Wazanzibar waweka ngumu kulipia umeme!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,190
671
naam ni kweli wataendelea au wakitishwa watanyauka? na nnaamini baada ya muafaka tutasikia mengi

SMZ yaigomea EWURA
na Waandishi Wetu, ZanzibarSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imegoma kutumia viwango vipya vya umeme vilivyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kwa kuwa taasisi hiyo haina mamlaka ya kuipangia bei.
Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansur Yussuf Himid, alieleza hayo jana alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kikao kinachoendelea mjini Zanzibar.

Katika kikao hicho, Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini, Ali Abdallah Ali (CCM), aliitaka serikali kueleza sababu ya EWURA kupanga kiwango kikubwa cha umeme kama hicho.

Waziri Mansour alisema Zanzibar imeamua kukataa kutumia viwango vilivyotangazwa na taasisi hiyo kwa vile vitaathiri uchumi wa Zanzibar na wananchi wake.

Alieleza kwa mujibu wa sheria taasisi hiyo inapaswa kupanga viwango vya Tanzania Bara na si kwa upande wa Zanzibar, kwa vile jambo hilo lilipaswa kufanywa na TANESCO kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).

Alisema mashirika hayo ya umeme yana mkataba wa huduma tangu Zanzibar kuanza kupokea umeme wa gridi ya taifa kutoka Morogoro, ambao unapita chini ya bahari.

“EWURA hawana mamlaka ya kuipandishia umeme Zanzibar, ndio maana hatujaafikiana katika suala la kutumia viwango vipya,” alisema Waziri Mansour.

Alieleza kiwango cha bei ya umeme kilichotangazwa na EWURA cha asilimia 168 kimevunja rekodi na kingeathiri wananchi wa Zanzibar na uchumi wake.

Waziri Mansour alisema ni jambo la kushangaza wakati Zanzibar imepandishiwa kiwango hicho, upande wa Tanzania Bara ulipandishiwa kwa asilimia 21.7.

Alisema kwa msingi huo, Zanzibar kuanzia Machi mwaka huu imekuwa ikitumia kiwango cha asilimia 21.7, badala ya kiwango cha asilimia 168, kwa kuwa suala hilo hadi sasa halijapata muafaka.

Waziri huyo alisema kutokana na uzito wa jambo hilo, hivi sasa Zanzibar imeamua kulipeleka katika mazungumzo ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi, ili kulinda maslahi ya wananchi wa Zanzibar na uchumi wa visiwani.

Kutokana na maelezo hayo, Mwakilishi wa Viti Maalum, Najma Khalfan (CUF) alitaka kujua mikakati ya serikali kuwa na umeme wa kujitegemea.

Waziri huyo alisema, mikakati tayari imekwishaanza kuchukuliwa, ikiwemo kufuta sheria ya ukiritimba ili kukaribisha wawekezaji katika sekta ya nishati Zanzibar.

Alisema hadi sasa kuna kampuni mbili, ikiwemo ya SDE ya Israel na Gold Solar Wind Management ya Ujerumani ambazo zimeonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme.

Waziri Mansour alisema SDE kutoka Israel inataka kuwekeza umeme wa mawimbi ya bahari (Wave Power) wakati kampuni ya Kijerumani wanataka kuwekeza umeme wa nguvu za jua kwa kuanzia na kuazalisha KWh 300,000 katika Kisiwa cha Pemba.

Hata hivyo, alisema kwa kuwa umeme huo kiwango chake ni kidogo utatoa huduma katika visiwa vidogo vidogo vilivyomo Zanzibar.

Zanzibar imekuwa ikipokea umeme kutoka Tanzania Bara tangu serikali ya awamu ya pili chini ya Rais mstaafu Aboud Jumbe Mwinyi, ambapo sasa inatumia kiasi cha shilingi milioni 900 kila mwezi kununua megawati 42 kwa matumizi ya Kisiwa cha Unguja, ambapo kwa upande wa Pemba wamekuwa wakitumia umeme unaozalishwa na vinu vilivyomo kisiwani humo.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wanaendelea kujadili muswada wa sheria ya kulinda haki za Tasnia na Mali za Ubunifu Zanzibar, uliowasilishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhan Abdallah Shaaban.
source tanzania daima
 
Kauli ya Dua na mimi imeniweka njia panda,tuambie ulikusudia nini kutuambia.Wazanzibar,kazeni uzi hapohapo.Mafisadi wanaotuzunguuka ni wengi.
 
Kauli ya Dua na mimi imeniweka njia panda,tuambie ulikusudia nini kutuambia.Wazanzibar,kazeni uzi hapohapo.Mafisadi wanaotuzunguuka ni wengi.

huyo dua hatusumbui, dua la kuku halimpati mwewe.

sasa tukitulia kumaliza matatizo ya ndani ni kuanagalia ni jinsi gani ya kunyanyua uchumi wetu.

na mungu ajaalie tupate njia mbadala ya nishati na tuachane na haya mambo ya kutegemea cha ndugu
 
sijakupata? unakusudia wazanzibari ni watu wa kunyonga?

Kauli ya Dua na mimi imeniweka njia panda,tuambie ulikusudia nini kutuambia.Wazanzibar,kazeni uzi hapohapo.Mafisadi wanaotuzunguuka ni wengi.

huyo dua hatusumbui, dua la kuku halimpati mwewe.

sasa tukitulia kumaliza matatizo ya ndani ni kuanagalia ni jinsi gani ya kunyanyua uchumi wetu.

na mungu ajaalie tupate njia mbadala ya nishati na tuachane na haya mambo ya kutegemea cha ndugu

Ubinafsi tu na umimi. Utaelewaje kama unasoma kama kasuku? Tehn teh ..........
 
Safi sana SMZ, haina maana kabisa kupelekeshwa na hao EWURA. Zaidi ni wakati mwingine muafaka wa kuangalia vyanzo vingine vya Umeme..

Mara ya Mwisho tatizo hili lilikuwa katika ofisi ya Waziri Mkuu.. Natumai muafaka wa bei ulifikiwa huko!

Zaidi kuhusu Zenj na EWURA bonyeza hapa
 
Ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huwezi.

Haya, na tuyasasambue. Nakubali kabisa ukizoea vya kunyonga vya KUCHINJA HUVIWEZI. Lakini kwa taarifa tu. Hivi vinavyozungumziwa vilikuwa toka mwanzo ni vya kunyonga (ndio makubaliano hayo-Umeme wa Kidatu tokea kutongoza wafadhili, feasibility study, na kulaza waya baharini wameshughulikia wenyewe znz toka Ras kiromoni "kumradhi kwa spelling" hadi Fumba znz -kwa makubaliano maalum ya wakati huo ya mtizamo na mwelekeo wa vya kunyonga), sasa kwa nini EWURA leo waje na hadithi zenye vigezo vya za-KUCHINJA. Si tungekubaliana hapo mwanzo kwamba mambo na yawe ya zakuchinja? na Tanzania-halisi ikafanya kila kitu toka Ubungo hadi Mtoni-Zanzibar.
 
Back
Top Bottom