WaZanzibari kutokusheherekea Siku ya Muungano. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WaZanzibari kutokusheherekea Siku ya Muungano.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Apr 24, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna fununu kuwa Wazanzibari hawatasheherekea Siku kuu ya Muungano na watakaoshiriki ni kuwaziba macho WaTanganyika ilihali ndani ya nyoyo zao si washiriki.

  Umoja wa Wazalendo, unachukuwa fursa hii kukumbushana kwamba kusherehekea siku ya msiba mkuu huu, ni kusherehekea uovu huu, kitendo hicho ni ishara ya upungufu wa uzalendo na khiyana juu ya Zanzibar.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ila mimi kubwa linaniuma ni kwa nini kuna tofauti kubwa sana kati ya mishahara ya wafanyakazi wa SMT na SMZ?

  As long as hii ni nchi moja basi SMT ingetoa fungu kuziba hii tofauti..maana wote ni nchi moja na Bara wana uchumu mkubwa na watu wengi!!

  Yaani ukiwa Mtanzania sekta ya umma Pemba au Mbinga basi mshahara uwe ni mmoja!
   
 3. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 340
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Haya yanatoka moyoni mwako au umetumwa?
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  lamba,

  Haya ni mawazo yangu: ikiangalia France wana Mountinique Islands kule

  Carebian, na Paris ziku zote hutoa fungu kusupport budget ya hivi visiwa!

  Hii ndo spirit nzuri ya Muungano..ili iwe rahisi kwa Mtu wa Visiwani pia kusikia yeye ni Mtanzania.

  Naongelea zile Wizara ambazo sii za Muungano kama elimu, afya n.k!
   
 5. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mmh! baniani mbaya kiatu chake dawa!
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mafuta yatajaza hilo Pengo muda si mrefu yatachimbwa
   
 7. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nawashauri wakubali tu kuwa kama ukerewe ilivyo sehemu ya Tanzania, kwani DC anayewakilisha Ukerewe au mkuu wa mkoa wa Rukwa halipwi tofauti na DC wa ilala au mkuu wa mkoa wa arusha.
   
 8. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi ni machungu kuikosa ZANZIBAR
   
 9. s

  sikukuu Member

  #9
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila mimi kubwa linaniuma ni kwa nini kuna tofauti kubwa sana kati ya mishahara ya wafanyakazi wa SMT na SMZ?

  Hebu nisaidie kidogo rafiki kuna tofauti ipo katika mishahara ya Wazanzibari na Wa Tanganyika?
   
 10. S

  Stone Town Senior Member

  #10
  Apr 25, 2009
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asalamu alaykum.

  Katika kosa kubwa watanzania tunapokosea ni hapa tnapojadili kitu kwa jazba na mwisho tunakosa pa kushika yaani utaona hoja inaingizwa humu ni nzuri lakini kila michango inavyokwenda ndivyo inavyokuwa mbaya kutokana na kupoteza maana na uhalisi wa mjadala wenyewe mimi naamini hakuna haja ya kuweka chuki za kitanzania na kizanzibari ingawa hilo ni gumu kulizuwia katika nyoyo zetu lakini inatubidi tujaribu sana kujadiliana bila ya kugombana ili tufike pahala tujivunie kuwa sote ni wamoja na lengo letu tunataka maisha mema na yenye udugu na mshikamano na sio mtengamano.

  hoja ikiletwa inayohusu suala la zanzibar watu wanaripuka sana tena kwa hoja za kishabiki na chuki nadhani tufike pahala ndugu zangu tujaribu kuondokana na haya hasa kwa sisi vijana hatupaswi kujadiliana na tusikubaliane nadhani tujadiliane lakini tukubaliane pamoja na hoja zetu kama zitakuwa ni moto lakini sote tulenge katika kutengeneza hilo ni ombi langu kwa vijana wenzangu wa leo.

  kila la kheri.

  kwa kusaidia tu mshahara wa kiwango cha chini wa SMZ ni 60,000
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Stonetown ndugu yangu vipi unaendeleaje?? Pole kwa kuuguza mguu: tunakuombea hapa upone haraka!
   
 12. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole sana kwa kufilisika kimawazo.
   
 13. stanluva

  stanluva Senior Member

  #13
  Apr 25, 2009
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa mawazo yangu nadhani kuna haja kuukaa chiini na kuzungumza tutafanikiwa! Nafikiri wazenji wanaona wanatawaliwa na Tanganyika! Sasa kama tume fikia kusheherekea miaka 45 ya uhuru ni upande mmoja tu ndiyo unasifia mafanikio ya uhuru huo na mwingine una ugulia mafanikio hayo sure there is a problem! Let's sit down tujiulize nini cha kurekebisha {kinacho kereketa}
  Pia wakati mwingine nakuwa na maswali ya sio na majibu labda wana JF mtanisaidia, kuwa nilisikia jana jioni waziri mwenye dhamana akisema mambo ambayo yana shughulikiwa na SMZ na SMT! Akisema ".........haya yanashughulikiwa na Serikali ya Zanzibar na .......haya yana shughulikiwa na Serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania....." Sasa swali langu ni, Je mambo ya nayo shughulikiwa na Serikali ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania ndio yamebeba dhamana ya serikali ya Tanganyika ya wakati huo? Kama ndio, kwanini? "kwakuwa na huu pia ni muungano wa nchi mbili"
   
 14. S

  Stone Town Senior Member

  #14
  Apr 25, 2009
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  asalamu alaykum.

  hili la wazanzibari kutosherehekea muungano limetangazwa wapi mbona mie sijasikia hii habari kwenye vyombo vya habari au katika mabaraza na nani anaweza kutoa amri hiyo na ikasikilizwa? hivyo kweli suala hili linaweza kuwa kweli haiwezekani kabisa.

  Na uthibitisho wa hayo maneno yangu kwamba hakuna kitu hicho wazanzibari watasherehekea kikamilifu muungano kwanza kwa namna tofauti tayari kuna kundi kubwa limeshatoka huku zanzibar na kuja huko tangayika na viongozi wa kitaifa wote watahudhuria na huku zanzibar kuna maadhimisho hayo kwa kufanyika makongamano tofauti hivi sasa ninavyokwambia kuna kongamano linaendelea mchana mzima lililoandaliwa na jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu linafanyika katika chuo kikuu cha zanzibar (SUZA) na kesho pia kuna kongamano jengine lililoandaliwa na chama cha wananchi (CUF) na wananachi kadhaa wanashiriki na kutoa michango yao.

  mchana mwema
   
 15. moza

  moza Member

  #15
  Apr 25, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani kubnwa tuchech which are the union matters,tukizichambua kwa kina tutajua kama na sawa kutosherehekea or not
   
 16. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Message, sent!

  Mie nimefilisika ila wewe, mawazo yako yanashabihiana na jina lako. Kwakuwa husomi katika ya misitari ndio taabu yako! Ujumbe ni kuwa Tanzania na Zanzibar ndani ni nchi 2 tofauti zenye uchumi usiofanana. Kuondoa hiyo tofauti, posti yangu ina maana ni kuwa na muungano wa serikali moja, ili zanzibar iwe mkoa kama ilivyo mikoa mingine!
   
 17. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kamando dr salim bin amour bin jumaa atakuwepo katika sherehe hizi hapa tanganyika?
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  zanzibar hakuna chombo huru cha habari kusemea mambo ya kawaida ya wananchi, fanya hivi, kama ushapata nafuu, tembea mitaani uwaskilize wananchi wa zanzibar wanavyosema. ni kweli,kuna mino'ngono ya chini kwa chini hata katika maskani za CCM, hawataki hata kusikia mambo ya sherehe.
   
 19. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  It is one thing to critic the union, but it is dangerous to influence predictions! Common, let not make serious matter's topic of free guessing as in the process you might plant bad seeds
   
 20. J

  JUZAMO Member

  #20
  Apr 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa wazanzibar wengi hawautaki muungano wa aina hii.muungano ambao hauna tija wala faida yeyote kwa upande wao.wazanzibari wanaona muungano ndo unaowarudisha nyuma kimaendeleo na kuwatia umaskini uliokithiri.
  na kama utafanyika utafiti wa kweli tena usio hitaji maprofesa na ukawa huru basi zaidi ya asilimia 90 ya wazanzibari wataukataa muungano.watakao ukubali ni kile kikundi cha watu wachache( kwa uku bara tunawajua kama mafisadi tu.)
   
Loading...