Wazanzibar Wapewe Haki yao Watakavyo. Je Ni Wenzetu au Si Wenzetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibar Wapewe Haki yao Watakavyo. Je Ni Wenzetu au Si Wenzetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duduwasha, Nov 30, 2011.

 1. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Kuna kila dalili zioneshazo Kuwa Watanzania wa Visiwani Hawawapendi Wenzao Watanzania Bara na hili lipo wazi kabisa
  kwani huwa wanakuja juu sana likitokeapo jambo litatizalo na huwa wanaonesha wazi kuwa hawautaki huu Muungano wa Karume na Nyerere.. Choko choko huwa Nyingi sana na mwishowe wabara wakiona maji yamezidi Unga hugawa Nyadhifa zao uongozi kwa Wavisiwani Mifano ni Mingi Sana.

  Sasa kwa Mwendo huu hizi Nyadhifa zitatolewa hadi lini siku wakitaka kupewa hadi ardhi yao ya kimagumashi ya pwani maybe Wabara ndipo watapoamka na kuwaona hawapendwi..

  Ningeona jambo jema Tuwajue kuwa kama hawa Wavisiwani Wanatupenda au la! siku nyingi wanaomba wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni kama wanauhusudu huu Muungano au La .. It means kwa sasa wamelazimishwa kuwa nao kwani hawajisikiii kabisa haki ya Mama Kuitwa wao ni Watanzania kama huamini muulize Mtu yeyote mwenye asili ya Visiwa vya Pemba na Unguja.

  Na sie wabara Tunahitaji kujuwa kama ''Wazanzibar they are with us or Against Us''

  Mie kwangu Ningependa Kujua hili. Katiba Mpya Watanganyika kuwa Serikali Yao.
   
 2. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nashangaa wanashabikia nao wawemo kwenye muundo wa katiba mpya. hapa dawa ni kurudi kwa Tanganyika huru tu, basi
   
 3. k

  kihami Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sioni faida yoyote ya muungano zaidi ya migogor. omwenye kujua faida zake anijuze. Pls
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  faida za muungano ni nyingi mfano kuna sababu za kiuchumi, kisiasa na kijamii, na ndio maana hata nchi nyingi na sehemu mbali mbali zimapenda kutengana. na hata waswahili wanamsemo wao wanasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu


  kuhusu muungano huu wa jamhuri ya muungano, kwa kweli ni muungano ulitokana na viongozi kwa utashi wa siasa za wakati ule, kwa hio ndio maana unasumbua maana una kasoro nyingi za kisheria na wananchi wa pande zote mbili wanalalamika juu ya muungano huu kwa staili inayotofautiana. ila si kuwa ni wazanzibari tu ndio wanalalamika, bali kwa kuwa wao wanaonekana nfio wanaumia zaidi ukaona sauti yao iko juu sana


  sasa wakati umefika turudi kwa wanachi, kuwauliza jee muuungano, uendelee? na kama uendelee uwe na muundo gani? tusiogope kiwa wakweli, maana kuogopa sio kutatua tatizo bali ni sawa na kufuga maradhi na kila ukifuga maradhi ugonjwa huzidi, sasa ugonjwa ukiripuka hakuna msalie mtume ila mauti
   
 5. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwenye red nilidhani ungezitaja faida zenyewe ila umepiga filimbi tu kama wengi wanavyofanya wakiambiwa wataje faida na ningependa tuzioanishe faida za muungano huu mimi nakiri sizijui
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika tufike sehemu tuseme ENOUGH IS ENOUGH,YANI IMETOSHA IMETOSHA,na kusema UKWELI watu wazima kimri walioko kwenye madaraka wajue kizazi cha watu chini ya umri wa miaka 45 kushuka chini Muungano wetu na Zanzibar hauna faida yoyote kwao zaidi ya kwenda Zanzibar kutalii kama Mtanzania wa Bara anavyoenda Bagamoyo ambako ni Tanzania huru kwake.

  Hivi lini tulisikia Mtanzania mzaliwa wa Moshi na Mbunge wa Moshi akaenda Zanzibar kuwa Waziri au katibu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Lakini wao wakizidisha choko choko zao kidogo tu utasikia wamewagawiwa Uwaziri tena zile sekta nyeti kama Waziri wa Mambo ya Ndani,kwa maisha haya mpaka lini.

  Hivi tunajambo gani hilo zito la SIRI KUU ambayo haipo kwa faida ya umma.Manake kwa sie tulio chini ya umri wa mika 45,Tanzania ya kesho ni yetu,yani kwa mwenye umri wa miaka 45 Mungu akimpa uzima anamiaka 35 ya kutumikia Taifa kama Mtanzania mwenye ushiriki Mkubwa wa Tanzania ya kizazi kipya kijacho.

  CCM watu wazima wajue vijana wao wanaowaaanda kulithi matendo yao ya kushabikia MUUNGANO WA KIMABAVU,USIO NA TIJA KWA UMMA,BALI TIJA ZA KIDOLA NA MATAJILI WA KIDUNIA,HAWAWEZI KUJA KUSHINDANA NA KIZAZI KIPYA AMBACHO KILA SIKU YA MUNGU KINAZIDI KUWA NA UFAHAMU MKUBWA TOKA WAKIWA NA UMRI MDOGO [Kwa wale wenye watoto wadogo nyumbani wa umri wa miaka mitano mpalka nane wanaweza kuona ufahamu wa watoto hao wadogo kupitia jinsi watoto wao hao wanavyocheza na vyombo ya kieletlonia vitu kama simu,televisioni,computer games,na stimulation games zinginezo katika uwezo wa ajabu ambao hata mzazi wake mwenye hana uwezo huo]."

  Kwa sasa sio kizazi cha kulazimisha kufuata bila kuhoji,ni kizazi cha majadiliano na majibu yenye ukweli mwingi kuliko uongo usio na msingi.

  Tufike wakati kabla wazee hao hawajaondoka watuondolee utata huu,tujue moja JE WAZANZIBAR WAKO NASI AU HAWAKO NASI [ARE THEY WITH US OR NOT-ni msemo wa sauti ya kimarekani kuwambia washirika wake wanapokuwa wanataka kujua ushiriki wao].

  Kama wanzanzibar watesema wako nasi basi jibu ni Serikali moja tu,hakuna cha Serikali Tatu,wakigoma wapewe Serikali yao ya Wanzanzibar ambayo tayari wanayo wakiwa na kila kiltu soon wataomba Bank Of Zanzibar [BOZ] yote hayo kwishney nasi tuchukue Tanzania iwe yetu the game is over.

  Kwa Wanzanzibar walioko Tanzania kama Watapenda kuishi Tanzania wakane uraia wa Zanzibar wao na Watoto wao,na kwa wale watakao taka kuludi kwao Zanzibar wapewe mabegi yao kwaheri na wasitoke na chochote,unyambilis unyambilisi, kwa kuwa vyote walichuma Tanzania barana kwa wasukuma,wanyamwezi,wangoni,waha na wanyakyusa walioko Zanzibar nao masharti ni hayo hayo kama wanataka kubali Zanzibar wabaki wakiona wanatka kuludi bara fungasha beki ludi kwenu Tanzania.

  Kwa wale waliobahatika kuwa viongozi wetu wakajua siri zetu tutaishi nao kimarekani, all Eyes on Them.Tufike sehemu watu wazima wajue kuwa kizazi chetu new generetion dotcom ni aina gani ya watu hao, yani vijana kama Tindu Lissu,Nape, Zitto, Mnyika ,Mdee,na wengineo wenye akili timamu ndani ya Bunge ni wachache mno yani ni cha Mtoto mno [A Tip oga na Iceber] ya vijana wa kitanzania wenye uwezo wa kufanya maajabu kwa Nchi hii.Ukitaka kuwajua walivyo wabaya tembelea mabenki na mashrika ya umma waulize wanavyopata shida na watyu hao.Wengi baada ya kuona Nchi haileweki wameamua kuiga matendo ya wasure/madingi wazee wao nayo ni kuchota na kusepa.Lakini laiti kama wangekuwa na heshima kwenye Serikali yao nao Serikali ikatambua ikawapa nafasi hakika Nchi hii miaka kumi na tano mingi,ingekuwa Nchi ya Pilia Afrika kuendelea baada ya South Africa.

  Wapo vijana kibao uku mitaani,ebu muone Sugu,hivi watu wazima ndani ya CCM madaraka, hawajiulizi,kuhusu kijana kama huyo ambae elimu yake ni ya wastani [Kasoma Kayumba Sekondari School-ambayo ndio wengi ya vijana wa Watanzani-Akaenda Chuo Kikuu Mitaani Universty Dot Com-Chuo pekee cha Watanzania walio wengi kati ya Laki tano [500,000] wanaomaliza kidato cha sita na wanapata nafasi ya chuo kikuu ni elfu hamsini [40,000] kati ya hao laki tano].Lakini leo hii SUGU anauwezo wa kuwatuliza Watanzania Millioni na ushee wenye gadhabu na Serikali yao ambayo imewachokoza na kushindwa kuwahudumia.

  Hivyo wasitegemee kwa kupindisha ukweli wataendelea kufanikisha mahitaji yao,bali ni kuwa wamechukua bomu wakategua pin wamelishikilia mkononi huku wanakula ole wao wakipitiwa na usingizi,au wakastukizwa ghafla kama tukio la Mbeya, na kisha watu aina ya SUGU wakago,ma kukaa upande wa SERIKALI ILI KUTULIZA WATU,wakasimama upande wa WANANCHI KISHA wakafanya kuwaongoza kumsaka mmoja baada ya mmoja kwenye majumba yao na hakika RISASI ZILIZO KWENYE MAGHALA YA JESHI,MALI YA HAO AMBAO LEO HII WAMEGOMA HAZITATOSHA KUMALIZA HASIRA ZAO.TUSIOMBE KUFIKA HUKO LAKINI WAZIMA HASWA VIONGOZ WA SERIKALI KUPITIA CCM WAJUE MFUMO WA NDIO MZEE UMEKWISHA SASA.
   
 7. t

  tumpale JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni vema na haki kumshukuru mundu na wapenda haki amani, umoja, uzalendo na mshikamano kama tundu lissu, lema, dr slaa na wengine kwa kuwaamsha watanzania toka katika usingizi mnene, angalizo haki haiombwi inadaiwa.
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kwa wale wafugaji wanajua ni jinsi gani banda ulilofugia mbuzi na kondoo kwa wakati mmoja linavyokuwa.
  muungano udumu ilitushuhudie mengi.
   
 9. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  m-bara wewe na bibi yako. Sisi ni Watanganyika sio wabara!
   
 10. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  1961 kulikuwa hakuna nchi inayoitwa Tanzania ilikuwa ni Tanganyika...Jina la Tanzania liliundwa April 1964..u foolish u should learn your faken history.
  kwanini unakataa jina la taifa lako la Tanganyika? hiyo ni aibu kubwa na unawadharaulisha watanganyika wenzako wenye kupenda asili yao ya kitanganyika...wake up man, u been foolish and sold for a long time...
  Republic of Zanzibar ilikuwepo toka mwanzo wa dunia hii Na itadumu hadi mwisho wa Dunia hii na kila siku ya dunia hii Wazanzibari wanajiproud kwa furaha tele kwa kujiita wao ni wazanzibari popote pale duniani.


  [​IMG]
   
 11. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Mie Asili yangu siijui fresh ila naweza sema ni Mbantu so napozungumzia bara namaanisha kama wengine wamaanishao bara ambayo haijazungukwa na maji kama bahari au ziwa so Wahenga walishayamaliza haya wakaona waite mtu anayetokea Bara ni Mbara na wanaotokea kwenye visiwa wanaitwa wa visiwani huo Utanganyika ulishafutwa ndio maana kuna choko choko za Wengine wanaudai

  Wacha kuleta ushabiki maandazi kama kwenye Mpira. Tizama filamu ya Sarafina wa South Africa Uone vibaraka kama Wewe wapotoshaji walivyokuwa Wanafanywa....
   
 12. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye Red Ndio Sijapaelewa Watanzania Wapo macho tatizo Kuna Vibaraka wasiojulikana huwanyamazisha au kuwapoteza wale wote watakao uzungumzia huu muungano kwa undani... Ukiulizia mkataba wa muungano upande wa zanzibar aliyeuona au kuuhifadhi naomba jibu haraka nikupe zawadi.....
   
 13. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wacha kuleta ujanja wa chura ku-troti bila bukta. Hapa tz bara inasimama badala ya Tanganyika na visiwani badala ya Znz. Hakuna habari ya maji na kwa taarifa yako Afrika yote imezungukwa na maji. Na Tanganyika ina visiwa vingi tu. Leo akija mtu kutoka Ukerewe utasema huyu ni mtanzania wa kutoka visiwani?

  Mimi ni Mtanganyika, kamwe usiniite mbara
   
 14. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Pole wewe usietaka kukubalii ukweli,mimi nimezaliwa na kukuta Tanzania iweje leo unilazimishe kuishi Tanganyika japo ipo,Upuuzi huo haupo japo,yawezekana wewe ni Mzanzibar unataka Tanganyika ili upate Zanzibar.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  ..si kweli kwamba waZNZ wamekuwa wakipewa haki mbalimbali.

  ..hawa ndugu zetu huwa wanadai, na huwabembelezi.

  ..rejea mswada wa kwanza wa katiba. waliukataa, wakauchanachana hadharani, mwisho serikali ikawasikiliza.

  ..sisi wa-Tanganyika huwa hatudai, bali tunasubiri tu tukisikia waZNZ wamepewa hiki na kile basi tunanung'unika kidogo then end of the story.

  NB:

  ..fuatilia mjadala wa katiba bungeni.

  ..hakuna Mzanzibari angeruhusu mwenzake ashambuliwe na wa-Tanganyika kama ilivyotokea kwa Tundu Lissu.

  ..Tundu angekuwa Mzanzibari, na akashambuliwa na mTanganyika hata mmoja, ingesababisha hoja zake ziungwe mkono na waZanzibari wote bila kujali vyama.
   
 16. T

  Taso JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Ziiiipi?

  Zitaje!
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Soko kama maana ya watu..

  Kwenda likizo katika kisiwa chenye marashi ya karafuu..bila passport

  Eneo kubwa la ardhi (nchi) tunatisha..

  Biashara, utalii ....

  Human resource, Prof.haroub, Dr. shein n.k wanatusaidia sana kusomesha watoto wetu..

  faida ni nyingi mkuu..tuwe na serikali tatu..
   
 18. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Nenda ukaishi Mwanza ndipo utajua wakerewe wanaitwa Wavisiwani au la. Kama wewe umeweza kutamka hayo kwanini mimi nishindwe eeh? mtanzania kutoka visiwani huko ukerewe au MAFIA au Unguja au Pemba... sema haijazoeleka tu sehemu zingine

  Africa ndio imezungukwa na Maji but we are talking about Country ambayo ni Tanzania mainland na Tanzania Island hapo nadhani utakuwa umenielewa yaelekea hupendi kiswahili hayo ndio majina ya wahenga waliokubaliana kuyaita hivyo yawezekana enzi hizo walishabishana sana hadi wakafikia muafaka.

  Huo utanganyika wako uitwe je umebatizwa au? manake hiyo nchi ya Tanganyika ilishaunganishwa ikawa Tanzania.
  HAta washabiki wa Simba hawajiiti wao ni Sunderland.
  Historia inaenda Mbele and ujue you can't change history

  Hukuwahi kuwa Mtanganyika ni hukuwahi tu kama uliwahi kuwa basi uliwahi tu.

  Nadhani wewe ndio unatroti bila bukta
   
 19. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ilikuwepo nchi moja ikiitwa Russia. Ikaungana na nyingine kibao zikawa USSR aka Soviet Union. Kisha zikavunjika na Russia ikarejea. SASA ENDELEA NA MAWAZO YAKO YA UTANZANIA. Siku moja utakosa nchi ya kuishi. Heri wanaotarajia kurejea kwa Tanganyika, maana uraia wa nchi hiyo ni wao.
   
 20. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Congo Du Zaire
   
Loading...