikikabiliwa na ukosefu wa vifaa mbalimbali,” alisema Hafidh. Wadi hiyo ya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu kwa sasa ipo katika matengenezo chini ya Wizara ya Afya ambapo hivi karibuni vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda vinatazamiwa kuwekwa
   
 2. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hongereni umoja wa wazenji waishio Denmark ...
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kutoa ni moyo. Na watanganyika igeni mfano wa Znz katika kutenda mambo kama hayo sio kuishia katika pombe na michango ya harusi na kipa imara.
   
 4. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mazingira mazuri waliyowatengezea 'makafiri' wa Denmark ndiyo yamewezesha hicho. Tusubiri misaada kutoka kwa wazenji waishio Qatar.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  muulize Mh Balozi wa Tz huku balozi Ali Saleh, atakwambia mengi sana.
  Siwezi kulisemea hili.
   
 6. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Ni jambo jema

  naomba mtumie umoja huo huo msaidie na wenzenu wanaoishi Tabora, Lindi, Mtwara, Kigoma na maeneo mengine ya jamhuri yetu

  nawatakieni ubebeji mzuri wa BOX
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  yaani milioni 80 tu ndiyo zinakufanya uchanganyikiwe uanze kutukana watu, hiyo haitoshi hata kununulia gari jipya la wagonjwa....Pole sana.
   
Loading...