Wazanzibar wautumie mwanya wa Samia Suluhu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuivua Tanganyika koti la muungano

Jan 22, 2014
29
56
Samia suluhu hassan, sio tu anaweka rekodi ya kuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa kwanza mwanamke lakini pia anakuwa mzanzibar wa pili kushika wadhifa huo baada ya mzee wa ruksa, rais mwinyi. Nafasi hii kibinadamu tunaweza sema ni kama bahati tu ila kwa mungu ilipangwa iwe na hakika imekua, nionavyo mimi mungu analo kusudi kumfanya samia suluhu kuwa rais wa jamhuri kwa nyakati hizi, na analo jukumu ambalo ni lazima alitekeleze kwa faida ya watanganyika, wazanzibar na muungano wao.

Utata, figisu, ulaghai na usiri wa muungano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ulianza mara tu baada ya kuungana mwaka 1964, haipingiki kwamba wapo wazanzibar na watanganyika ambao kwa namna moja au nyingine wameathika juu ya kuhoji uhalali wa muungano huu. Utata wake unaanza siku chache tu baada ya kuungana mwaka 1964.

Lakini kutokana na masrahi fiche ya viongozi wa muungano hasa wa jamuhuri ya watu wa Tanganyika walihakikisha kila ahojie juu ya muungano basi anashughurikiwa ipasavyo.

Dosari za muungano huu zinaanzia kwenye Hati ya Muungano, katika hati hii kitu kilichofanyika ni kwamba, jina la Serikali ya Tanganyika lilikabadilishwa na kupewa jina la Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Baadae tena ikabidilishwa kuwa Tanzania, na kutaka kuufuta kabisa utaifa wa Zanzibar. Wako wanaosema kuwa hiyo haikuwa sawa. Na kipindi hicho Katiba ya Tanganyika ikatumika, baada ya kurekebisha mambo machache tu, kama kubadilisha jina na bendera.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) ikabakia, lakini madaraka 11 ya serikali hiyo yalihamishwa na kupelekwa kwenye Serikali ya Muungano. Sasa, tukiweka serikali 2 hizi katika mizani, zitakuwa hazina usawa tena, kwa sababu Serikali ya Muungano sasa imekusanya madaraka yote ya Tanganyika na mambo 11 ya Zanzibar.

Watu wengi wanaamini kwa makossa kwamba, Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964, ziliunda muungano wan chi inayoitwa Tanzania. Ukweli wa mambo ni kwamba, tangu kuungana kwa nchi hizi mbili hadi miezi sita baadaye, hapakuwa na muungano wala nchi iliyoitwa Tanzania. Ndiyo kusema kwamba, muungano wan chi hizi haukuzaa Tanzania, wala Tanzania siyo muungano wan chi hizi mbili.

Kwa mujibu wa mkataba wa muungano uliotiwa sahihi arpril 22, 1964 kati ya mwalimu Julius kambarage nyerere na sheikh abeid Amani karume, na kwa mujibu pia wa sharia ya muungano, na 22 ya 1964 iliyoridhia mkataba huo kuupa nguvu ya kisheria na kutumika nchini, jina sahihi la muungano limetajwa kama ifuatavyo: jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar, kuanzia siku ya muungano na baada ya hapo, zitaungana kuwa jamhuri moja kwa jina la JAMHURI YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

Pamoja na kizungumkuti cha muungano, baadhi ya wazanzibar waliendelea kupigia kelele swala la Tanganyika kuvaa kote la muungano na kuinyima Zanzibar fursa nyingi kama ambavyo wakoloni walivyozitawala nchi za kiafrika na hivyo ndivyo Tanganyika inavyoikalia Zanzibar kwa koti la muungano.

Wazanzibar sasa kuwa na kiongozi mkuu anayetoka upande wao ni wasaa sasa wa kuyatazama upya masrahi ya Zanzibar katika muungano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Malalamiko na manung’uniko amabayo baadhi ya Wazanzibar wa upande wa upinzani na hata baadhi ya wanachama wa chama tawala juu ya muungano huu, ni fursa kwao kumtumia mama samia kupitia na kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu swala la muungano.

Muungano mfupa uliowashinda wengi, jiwe waliloliangukia wengi na wakasagika, mamba aliyewala wengi. Sasa ni kazi ya samia na wazanzibar wenzake kuhakikisha wanatatua changamoto zao na kama watatshindwa kwa kipindi hiki basi wasitegemee wakati mwingine wowote kulitatua swala la muungano.
 
Mwenzie karume alikuwa anajiandaa kuvunja muungano wakamtia shaba.

Muungano ni Mali ya Bibi wa uingereza.
 
Wazanzibar wanakula keki ya Tanganyika hawawezi kudai nchi yao, kwenye huu muungano tunaonyonywa ni wadanganyika lakini kwa vile vichwa vyetu havipo vizuri tumo tu.
 
Daah..rudi shule kajifunze kuandika vzr..hii ni aibu kwa taifa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom