Wazanzibar wengi wameanza kuwa na sifa za kuajirika, wapewe 25% za nafasi za ajira na sio 21%

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
kwa sasa nadhani wengi mmekuwa mashuhuda wa matokeo ya form 4 na form 6, hapo zamani ufaulu ulikuwa ni mdogo sana, si ajabu kukuta darasa zima lina division 4 na 0 pekee, Na linapokuja swala la ufaulu basi zanzibar ilikuwa ikishika mara kwa mara namba za mwisho, wazanzibar wengi walikuwa wanafeli kupita maelezo.

Ila kuanzia miaka ya 2018 matokeo ni mazuri mno kote Bara na zanzibar, Sikuhizi ufaulu umeongezeka mno, Ni kawaida sama kukuta darasa halina division 0 na 4, hata zikiwepo basi za kumulika kwa tpchi.

Ufaulu huu unaashiria kwamba sasa wazanzibari wengi wameanza kujaa vyuoni ili kusomea taaluma mbali mbali na kuhitimu huku wakiwa na sifa za kupata ajira katika fani kama uhandisi, udaktari, uhasibu, tehama, ualimu, n.k. Mimi ni shuhuda nmeona wazanzibar kibao sikuhizi katika vyuo vya huku bara, hususan kuanzia 2019.

miaka ya nyuma wazanzibari wengi sana walikuwa wanapata divisioni 0 na 4 nyingi sana kuliko mkoa wowote Tanzania, wengi wakawa hawana sifa za ajira, Walippata hizo division 4 wengi ndio hawa mnawaona polisi, jkt, jwtz, n.k

Sasa nilikuwa naona ni bora zanzibar waanze kupewa ajira za huku bara walau asilimia 25 za ajira maana hata ajira zimekuwa zikitangazwa mara chache, basi zinapotangazwa wachukuluwe wazanzibar 25% na sio 21%

Mfano zikitangazwa ajira za Tra, Bot, Nssf, Bandarini, Pccb, n.k basi katika kila watu 100 kuwepo na wazanzibar 25 na sio 21,

Asanteni sana,
 
population ya bara na visiwani ni ratio ya ngapi kwa ngapi

mgao wa ajira kwenye taasisi za Muungano baina ya Bara na Zanzibar ni 79:21....Lakini kwasababu huko miaka ya nyuma wazanzibari wengi sana walikuwa wanapata divisioni 0 na 4 nyingi sana kuliko mkoa wowote Tanzania, wengi wakawa hawana sifa za ajira na kuishia labda kujazana huko polisi na jeshini.

Ila kwa sasa nadhani wengi mmekuwa mashuhuda wa matokeo ya form 4 na form 6, kuanzia miaka ya 2018 matokeo ni mazuri kote Bara na zanzibar, Sikuhizi ni nadra sana kukuta division 4 na 0.

Ufaulu huu unaashiria kwamba sasa wazanzibari wengi wataanza kuwa na sifa za kupata ajira katika fani kama uhandisi, udaktari, uhasibu, tehama, ualimu, n.k.

Sasa nilikuwa naona ni bora zanzibar waanze kupewa ajira za huku bara walau asilimia 25 za ajira maana hata ajira zimekuwa zikitangazwa mara chache, basi zinapotangazwa wachukuluwe wazanzibar 25% na sio 21%

Mfano zikitangazwa ajira za Tra, Bot, Nssf, Bandarini, Pccb, n.k basi katika kila watu 100 kuwepo na wazanzibar 25 na sio 21,

Asanteni sana,
 
population ya bara na visiwani ni ratio ya ngapi kwa ngapi
Hio population sio kigezo, Kigezo ni nchi 2 kuungana,

wazanzibar walikuwa wachache kidogo kwenye mashirika kwasababu wengi walifeli form 4, siku hizi kufaulu form 4 na 6 limekuwa jambo la kawaida, Vijana wa kizanzibari nao naona ni wakati wao waanze kufaidi tam tam za mishahara.

Ufaulu ulikuwa ni kikwazo kikubwa ila kwa sasa ni history
 
In fact hata muundo wa cabinet ulitakiwa ufuate hiyo ratio. Rais akiwa mazanibar, basi sehemu idadi ya mawaziri kutoka zanzibar inapungua ili power ratio iwe ni proportional na population ratio.
Hayo mambo ya population mtaongea ninyi, Vijana wa kizanzibar saizi wengi wana sifa za ajira kwasababu ufaulu umeongezeka tangu 2019, Ni muda wa vijana nao waanza kuonja tam tam kidogo ya muungano,
 
Hio population sio kigezo, Kigezo ni nchi 2 kuungana,

wazanzibar walikuwa wachache kidogo kwenye mashirika kwasababu wengi walifeli form 4, siku hizi kufaulu form 4 na 6 limekuwa jambo la kawaida, Vijana wa kizanzibari nao naona ni wakati wao waanze kufaidi tam tam za mishahara.

Ufaulu ulikuwa ni kikwazo kikubwa ila kwa sasa ni history
Kigezo kisichofuata population ratio..hakitendi haki
 
Hayo mambo ya population mtaongea ninyi, Vijana wa kizanzibar saizi wengi wana sifa za ajira kwasababu ufaulu umeongezeka tangu 2019, Ni muda wa vijana nao waanza kuonja tam tam kidogo ya muungano,
kwani ufaulu wa vijana wa kitanganyika umepungua?
 
kwani ufaulu wa vijana wa kitanganyika umepungua?
Ufaulu huu umemsaidia mzanzibari mno kuliko wa bara.

Yani zamani zanibar kukita disioni 1 na 2 ilikuwa nadra sana, siku hizi wengi tu wanatusua.

Kwa bara impact yake itakuwa ndogo maana ajira ni chache kulingana na watu wengi sana watakaokuwa wanafaulu, litageuka kuwa tatizo kubwa la vijana wengi mno kutokua na ajira
 
Hio population sio kigezo, Kigezo ni nchi 2 kuungana,

wazanzibar walikuwa wachache kidogo kwenye mashirika kwasababu wengi walifeli form 4, siku hizi kufaulu form 4 na 6 limekuwa jambo la kawaida, Vijana wa kizanzibari nao naona ni wakati wao waanze kufaidi tam tam za mishahara.

Ufaulu ulikuwa ni kikwazo kikubwa ila kwa sasa ni history
jibu swali population ratio ngapi! yaan watu 59M wawe 75% halafu 1M wawe 25%?

ujinga huo
 
jibu swali population ratio ngapi! yaan watu 59M wawe 75% halafu 1M wawe 25%?

ujinga huo
Gharama ya muungano lazima ilipwe kwa namna moja au nyingine.

Bara mnachukua mikopo ya kimataifa kwa niaba ya zanibar, mnaiwakilisha zanzibar kimataifa, n.k yani kuna vitu pia zanzibar inanyonywa vingi tu.

Hio gharama ni kubwa sana huwezi linganisha na hizi ajira asilimia 21 anazopewa mzanzibar kwa sasa, ikibidi ipngezwe iwe 30% ila kwa sasa wafanye iwe tu 25%.

Hakunaga cha bure mkuu, Msubiri kuwakuta wazanzibar kila idara kwa wingi
 
Zikitangazwa zanzibar watanganyika wapewe asilimia ngapi?
Huku nchi ni ndogo, mtaijaza.

Bara ni kubwa sana, wazanzibar wanaweza kuwekwa wilaya moja tu na wasijae.

Kwani mnaumia wapi aisee, hui si muungano, au?? 😂😂
 
Ufaulu huu umemsaidia mzanzibari mno kuliko wa bara.

Yani zamani zanibar kukita disioni 1 na 2 ilikuwa nadra sana, siku hizi wengi tu wanatusua.

Kwa bara impact yake itakuwa ndogo maana ajira ni chache kulingana na watu wengi sana watakaokuwa wanafaulu, litageuka kuwa tatizo kubwa la vijana wengi mno kutokua na ajira
wacha kuleta zako mzee wangu, miaka ya 80 mimi nilisoma UDSM na msichana mmoja wa kizenji aliyemaliza na 3rd class, lakini akaishia kupata nafasi kubwa sana serikalini kuliko watanganyika wote waliomaliza naye mwaka huo.
 
Sasa wewe ulitaka iweje, Apewe mtanganyika??

Hapana aisee huu ni muungano,

Zamani, kama nikivyoandika ufaulu ulikuwa mdogo sana aisee, hata wenye ufaulu mdogo hao hapo ilibidi waiqakilishe zanzibar na hata hivyo bado walikuwa wachache.
 
Back
Top Bottom