Wazanzibari kuigomea sensa ni maamuzi yetu na sio Tanganyika ituingilie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari kuigomea sensa ni maamuzi yetu na sio Tanganyika ituingilie

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Califgoban, Aug 9, 2012.

 1. C

  Califgoban Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Sensa ni zoezi la kuhesabu pamoja na mali zao na mambo mengine ya msingi ili kuweza kuipa nafasi Serikali ipange mipango na mikakati mbambali ya maendeleo kwa jamii kama vile ya uchumi, afya, kielimu nk. Ni hatua moja muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa lolote lile duniani.

  Narudi tena kwa mara nyengine ili basi niweze kwa uchache kupitia jukwaa hili la Jamii Forum kuwakumbusha Wazanzibar wenzangu juu ya suala la sensa ambalo kwa namna moja au nyengine limeonekana kuwa na ajenda nyingi za siri zilizofichwa ndani yake kwa lengo zima la kutaka kuipa tena nafasi jamii fulani ya Imani fulani nchini hapa iweze kutekeleza malengo yake kwa ufanisi zaidi maana katika hali isio ya kawaida inaonekana mwelekeo wa Imani hio sasa iko MASHAKANI NA KITANZI KINAZIDI KUIKAZA SHINGO YA IMANI YAO KIMASLAHI.

  Kwa upande mwengine, Waislamu, nao waomeonekana wazi kutumia zoezi hili Sensa kuitunishia Serikali misuli kwani bila ya utafiti wa kina utaona jinsi ilivyojiegemeza kwenye upande dini ambayo ndio inayo-iongoza UISLAM katika kila Wizara na Idara Seerikalini, kutokana hali hii na ikiwa ni katika kuwaridhisa zaid UPANDE HUO PENDWA, Serikali imeamua kukiondosha kipengele cha kuwahesabu watu kwa mujibu wa DINI zao ili kisiwe ni sehemu ya Zoezi la Sensa lakini huo huo kiwekwe kipengele cha kuhesabu NYUMBA za ibada kwani kwa kupitia nyumba za Ibada wana UHAKIKA wanazo nyingi kuliko MISIKITI kwani jamii yote ya Waislamu haichagui msikiti wa kufanyia Ibada zao eti kwa sababu ya Madhehebu yao, tofauti na upande wa pili ambao wao lazima ufanye ibada kulingana na imani ya kanisa lako kama ni kakobe au kanani basi iwe humo. Hapo ajenda yao baada ya Sensa kwisha ni kusema kwa vile nyumba zao ni nyingi kuliko Waislam basi ni wazi na idadi yao ni kubwa kuliko Waislam. Kwa hili Waislam Amkeni..! Msilale..!!

  Ndugu zangu Wazanzibar sisi kwa asilimia 99.9 ni Waislamu ni jambo la wazi wala halihitaji utafiti kwani Mizengo alikiri hivo Bungeni majuzi tu kama mnakumbuka alipomjibu yule "MHARIBIFU, MCHAFU WA MAADILI". Kwa sababu hii sisi hatuna haja ya kuwa woga na wasiwasi na hizi MBINU CHAFU za wenzetu, ni laziwe tuwe macho MARA MBILI HATA ZAIDI tusije tukaingizwa katika mtego wa Waislamu wanafiki wa Tanzania Bara, hawa hawana umoja wa mshikamano katika kudai haki zao huku na wao ni rahisi sana KUGAWANYWA na kupigwa MAPANDE ndani ya misikiti, katika Taasisi Zao Kiislam na kweningineko. Hebu Wazanzibar angalieni hivi sasa kuna makundi mangapi tayari yameshajitokeza juu ya Suala hili la Sensa ndani ya Waislamu wa T,Bara? Kuna kundi la Bakwata,
  kundi la Ally Baseleh nk hali hii yote inaonyesha UDHAIFU wa Waislamu T,Bara pale wanapodai haki zao kwani bila ya kuficha wa hawa wanaweka mbele MASLAHI yao kuliko Uislamu. Lengo la kusema hivi ni kutaka kuwaambia kinagaubaga eti Waislamu wa T,Bara wanataka wapate kuugwa mkono na Waislamu wa Zanzibar katika suala hili la Sensa ili tuigomee kwa kuwasaidia wao mpaka pale serikali itakapo rejesha Kipengele cha Dini kwenye Sensa 2012. Hizi ni njama zisizo chembe ya UKWELI ndani yake na Sisi Wazanzibar tusijiuze kwa bei rahisi kwa UNAFIKI wao huu.Sisi tuna madai yetu maalum na ya msingi kweli kweli kipindi hiki na tuwaepuke waislamu wa aina hii kwani NGUO YAO KUBWA NI UNAFIKI. hawa ni watu hatari sana katika jamii ya kiislam na hata Uislam hushindwa kusonga mbele kwa kuweka mbele Maslahi yao.

  Sisi wazanzibar tusiiamuliwe mambo yetu na WATU WAISLAMU HAWA HATARISHI, sisi tuna hiari yetu kama tunahisi tuna sababu zetu za msingi basi tutaigomea SENSA na kama hatuoni sababu ya msingi basi tutashiki kama kwani haya ni maamuzi yetu kama Waislamu wa Wazanzibar.

  Kuna sababu za msingi za Wazanzibar kutowaunga mkono Waislamu wa T,Bara, na hizi zifautazo ni baadhi hizo kwa UCHACHE tu:-

  1. Kama wanataka waungwe mkono na Wazanzibar basi kwanza wangeungana mkono wao kwao kwanza
  2. Hakuna dhamira ya DHATI walio-ionesha Waislamu T'Bara katika kugomea sensa 2012.
  3. Hata Waislamu wa Zanzibar wakiunga mkono, basi lengo halitofikiwa kwa vile waislam wengi T'Bara hawaonyeshi kuigemea Sensa. Jee waislamu karibu milioni 1 na nusu Zanzibar watafua dafu mbele ya Watu karibu milioni 50 na wengi wao wanashiriki Sensa?
  4. Bado hatujawahi kuona juhudi za Waislam T'Bara kuisadia Zanzibar kisiasa ijikwamue na makucha ya Mkoloni mweusi kwani hivi juzi tu Waislamu wa BAra walishirikiana na Kanisa kulaani vikundi vya kiislamkutokana na machafuko yalitokea hapa wakati msingi wa kutokea kwake sio Waislam wahusika wanajulikana?
  5. Sensa ya Zanzibar ni kwa ajili Wazanzibar na sio T'Bara na idadi ya watu wake itakua ni kwa ajili ya Zanzibarkila upande una watu wake wa kuhesabiwa, msichanganye vitu ambavyo ni "UNPAIRED"

  ZANZIBAR DOWN! DOWN! WITH TANGANYIKA!!!
   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mmeanza

  Waislamu wa Zanzibar v Waislamu wa Tanzania Bara: Mkimaliza hilo, litafuata

  Waislamu wa Unguja V Waislamu wa Pemba, halafu baadaye

  Waislamu wa Zanzibar v Waislamu wa Oman and Finaly

  Sunni v Shia, Dhambi ya ubaguzi ni mbaya!
   
 3. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Uamsho......VS Bakwata....
  Kamati ya Misikiti VS ....
   
 4. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Usitufundishe maana ya SENSA twaijua na ndio maana tutaheshimu ili kuona mazuro yake. Wewe usiejua goma wew na familia yako ila hata yule mwanao atakutoroka akahesabiwe kwa manufaa yake kwani wewe unakaribia kuiacha Zanzibar (Kufa) hivyo unawahadaa wanaokuja kukulia hapo wewe ushakufa kitambo.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huku UK kuna waislam wa Pkistan vs wengine kutoka Afrika!
   
 6. C

  Califgoban Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Mnaotaka kuleta hoja basi ni HOJA na sio kumleta mtu mmoja mmoja, kikundi au taasisi fulani kwani huo mchango wa hoja.

  Nawatahadharisha wale wote mnao onyesha NIA ya kutaka kuipindisha HOJA hii TAKATIFU.!!

  Mungu awaongoze mchangie kwa haki.
   
 7. STALLEY

  STALLEY JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Uchochezi usio na kichwa wala miguu mi sioni sababu ya kugomea sensa.sensa ni kwa matumizi ya serikali kupanga mipango kwa wananchi wake bila kubagua dini yeyote
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mada imepotea njia - kwa vile ni ya uchonganishi ipeleke Radio Iman wataichangamkia. Na kama ni lazima JF basi ipeleke Jukwaa la Dini.

  Mada hii ni Sumu, ni Aibu kwa Uislamu, dini ya Amani, Mapenzi na Umoja! Haya ndiyo mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W)?
   
 9. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mtoa mada,
  Nimeuliza sana hili swali lakini sijawahi kusaidiwa.
  Hivi nyumba za ibada ni Kanisa na Msikiti tu? Kwenye dodoso la sensa wanataka kujua tu nyumba za ibada kwenye eneo husika au wanataka kujua kabisa kuna kanisa/msikiti etc mingapi katika eneo husika? Tafadhali nisaidie...
   
 10. k

  kiwososa JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,083
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Dhambi hiyooooooooo....... dhambi ya kubaguana inaendelea kufanya kazi yake. Mnafikiri Mzee Nyerere alikuwa mjinga??!! alishaona tangu mapema wenzetu wa dini fulani wana kalaana flan hivi ka kubaguana baguana hata wao wenyewe kwa wenyewe.
  Acheni hizo bana tufanye kazi na kujadili namna ya kukwamua taifa letu kwenye huu mdororo wa uchumi na umasikini uluokithiri kwa watanzania
   
 11. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mtoa mada,
  Nimeuliza sana hili swali lakini sijawahi kusaidiwa.
  Hivi nyumba za ibada ni Kanisa na Msikiti tu? Kwenye dodoso la sensa wanataka kujua tu nyumba za ibada kwenye eneo husika au wanataka kujua kabisa kuna kanisa/msikiti etc mingapi katika eneo husika? Tafadhali nisaidie...
   
 12. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  waacheni wakimaliza hili wataanza kubaguana uzanzibari wao kwa rangi.....
   
 13. tigana

  tigana Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Acha uvivu wa kifikra
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,977
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  mkuu, hapa utauliza sana hili swali...hutopata jibu, labda anam-consult mwanasheria mkuu, Werema amasaidie kujibu.
   
 15. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kama HOJA TAKATIFU. Wamombasa nao wanataka kujitenga na Kenya na wanavijimambo vya ajabu ajabu na kitoto kama hivi vya zanziba. Nachelea kusema hawa watu wavisiwani wanatatizo la kimsingi ambalo linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi. Au wameahidiwa kitu na waarabu.
   
 16. M

  Mbofu JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa waz'bar c waondoke tu kwenye muungano,hili la kila cku kulalamika ltaisha ln nyie swalaa? Eti kila wizara wanaongoza,waachen waongoze,taifa likiongozwa na nyie ttakoma
   
 17. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Hivi wazanzibar wana matatizo gani ? Ndio maana watu usema wapemba ni wakorofi sana na wana akili kidogo huku wataka na kule wataka. Ukimuuliza mpemba yeyote aliyeko bara kwenye kiduka chake kuhusu muungano utasikia haa yakheee bara wanatunyonya tunataka kupumua yakhe . Sasa mwambie basi rudi kwenu kwa kuonyesha kuwa unapinga kunyonywa atakwambia vipi tena yakhe kitumbua changu mbona watia mchanga.
  Sasa hawa watu tuwaelewe namna gani . Njia rahisi ya wazanzibar kujitenga ni kuingizana kwenye mashua na kwenda zenu msije bara na sisi tusije huko mtakuwa muungano mmevunja. Lakini huku mwataka na kule mwataka vipi yakhe
   
 18. m

  mfumo JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Califgoban,

  Nimesoma ulichokiandika. Nimekuelewa kama ifuatavyo; 1
  1. Ni mtu wa kutukuza UTAIFA zaidi kuliko UISLAMU. Unaona UZANZIBARI ni bora kwako kuliko UISLAMU wako
  2. Unawaita waislamu wa bara kuwa ni WANAFIKI, unauhakika gani na unachokisema, mimi sikubaliane na wewe hata kidogo kuwa waislamu wa bara ni wanafiki wapo ambao wanaimani nzuri hata kuliko wewe mropokaji.
  3.Nadhani huishi hapa nchini, na kama upo inaonekana hujui kinachoendelea katika sensa. Kwa taarifa yako Waislamu kupitia UAMSHO wameshatangaza kutoshiriki sensa kwa kuwaunga mkono waislamu wenzao wa bara. Sheikh faridi anaushirikiano mzuri tu na waislamu kutoka bara ( sio wa BAKWATA). Amekuwa akishiriki mikutano ya waislamu wa bara (mfano mkutano wa uzinduzi wa kupinga mfumo kristo uliofanyika diamond jubilee).
  4. Si mchambuzi mzuri wa mambo ya waislamu bali mchambuzi mzuri wa UTAIFA. Wewe hujui kuwa hata zanzibar waislamu wamegawanyika, kuna wa serikali (kina suraga) na UAMSHO. Hata hayo bara yapo kuna waislamu wa serikali (BAKWATA) na BARAZA KUU ( KIna Kundecha,ponda, kilemile nk). Je na waislamu wa Zanzibar wote tuwaite WANAFIKI kwa kuwa wamegawanyika? hawana umoja?

  Namalizia uwe makini na tabia yako ya kujali UTAIFA zaidi kuliko DINI yako.
   
 19. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  samahani kabla huyo hajakujibu, hebu nisaidie na mimi hapa kidogo tu: binafsi natatizwa na hiki kipengele cha nyumba za ibada. hivi kinahusika vipi na mambo ya maendeleo??? kama dini haihusiki na maswala ya maendeleo, hiki kipengele cha nyumba za ibada sio element ya udini kweli??? halafu ni vizuri tuishauri serikali yetu kama haitahesabu watu kwa imani zao mara hii, basi tusije tukasikia tena taasisi yoyote inatoa takwimu kwa ulingano wa imani za kidini za watu kama tulivyoona hivikaribuni tbc, idara ya utalii na ofisi ya waziri mkuuu. jiulize walizitoa wapi wakati hii nchi haina utaratibu huo????
  ingawa mnawashangaa waislamu kwenye hili, lakini kiukweli kuna haja ya serilkali na nyie mnaojifanya wajuaji wa kujenga hoja mkafafanua hizo takwimu zilipatikanaje??? msijifanye nyie tu ndo mnaojua kufikiri kuliko kina sheikh Ponda. wao pia wana logic kwenye hili.
   
 20. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,180
  Likes Received: 1,261
  Trophy Points: 280
  Kila taasisi haizuiliwi kukusanya takwimu kwa maslahi yake. Waislam wanaweza vile vile kuamua kufanya sensa ya waislamu na Dini nyingine haizuiliwi na yeyote!!
   
Loading...