Wazanzibar waanza kumbana dk ndalichako wa necta: Gazeti la mwanahalisi

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Leo nimesoma gazeti la Mwanahalisi na kuona makala moja inayopinga hoza za Dk Ndalichako kuhusu kufutiwa matokeo ya wazanzibar.
makala hiyo inazungumzia jinsi matokeo hayo yalivochahakachuliwa.
kwa mfano, wanadai kuna shule zipo pua na mdomo, moja imefutiwa matokeo ya wanafunzi 170 na mmoja kusalimika , lakini nyegine haikuguswa na hata mtu mmoja. Makala hiyo inadai haingii akilini swali hili la Mtihani uvuje sehemu ya shule usiambukize shule nyengine.
kwa mfano kutoka shule ya kiislam na hadi shule ya Kiembe samaki ni dakika 2 kwa miguuu. lkn shule ya kiembe samaki hakuna alieguswa shule ya kiislam amesalimika 1 kati ya 52. hivyo hivyo kwa shule ya Hamamni na Vikokotoni, Benbella na Haile salas ambazo zipo karibu sana. lkn Hamamni ambayo inaonekana inafanya vizuri zanzibar imebakwa na Necta kwa kuwafutia matokeo ya wanafunzi 152 kati ya 172 lakini hizo nyegine hakuna alieguswa. Hii anasema sawa na moto umeunguza nyumba ya mtaa mmoja ukaambukiz mtaa wa 2 lkn nyumba za jirani zimeachwa. moto huu wanadai utakuwa wa Kichawi
lkn pia anadai haiwezekani uvuje Zanzibar ushindwe kuvuja bara hasa huko wanafunzi waliopata div1 yaani hapa shule za seminary
pia wanadai Necta imejaribu kufuta zile shule ambazo ni bora kw miaka ya nyuma huko Zanzibar na kupeleka Alama ya D na F shule ambazo zimepakana na shule zilizofutiwa matokeo.
Pia imejidai hao wanafunzi wa shule waliofutiwa ambao wao wamesalimika wameangua Div 1v kwa alama ya D na F.

jeografia ya zanzibar kutoka shule hadi shule ni dakika 5 hadi 10 kwa miguu huku mtihani ulifanywa siku 14.

lakini haiwezekani uvuje zanzibar usipande meli au Ndege kufika Iringa na Bukoba.lkn hat hii njia ya Email au simu nayo ipo lkn nndalichako anadai Wabongo hawakuona.
Kikubwa zaidi wanadai shule zilizolengwa na sakata hili shule ambazo zikifanya vizuri sana huko nyuma mfano shule ya Mikunguni, High view na Lauret.
pemba shule ya kiislam wamefutiwa wote .
 
Kwani kuvuja kwa mitihani huwa unaambukizwa kwa kuvuma kwa upepo?

Hivi kwanini 1997 mtihani ulifutwa?jee unaamini mtihani unaweza kuvuja Shule 1 halafu usiangukie shule nyengine?tena ukiwa kwa mwanafunzi siku 14 mkononi?. hakuna duniani formula walioutumia NECTA.
 
Nadhani tumefikia wakati sasa kutafuta utaratibu mwingine wa kuwapima watoto wetu badala ya mtihani unaofanywa sikui moja na kuamua hatima yako kwani serikali yetu imeshindwa kabisa kusimamia mitihani hii.
 
Mimi naamini NECTA WAMAEYACHAKACHUA HAYA MATOKEO
 
vita ya uislamu na ukristio hii. weledi hamtaki uzingatiwe. lakini kuna ukweli kuwa zanzibar mnapenda holoholo. ni vema mngewatafuta waliosahihisha mitihani toka zanzibar wawaeleze kilichojiri NECTA sio kulalama na kutaka hurma kwa mabo yanayohitaji seriousness
 
wawafundishe watoto umuhimu wa elimu, huku wakiwafundisha watoto wao umuhimu wa kushika elimu, kuhakikisha walimu ni bora na vifaa vya kufundishia vipo vya kutosha bila kusahau vitabu, library na labs. wakisaidiwa na wazazi watoto watafanya vizuri na si kutafuta visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.

hata kwenye shule moja baadhi ya wanafunzi wanaweza pata feki, na wengine wasipate sembuse kati ya shule na shule
 
Miaka ya zamani tulipofanya mitihani hawa mdebwedo walikuwa na mitihani yao maalum.........yaani ilikuwa rahisi mno kuliko ya huku Tanganyika...na bado walifeli vibaya sana
 
Kwani kuvuja kwa mitihani huwa unaambukizwa kwa kuvuma kwa upepo?

Hata mimi nashangaa, hawajawahi kusikia mke ana virusi lakini mme yuko salama.

Nilidhani watakuwa na vitu concrete tu-discuss but all of what they say is based on the old age conspiracy theory "UDINI".
 
Hivi kwanini 1997 mtihani ulifutwa?jee unaamini mtihani unaweza kuvuja Shule 1 halafu usiangukie shule nyengine?tena ukiwa kwa mwanafunzi siku 14 mkononi?. hakuna duniani formula walioutumia NECTA.

wewe kiziwi hivi unaweza kufikiri ukiwa open mind??? maana unalalamika bila hoja ya msingi...kwani shule A wakipata majibu au wakipewa majibu ni lazima na shule B wapewe???au shule A wakiwa wezi ni lazima na shule B wawe wezi eti kisa ni majirani........??
hatuwezi kuhukumu watu bila ushahidi waliopatikana na kosa ndo wanahukumiwa.km unaona wameonewa waambie waende mahakamani au wakaombe kusahishiwa upya NECTA na wao wenyewe wakiwepo. ili ithibike kuwa ni kweli au la.
acha kuwa na mawazo ya kibaguzi na udini,au kufikiri tu unaonewa...
 
Leo nimesoma gazeti la Mwanahalisi na kuona makala moja inayopinga hoza za Dk Ndalichako kuhusu kufutiwa matokeo ya wazanzibar.
makala hiyo inazungumzia jinsi matokeo hayo yalivochahakachuliwa.
kwa mfano, wanadai kuna shule zipo pua na mdomo, moja imefutiwa matokeo ya wanafunzi 170 na mmoja kusalimika , lakini nyegine haikuguswa na hata mtu mmoja. Makala hiyo inadai haingii akilini swali hili la Mtihani uvuje sehemu ya shule usiambukize shule nyengine.
kwa mfano kutoka shule ya kiislam na hadi shule ya Kiembe samaki ni dakika 2 kwa miguuu. lkn shule ya kiembe samaki hakuna alieguswa shule ya kiislam amesalimika 1 kati ya 52. hivyo hivyo kwa shule ya Hamamni na Vikokotoni, Benbella na Haile salas ambazo zipo karibu sana. lkn Hamamni ambayo inaonekana inafanya vizuri zanzibar imebakwa na Necta kwa kuwafutia matokeo ya wanafunzi 152 kati ya 172 lakini hizo nyegine hakuna alieguswa. Hii anasema sawa na moto umeunguza nyumba ya mtaa mmoja ukaambukiz mtaa wa 2 lkn nyumba za jirani zimeachwa. moto huu wanadai utakuwa wa Kichawi
lkn pia anadai haiwezekani uvuje Zanzibar ushindwe kuvuja bara hasa huko wanafunzi waliopata div1 yaani hapa shule za seminary
pia wanadai Necta imejaribu kufuta zile shule ambazo ni bora kw miaka ya nyuma huko Zanzibar na kupeleka Alama ya D na F shule ambazo zimepakana na shule zilizofutiwa matokeo.
Pia imejidai hao wanafunzi wa shule waliofutiwa ambao wao wamesalimika wameangua Div 1v kwa alama ya D na F.

jeografia ya zanzibar kutoka shule hadi shule ni dakika 5 hadi 10 kwa miguu huku mtihani ulifanywa siku 14.

lakini haiwezekani uvuje zanzibar usipande meli au Ndege kufika Iringa na Bukoba.lkn hat hii njia ya Email au simu nayo ipo lkn nndalichako anadai Wabongo hawakuona.
Kikubwa zaidi wanadai shule zilizolengwa na sakata hili shule ambazo zikifanya vizuri sana huko nyuma mfano shule ya Mikunguni, High view na Lauret.
pemba shule ya kiislam wamefutiwa wote .

Mkuu hii habari siyo ngeni hapa,ilishawahi kuwekwa kule jukwaa la elimu kama sijasahau. Nikuulize kitu kimoja, Ndalichako alitoa sababu gani za kufutia hao watu matokeo?,kuvuja kwa mitihani au udanganyifu kwenye chumba cha mtihani? kama ni ile ya kwanza unaweza kuwa na hoja lakini kama ni sababu hiyo ya pili(udanganyifu kwenye chumba cha mtihani) unapaswa kufanya utafiti na kujiridhisha kabla ya kuweka ***** wowote hapa jukwaani kwa sababu udanganyifu unaweza kuwa wa majibu ya wanafunzi kufanana (hata kama majibu hayo si sahihi),yaani kwa kujua udhaifu wa wanafunzi wao walimu kwa kushirikiana na msimamizi wa mtihani wanaweza kupanga namna ya wanafunzi wasiojiweza kupata msaada kutoka kwa wenye afadhali.Ushanifahamu?
 
Mbona wanapoteza muda wao bure. Si waamue kufuata mfumo wa elimu wanaotaka badala ya kuendelea kutegemea mtaala wa elimu unaotumiwa na Watanganyika!
 
yaani sikuhizi naona watu wanataka kufaulishwa kwa nguvu naona kuna kikundi cha watu wenyewe wanataka kufaulu kwa kutumia nguvu, hii tunaiita you think small and you will remain small for life!
 
Back
Top Bottom