Wazanzibar wamechachamaa wanadai talaka,nini hatma ya muungaano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibar wamechachamaa wanadai talaka,nini hatma ya muungaano?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MUSTAPHA, Apr 19, 2011.

 1. M

  MUSTAPHA Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika mjadala wa muswada wa katiba uliofanyika Zanzibar,wazanzibar waliojitokeza katika mjadala huo sio tu waliupinga muswada huo,bali walisikika wakiukataa na muungano pia.Katika fikra zao wanaamini ya kuwa wao hawanufaiki na muungano kama wanavyonufaika nao watu wa bara.Hekima na busara za kutosha zinahitajika ili kuziondoa kero za muungano.Vinginevyo,muungano upo matatani.
   
 2. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu busara hii hapa ya Mwalimu na Wazanzibari ndio wameshasema loud and clear:

  "Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu NCHI shiriki itakapoamua kujitenga" by Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Km wasemavyo makada wa chama tawala, sasa ni wakati wa kufanya maamuzi magumu, lujivua gamba kwa ccm na matakwa ya Katiba mpya kuendane na kuzaliwa kwa tanzania mpya, mawazo ya wengi yasikilizwe, KURA YA MAONI NI MUHIMU KTK KUFANYA MAAMUZI..
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kura ya Maoni?

  Tupige kura kuulizwa kama tunataka Uhuru wetu tulioporwa na Tanganyika?

  Kwani Mkuu nyinyi mliwahi kuulizwa iwapo mnautaka huu Muungano? Maana sisi hatukuwahi kuulizwa.

  Muungano huu hauna uhalali wa kisiasa na kisheria, uvunjike tu.

  Baada ya hapo na kama tutakubaliana, tutatafuta njia nyengine ya kushirikiana kwa misingi ya kuheshimiana.

  Zanzibar for Zanzibaris.
   
 5. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
 6. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Katika mchakato kueelekea katba mpya suala la mhungano litleta utata sana. Lingine ni dini. mengine yataenda vizuri tu. Basi sote tujiandae na hali hiyo.
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili nalo FUPA jingine kwa JK....

  Jamani Wazanzibar kuliko kulalamika na kutishia nyau, nyie fanyeni kweli.......tekelezeni ushauri wa Mwl. timueni

  Mwanzoni binfasi nilitamani tungeendelea kuwa kama nchi moja kwa mwamvuli wa muungano lakini kwa sasa nimekana mtazamo huo kwa asilimia 500% na nawaunga mkono mtimue kabisa....!!!!

  That is better, at least to say, for you kwani hakuna kitu muhimu kama mtu kujisikia kuwa salama na soveereign inayompa kuweza kufanya mambo yake mwenyewe hasa anapojitambua anaweza kufanya hivyo.....

  Kama mtoto wa kike amekuwa anataka kwenda kuolewa mkimchelewesha anaweza kuliwa na kaka zake au wa kiume akala dada zake.........wish to see one day nikiwa ukingoni mwa bahari nikipunga mkono kusema KWA HERI ZANZIBAR, KWA HERI MUUNGANO
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  mkamiati !! wewe ni mznzbr! basi shekh utakuja kuwa shemeji yangu.. nakuja kuoa huko.... btw! kura za maoni anazosema madau hapo juu ni kwa ajili yenu.. sababu si wa znz wote wanaotaka muungano uvunjike! amini hilo...
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hii unayoleta ni kashfa kubwa kwetu waZanzibar.

  Kwani siku zote anaedai na kupewa talaka ni mwanamke. Sasa kwa taarifa yako ndani ya muungano hakuna mwanaume wala mwanamke wote ni sawa.

  Na hata kama alikuwepo mwanamke basi atakuwa ni Tanganyika kwani baada ya ndoa tu alibadili jina na kujiita Mrs Tanzania. Sisi waZnz tunaitwa wazanzibari kama kawaida hatubadili jina.

  Badilisha heading yako
   
 10. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,405
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  WAKIISHA WABAGUA WATANGANYIKA DHAMBI ILE YA UBAGUZI HAIISHI HAPO , ITAENDELEA. WATAJIKUTA KUMBE HUMO NDANI(pemba na unguja) KUNA WAZANZIBARIIIIII NA WAZANZIBARAAAAAAA.--------MWL J K NYERERE.
   
 11. J

  Joshua Bukuru Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  mimi nazielewa hisia na maoni ya watu wa zanzibar juu ya muungano na katiba mpya. Wazanzibar hawapashwi kulaumiwa hata kidogo isipokuwa tulaumu muundo wa muungano uliopo ambao hautoi fursa wa wananchi wa nchi hizi mbili. Kero za muungano hazizungumziwi kweupe na badala yake mikutano ya kero hufanyikia uvunguni na kinachoamriwa huko hautujui raia. Ili muungano uimarike kwa sababu tusingependa kuona unavunjika wakati historia yetu ni moja, na asili za mila na desturi zetu kwa kiasi kikubwa hufanana. Hivyo, katika katiba mpya ijayo, ni lazima suala la serikali tatu lipewe kipaumbele kwa muktabali wa muungano wetu. Na hii hoja ilipendekezwa na tume ya jaji Nyalali lakini serikali zikapiga marufuku mapendekezo hayo. Sasa ni wakati wake vinginevyo tutakosa serikali 3 au 2 zilizopo na badala yake tutarudi kuwa na serikali zilizokuwepo kipindi kile cha 1964. Wazanzibar wana hoja ya msingi na wasipuuzwe hata kidogo!
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nawaonea huruma wanawake wa Zanzibar Muungano ukifa! Yaani hadi leo hujawahi kusikia na mwanaume anadai talaka! Nadhani wewe neno sheria halimo kwenye msamiati wako kabisaaaa!

  Btw: Hoja yako ya Mrs Tanzania mbona haijakaa vema, ungeniambia Mrs Zanzibar ningeelewa.
   
Loading...