‘Wazanzibari jitokezeni kwa wingi kupiga kura’

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
VIONGOZI wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania umewaomba Wazanzibari kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar, utakaofanyika Jumapili wiki hii. Viongozi hao wanaofanya ziara ya siku mbili Zanzibar ni wa vyama visivyokuwa ndani ya Ukawa vya UPDP, SAU, UDP na ADATADEA.

Ujumbe huo upo Zanzibar kwa ajili ya kuonana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Zanzibar na kuangalia shughuli za uchaguzi wa marudio. Kauli hiyo imetolewa na viongozi saba wa vyama hivyo, wakiongozwa na John Shibuda wakati walipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.

Shibuda alisema kinachohitajika wakati huu kwa Taifa ni kuona Watanzania wanaendelea kuishi kwa amani na ushirikiano, utakaotoa nafasi pana kwa wananchi wake kujikita zaidi katika uzalishaji mali badala ya kuhubiri siasa. Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vikosi vyake vya ulinzi kwa kulinda amani ya Zanzibar zaidi katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.

Shibuda aliwataka wanachama wa vyama vya siasa, viongozi na wananchi kukamilisha upigaji kura kwa amani na usalama ili lengo la kurejewa uchaguzi huo likamilike na kuleta mafanikio makubwa. Alionya kwamba si vyema wakati wa uchaguzi, wakajitokea baadhi ya watu kutaka kuchezea matokeo ya kura, jambo ambalo ni hatari na matokeo yake ni kwamba gharama za kuja kulinda vurugu ni ndogo.

Mjumbe wa Umoja huo wa Rufaa za Wananchi Tanzania, John Cheyo alisema upigaji kura siku ya Jumapili ndio njia pekee itakayotoa mwanga kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar kuamua wapi wanataka kuelekea katika mustakabali wa maisha yao ya baadaye.

Akitoa shukrani zake kwa Ujumbe huo wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar ( ZEC ) haikufanya makosa kufuta uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.

Balozi Seif alisema yapo mambo tisa yaliyoainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jecha Salum Jecha ambayo yalichangia kuvuruga uchaguzi huo wa mwaka jana na kufikia hatua ya kufuta uchaguzi na matokeo yake yote. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia ujumbe huo kwamba Serikali itaendelea kusimamia amani ili kuona zoezi hilo la uchaguzi linakamilika kwa utulivu.

Balozi Seif alisema jukumu hilo la Serikali, limelenga kuona maisha ya kila siku yanatoa nafasi kwa wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kimaisha kama kawaida kwa ajili ya kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Wakati huo huo, Wazanzibari waishio Tanzania Bara wamewataka wenzao walioko visiwani humo kutokubali kutumiwa na wanasiasa kufanya vurugu na kuvunja amani ya nchi, badala yake washiriki kwa amani uchaguzi wa marudio.

Wamesema kushiriki uchaguzi ndiyo njia sahihi na ya pekee ya kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo. Mwenyekiti wa Kamati ya Wazanzibari Waishio Tanzania Bara, Abdu Babu Mussa alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kutoa tamko la pamoja kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea visiwani humo na uchaguzi mkuu.

Alisema wao wanaoishi na kufanya shughuli zao bara, wanaamini mgogoro uliopo Zanzibar hauwezi kutatuliwa kwa kupandikiza chuki ndani ya jamii. “Tunatoa mfano wa mataifa ya Kiarabu yaliyoingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kama Libya, Misri na Syria…leo zimebaki magofu huku wananchi wake wakigeuka wakimbizi katika nchi za wazungu,” alisema Mussa.

Alisema wanaunga mkono uchaguzi wa marejeo, utakaofanyika keshokutwa kwa kuomba Wazanzibari kuwa makini. Aliwaasa dhidi ya kusikiliza wanasiasa wasioitakia mema nchi.

Mussa aliwataka wanaoshabikia vurugu na yanayotokea sasa visiwani humo, kuonea huruma akinamama, wazee na watoto ambao ni waathirika wakubwa wa vurugu. “Hata mbuyu ulianza kama mchicha,” alisema na kusisitiza wanaoshabikia vurugu kuonea huruma makundi hayo katika jamii.

Taasisi na makundi mbalimbali yametoa matamko yakieleza kusikitishwa na hali ya kisiasa iliyoko Zanzibar kwa kutoa mapendekezo mbalimbali ya kurejesha amani na utulivu. Mbali na Wazanzibari hao waishio Tanzania Bara, juzi Jukwaa la Wakristo Tanzania (TFC) pia lilikutana kujadili hali ya kisiasa visiwani humo na kuhimiza maombi kwa wananchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema ulinzi umeimarishwa kuhakikisha upigaji kura unafanyika kwa amani na utulivu. Habari hii imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko, Dar na Khatib Suleiman, Zanzibar
 
Lo! John Shibuda anaongoza Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania?
Sijawahi kusikia umoja wa aina hii halafu ukiunganishapo Shibuda bila shaka utapata SIFURI
 
VIONGOZI wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania umewaomba Wazanzibari kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar, utakaofanyika Jumapili wiki hii. Viongozi hao wanaofanya ziara ya siku mbili Zanzibar ni wa vyama visivyokuwa ndani ya Ukawa vya UPDP, SAU, UDP na ADATADE
 
VIONGOZI wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania umewaomba Wazanzibari kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar, utakaofanyika Jumapili wiki hii. Viongozi hao wanaofanya ziara ya siku mbili Zanzibar ni wa vyama visivyokuwa ndani ya Ukawa vya UPDP, SAU, UDP na ADATADEA.

Ujumbe huo upo Zanzibar kwa ajili ya kuonana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Zanzibar na kuangalia shughuli za uchaguzi wa marudio. Kauli hiyo imetolewa na viongozi saba wa vyama hivyo, wakiongozwa na John Shibuda wakati walipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.

Shibuda alisema kinachohitajika wakati huu kwa Taifa ni kuona Watanzania wanaendelea kuishi kwa amani na ushirikiano, utakaotoa nafasi pana kwa wananchi wake kujikita zaidi katika uzalishaji mali badala ya kuhubiri siasa. Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vikosi vyake vya ulinzi kwa kulinda amani ya Zanzibar zaidi katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.

Shibuda aliwataka wanachama wa vyama vya siasa, viongozi na wananchi kukamilisha upigaji kura kwa amani na usalama ili lengo la kurejewa uchaguzi huo likamilike na kuleta mafanikio makubwa. Alionya kwamba si vyema wakati wa uchaguzi, wakajitokea baadhi ya watu kutaka kuchezea matokeo ya kura, jambo ambalo ni hatari na matokeo yake ni kwamba gharama za kuja kulinda vurugu ni ndogo.

Mjumbe wa Umoja huo wa Rufaa za Wananchi Tanzania, John Cheyo alisema upigaji kura siku ya Jumapili ndio njia pekee itakayotoa mwanga kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar kuamua wapi wanataka kuelekea katika mustakabali wa maisha yao ya baadaye.

Akitoa shukrani zake kwa Ujumbe huo wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar ( ZEC ) haikufanya makosa kufuta uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.

Balozi Seif alisema yapo mambo tisa yaliyoainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jecha Salum Jecha ambayo yalichangia kuvuruga uchaguzi huo wa mwaka jana na kufikia hatua ya kufuta uchaguzi na matokeo yake yote. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia ujumbe huo kwamba Serikali itaendelea kusimamia amani ili kuona zoezi hilo la uchaguzi linakamilika kwa utulivu.

Balozi Seif alisema jukumu hilo la Serikali, limelenga kuona maisha ya kila siku yanatoa nafasi kwa wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kimaisha kama kawaida kwa ajili ya kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Wakati huo huo, Wazanzibari waishio Tanzania Bara wamewataka wenzao walioko visiwani humo kutokubali kutumiwa na wanasiasa kufanya vurugu na kuvunja amani ya nchi, badala yake washiriki kwa amani uchaguzi wa marudio.

Wamesema kushiriki uchaguzi ndiyo njia sahihi na ya pekee ya kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo. Mwenyekiti wa Kamati ya Wazanzibari Waishio Tanzania Bara, Abdu Babu Mussa alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kutoa tamko la pamoja kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea visiwani humo na uchaguzi mkuu.

Alisema wao wanaoishi na kufanya shughuli zao bara, wanaamini mgogoro uliopo Zanzibar hauwezi kutatuliwa kwa kupandikiza chuki ndani ya jamii. “Tunatoa mfano wa mataifa ya Kiarabu yaliyoingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kama Libya, Misri na Syria…leo zimebaki magofu huku wananchi wake wakigeuka wakimbizi katika nchi za wazungu,” alisema Mussa.

Alisema wanaunga mkono uchaguzi wa marejeo, utakaofanyika keshokutwa kwa kuomba Wazanzibari kuwa makini. Aliwaasa dhidi ya kusikiliza wanasiasa wasioitakia mema nchi.

Mussa aliwataka wanaoshabikia vurugu na yanayotokea sasa visiwani humo, kuonea huruma akinamama, wazee na watoto ambao ni waathirika wakubwa wa vurugu. “Hata mbuyu ulianza kama mchicha,” alisema na kusisitiza wanaoshabikia vurugu kuonea huruma makundi hayo katika jamii.

Taasisi na makundi mbalimbali yametoa matamko yakieleza kusikitishwa na hali ya kisiasa iliyoko Zanzibar kwa kutoa mapendekezo mbalimbali ya kurejesha amani na utulivu. Mbali na Wazanzibari hao waishio Tanzania Bara, juzi Jukwaa la Wakristo Tanzania (TFC) pia lilikutana kujadili hali ya kisiasa visiwani humo na kuhimiza maombi kwa wananchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema ulinzi umeimarishwa kuhakikisha upigaji kura unafanyika kwa amani na utulivu. Habari hii imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko, Dar na Khatib Suleiman, Zanzibar
Safiiii
 
Back
Top Bottom