Wazanzibari si wachoyo, wanaogopa EPA zetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari si wachoyo, wanaogopa EPA zetu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teamo, Apr 15, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  WANAJAMII HEBU NAOMBA MUISOME HII MAKALA KWA MAKINI,i believe mtagrasp kitu fulani.Naona kweli moto wa mabadiliko umewaka


  SOURCE:RAIA MWEMA!
  KATIKA moja ya mambo ambayo hayahitaji utafiti kuyabaini ni ukweli kwamba kwa kiwango kikubwa vitu kama nishati, mafuta, madini, na rasilImali nyingine kubwa havijawahi kuwa baraka kwa Afrika.

  Tukianzia Afrika Kusini miaka zaidi ya 400 iliyopita Wazungu waliofika eneo lile walikuwa wakihangaika kutafuta hazina ya madini ambayo yalikuwa mengi tu ardhini. Walipoamua kuweka makao ya kudumu watu Weusi hawakuwa salama tena.

  Walitawaliwa kinyama wakibaguliwa katika kila nyanja ilhali mfumo ule ukiwawezesha Wazungu wachache kufaidi rasilmali nyingi za nchi ile na pia kusafirisha kwa wajomba zao ziada waliyochuma.

  Hapana shaka kwamba ubaguzi na unyama walioufanya Makaburu kwa ndugu zetu Weusi kwa karne kadhaa haviwezi kufutika, na vitaendelea kukaa katika saikolojia ya vizazi kadhaa vijavyo.

  Lakini jambo moja ni dhahiri pia kwamba miundombinu waliyoijenga Makaburu nchini Afrika Kusini na jirani yake Namibia, kwa kipindi walichokaa madarakani inabaki kama kielelezo cha tofauti ya msingi kati ya fikra za waongoza dola Wabantu na wale wa kutoka ughaibuni.

  Niliwahi kuandika kwamba unaposafiri kwenda Afrika Kusini, unabaini mara moja kwamba sasa umetoka Afrika ya Wabantu na umeingia Afrika ya Wageni. Mpangilio wa mashamba ardhini na barabara zinazopandana, bila kusahau ujenzi wa makazi yaliyopangwa kiakili, unakukumbusha pale pale kwamba Afrika unayoiona kwa wakati huo ni tofauti.

  Ukifika Afrika Kusini unaona kabisa vielelezo vya thamani ya madini na rasilimali nyingine zilizovunwa pale kwa karne kadhaa. Unaviona vimewekezwa katika miundombinu, mashamba, viwanda, biashara mbalimbali, makazi bora (kwa wenye heri walio wengi) vyuo, shule n.k.

  Vinaonekana kwa macho. Kule hautakiwi kumsikiliza kiongozi akikuhadithieni jinsi serikali yake ilivyojenga barabara kilomita kadhaa huku wakitaja vijiji ambavyo wao hawajawahi kufika. Kule mnaziona wenyewe kwa macho yenu wenyewe. Sawa zilijengwa kwa ajili ya kuwanufaisha Wazungu na uchumi wao; lakini zilijengwa, zipo. Zinaonekana. Zinatumika.

  Tukitoka Afrika Kusini tunaweza kupanda kidogo kwa jahazi kupitia Namibia hadi Angola. Kule kulikuwa na vita iliyoendelea kwa muda mrefu, tena ya kikatili kuliko maelezo. Yule jambazi aliyeitwa Jonas Savimbi akatumika kwa miaka kadhaa kuhakikisha nchi iko vitani muda wote ili almasi ya nchi ile iliwe vizuri na wajanja. Najua kimtazamo wapo wanaoamini Savimbi alikuwa mpigania haki na kadhalika. Lakini unahitajika umakini kidogo sana kumuona Savimbi katika mwanga tofauti na wapigania uhuru wengine. Wanaojua wanajua.

  Pamoja na vita kwisha bado Angola haijafikia mahala ikawa na mambo iliyoyafanya yakaonekana kwa macho kuwa yanalingana na utajiri mkubwa wa almasi na mafuta ilionao. Bado. Kuna mfuatiliaji mmoja wa masuala ya Afrika alinieleza kwamba kuna wakati kila waziri Angola alikuwa na ndege (jet) yake binafsi.

  Kwamba yakitokea mapinduzi au lolote basi anaingia yeye na familia yake wanaruka kwenda kuliko na heri ili waweze kufaidi walichochuma wakiwa madarakani.

  Tukitoka Angola inabidi tutembee kwa miguu hadi Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ndiyo, tunatembea kwa miguu kwa sababu Kongo hakuna barabara. Mobutu Seseseko (marehemu) alikuwa anatia mfukoni moja ya tatu ya fedha za mauzo ya madini yote ya Zaire wakati akiwa rais. Japokuwa alijenga uwanja wa ndege kijijini kwake Gbadolite kwa gharama kubwa, hakuweza kujenga barabara kuunganisha nchi yake. Na Kongo ambayo hutajwa kama nchi ya nne duniani kwa utajiri wa madini imekuwa vitani mara kadhaa na hakuna lolote la maana la kuonyesha utajiri wa madini ilio nao nchi ile.

  Tunaruka kwa ndege kutoka Kinshasa – usafiri wa ndege unapatika kwa wenye uwezo – kuelekea Tanzania Bara. Huku tunaambiwa kwamba Serikali bado inashughulikia ile ripoti ya Jaji Mark Bomani ambayo ilitathmini hali halisi ya Sekta ya Madini na kupendekeza namna nchi inavyoweza kunufaika zaidi kutokana na utajiri wa madini.

  Tunavuta subira uwanja wa ndege. Baadaye tunapanda ndege kuelekea Monrovia, Liberia. Kule kuna magofu mengi yenye matobo ya risasi yanayodhihirisha jinsi fedha iliyotokana na almasi ilivyokuwa ikiporwa na Charles Taylor na jambazi mwenzie Foday Sankoh ilivyokuwa ikitumika.

  Lakini tunapoamua kuelekea Sierra Leone na Ivory Coast, ambazo pia zina utajiri wa madini na mafuta tunakutana na wananchi wengi wenye mikono iliyokatwa. Wengine wana miguu iliyokatwa. Tunauliza tunaambiwa hawa walicharangwa wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Kisa? Askari wa adui walikuwa wakija na kuwauliza: Unataka tukatie wapi mikono yako, tukatie juu au viganjani?”

  Hiyo ndiyo aina ya demokrasia waliyolazimika kuishi nayo ndugu zetu wa Afrika Magharibi. Demokrasia ya kuchagua kuwa na mikono mirefu au mifupi, lakini inayokuwa imekatwa kikatili kwa panga huku ndugu na jamaa za mhusika wakiangalia kwa uchungu. Almasi, madini mengine na mafuta vilitumika kununua silaha zaidi za kuja kuendesha vita ya wenyewe kwa wenyewe!

  Tunatoka Sierra Leone tukiwa tumepanda punda. Barabara nyingi zilikwishakuwa mashimo hazipitiki. Tunashuka kuelekea Gabon, nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta na madini. Pale tunakutana na watu wanaotembea wameinama. Wamekuwa wakitawaliwa na mtu mmoja anaitwa Omar Bongo kwa miaka 42 sasa. Kwa miaka yote hiyo amehakikisha anawanyamazisha wananchi wake huku yeye akiendelea kuweka mfukoni fedha za mauzo ya madini na zile za mafuta.

  Ukienda Ufaransa unaonyeshwa misururu ya majumba na magari yake ya kifahari utaduwaa. Lakini huku nchini kwake wananchi wake wengi ni kapuku, hohehahe, mbumbumbu wazungu wa reli. Wanatembea wameinama. Miundombinu imechoka. Hakuna shule. Hakuna barabara. Hakuna maendeleo. Lakini kuna rasilimali nyingi ajabu.

  Kutoka huko hatuna haja ya kupitia popote tena. Huko tulikopita kunatosha kutufundisha kwamba ukiwa Afrika, kugundua tu kwamba sasa una madini mengi au una mafuta hakukuhakikishii kwamba kuanzia kesho nyote mtaishi katika bangaluu au mtanunuliwa Benz na kuishi kama wananchi wa Brunei.

  Tumejaribu kuonyesha hapo juu kwamba katika bara hili kuvumbua madini, mafuta, gesi au utajiri mwingine wowote si kama kupanda chombo kwamba sasa utafika uendako.

  Juzi kumekuwa na habari iliyopewa uzito mkubwa na vyombo vya habari kuhusu suala la mafuta na gesi iliyoko Zanzibar. Watanzania, hasa wa Bara, wamelichukulia suala hilo kwa mitazamo tofauti. Kwanza wapo wanaosikitika kuona ndugu zetu wa Zanzibar wakionyesha hisia kwamba katika hili la utajiri wao, piga ua, hatuwezi kuwa wamoja.

  Lakini wapo wenye mtazamo unaotokana na utafiti tulioanza nao hapo juu kuhusu utajiri wa Afrika unavyogeuka na kuwa kadhia. Kwamba ni vigumu kupata maelezo yenye mantiki ni kwa nini kila kunapogundulika mafuta, madini au utajiri mwingine hapa Afrika (ukiachilia mbali nchi kama Botswana) kunakuwa na migogoro, kadhia na karaha badala ya migololo, pazia na raha.

  Huenda kuna tofauti moja inayojitokeza kwa ndugu zetu wa Zanzibar. Na huenda utajiri wao ukaonyesha tofauti kwa watu wa Visiwa vile, endapo nyang’au wa kimataifa wazoefu hawataingiza ujanja wao katika mikataba. Kiutamaduni, ndugu zetu wa Zanzibar si walafi. Si wabinafsi. Wao huwajali ndugu zao, jirani zao, n.k. na hata hiki wanachokisema sasa, kwamba wangependa mafuta na gesi viwe mali yao wao tu, hakitatekelezeka hivyo.

  Kule Zanzibar kiongozi mkubwa wa serikali, wakiwamo mawaziri, anaweza kumkuta mgonjwa barabarani, akaamuru gari limpeleke hospitali huku yeye waziri akiteremka na kutembea kwa miguu kuelekea ofisini. Ile roho ya viongozi kuwajali watu wa kawaida, kuishi maisha yao, kufikiri pamoja nao, kuonja kadhia zao ni tunu moja kubwa inayoweza kusalimisha rasilimali za Visiwa hivyo zisitumike kwa manufaa ya wabinafsi.

  Viongozi wengi Zanzibar, kama ilivyo hulka ya watu wengi Visiwani, wanajali zaidi utu kuliko vitu. Wanajali zaidi maslahi ya umma kuliko ya mtu binafsi. Haikuwa hivyo katika nchi nyingine nilizozizitaja hapo juu. Na kama kuna nchi nyingine hapa Afrika ambayo inaweza kuonyesha kwa vitendo jinsi ilivyotumia rasilimali zake vizuri basi huenda ikawa Zanzibar. Na ninaamini kutokana na roho yao ya kutokuwa wachoyo, basi Wazanzibari hawatatuacha hivi hivi tu sisi Watanzania Bara eti kwa sababu ya mafuta na gesi. Labda wanachoogopa tu ni wana-EPA wetu wasije wakatia mkono katika mafuta yao halafu wao wakatoka kapa!
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  wala siwalaumu wazanzibari

  hili watakuwa wamefanya akili sana
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wewe tupo pamoja!
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  So am i.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  so am i.
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zanzibar! unajua mimi na wewe ni mtu na nduguye! Katika maisha yetu ya hivi karibuni nadhani umeona uhalisi wa tamaa ya viongozi wa Tanganyika. Zanzibar ndugu yangu! mimi mwenyewe sijiamini katika tanganyika yangu, kama unauwezo wa kulinda hayo mafuta yako kabla ya mkono wangu mrefu hajakufikia, jitahidi uyalinde! Sikuahidi kwamba tamaa haitanikumba, na kutumia kadi ya undugu wetu kushinda hoja zako, lakini niangaliea jichoni na unipe ukweli wangu!
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kama dhahabu, almasi,tanzanite.ni Za Tanganyika basi waacheni WAZENJ na Mafuta yao
   
 8. M

  Mtwike Senior Member

  #8
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wazanzibari wamemegewa kitu gani kutokana n gesi ya SONGOSONG?
  Leo kuna ndoto tu za mafuta, wananyemelewa!

  Kweli, usiposhiba na chako, mpokonye mwenzako!
   
 9. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  HIvi hawa RAIAMWEMA wanaiongelea Zanzibar ipi? Ni hii ya MFALME KARUME II
  ama nyingineyo? Ninaamini RAI MWAMA wanajua ukweli wa mambo Zanzibar haswa kuhusu UNYANG'ANYI WA WATAWALA unaoendelea huko na hapa wanajaribu KUSPIN kwa sababu wanazozijua wao. Zanzibar ya leo na UTAJIRI wa mafuta ni ZAHMA kubwa sana.......Laana ya MAFUTA itaimaliza kabisa Zanzibar yetu....

  omarilyas
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kusema hapa kuwa dhambi ya ufisadi ikiendelea matokeo yake si mazuri Omar nakubaliana nawewe kabisa kwa kutazama mifano mbali mbali kenya machafuko yamekubwa sababu ya ubadhirifu mkubwa uliokuwapo (ambao sijui ka umepungua), Sierra Leone the same, Thailand sasa tunaona wananchi wamechoka wanaamua kujichukulia sheria mkononi Tanzania wasipokuwa makini itakuja kutokea the same. Nanukuu mwanafalsafa mmoja wa kiislamu aliwahi sema kuwa umaskini ukikthiri huishia kuwa ukafiri yaani roho za watu huwa mbaya, mtu hajali litakalomtokea, etc jamani jamani viongozi wetu mliangalie hili kuikoa amani ya Tanzania
   
 11. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama ni kwasababu ya EPA hawa jamaa wangekuwa wamesema kama wanaogopa EPA. Kwani chokochoko siza leo hizi tangu muda mrefu wamekuwa wakija na kitu kipya.

  Mimi nafikiri hawa jamaa walifaidi sana vunono vyetu kwani wakati huo wanapewa umeme bure walikuwa wanalipa? Je hiyo miundombinu ya umeme imejengwa kwa hela gani? Si mapato ya Taifa ikiwemo madini? Sasa wao wanataka gawio katika lipi? Je hao wawakilishi wao wanapokuja kwenye bunge kazi yao ni nini? Maana hela wanakula za watanganyika ati! Au kwakuwa Wadanganyika huwa hawasemi?

  Mimi nafikiri hawa jamaa waachiwe hayo mafuta yao ila nao waondolewe tax holiday yoyote maana wakija bara kufanya biashara ni watz lakini inapokuja suala la kumiliki vitu hawa jamaa wakali kama mbogo.

  Kwani wamesahau kuwa 90% ya vitu vya muungano nivya wadanganyika? Je wadanganyika ukitoa G55 kipindi kile umewahi kusikia wanalalamika? Lakini wacha wapige kelele kwani hiyo itaamsha na wadanganyika wadai chao hapo ndiyo ngoma itakuwa tamu.

  PIA ZANZIBAR HAKUNA HALI KAMA INAYOSEMWA KWANI WATU WENGI WAMEKIMBIA NA WAKO HUKU BARA HAWATAKI KWENDA TENA KULE HASA WAPEMBA LEO HII INAKUWA KUWA HAWA VIONGOZI HATARI KABISA WANAKUWA WAKARIMU! SIDHANI ZANZIBARA HAKUFAI.
   
Loading...