Wazanzibar ni wajibu wenu kisheria kudai nchi yenu

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,885
2,000
[h=1][/h]


Na Hamed Mazrui
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kujifahamu kwamba wanawajibu kisheria kudai haki yao ya Nchi pamoja na kuitetea Zanzibar ili irejeshe hadhi yake na Mamlaka yake kwa lengo la kujenga uchumi ulio imara na maslahi kwa wananchi wa Zanzibar.
Wito huo umetolewa na katibu wa Jumua ya Vijana Taifa CUF Mh,Khalifa Abdalla wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho pamoja na wazanzibar wapenda mamlaka kamili ya Nchi yao katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Komba wapya mkoa wa Mjini magharib Unguja.
Mh,Khalifa alisema ipo kila sababu hivi sasa Vijana wakizanzibar kuzidi kuamka na wahakikishe wanasimama mstari wa mbele kuitetea Zanzibar mpaka pale watakapohakikisha Zanzibar ina simama kama nchi kamili.
Alisema kuwa hivi sasa Chama cha mapinduzi CCM kimekuwa kikiandaa mkakati maalumu wa kuwaingiza vijana wasiokuwa wazanzibar kutoka Tanzania bara na kupewa vitambuilisho vya mzanzibar mkaazi ili waweze kupiga kura za kuamua mustakbali wa Zanzibar mnamo mwaka 2014.
‘’Tunasema wazi kwamba wazanzibar hatutoendelea kukubali tena kuingiziwa watu wasiohusika kikatiba kwa kutufanyia maamuzi ya kutuchagulia viongozi tusio wataka’’ Mh,Khalifa.
Nae Makamo Mwenyekiti Taifa (JUVI CUF) Mh,Yussuf Kaiza ametoa pole kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Zanzibar ’’ (SUZA NA ZU) ’’kutokana na baadhi ya wanafunzi wao waliokuwa katika ziara za kimichezo Dododoma kupata ajali na baadhi yao kujeruhiwa.
Alisema chama cha CCM kupitia Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)kwa makusudi wamefuta takuwimu za wapiga kura majimbo matano ya Zanzibar kwa ajili ya mkakati maalumu ambao una lengo la kuwapa ushindi CCM katika uchaguzi mkuu unaokuja.
Licha ya hayo Mh ,Kaiza alisistiza kwamba itakapofika 26/1/2013 Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF)watafanya maandamao maalumu ya amani kupiga kitendo cha wazanzibar waliowengi kunyimwa vitambulisho vya zan id.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa JUVI CUF Mh,Katani Ahmed Katani amewashauri wanacham wa CCM Zanzibar kuamka na kuacha kabisa fikra potofu ya kuthamini chama kwanza badala yake wathamini nchi yao.
Ameleza kuwa Mansour Yussuf Himid ni jemedari wa kupigiwa mfano ndani ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kutokana na kitendo chake cha kusimama kidete kutetea mamlaka kamili ya Zanzibar kinyume na itikadi ya chaama chake alichokuwa,na kwa heshima hio alioionesha Mansour katika Nchi basi anastahi na tunamtunuku kuanzia leo kuwa ni Dokta Mansour Yussuf Himid.
Alifahamisha kuwa iwapo vijana wazanzibr wasipo kuwa na upeo wa kudai Nchi yao watakuwa na upeo finyu kabisa wa fikra kwani katika mazingira ya sasa hakuna kijana ambae hatothamini maslahi ya nchi yake.
‘’Vijana amkeni teteni nchi yenu nyinyi ndio Taifa la kesho’’alisema Mh.Katani.
Aliendelea kufahamisha iwapo wazanzibar watasimama kidete kuhakikisha wanaikomboa Nchi yao basi hakuna sababu Maalim Seif asingie Ikulu mwaka 2015 na mara tu atakapoingia basi awamu inayofuata ataachia vijana waongoze nchi hii,kwani lengo lake nikuwakomboa wazanzibar na hana kabisa uroho wa madaraka.
Aidha Mh,Katani alieleza kuwa suala la ukombozi wa nchi sio lelema na linahitaji ujasiri mkubwa pamoja na kuwa na moyo, kuondoa kabisa woga iwapo wazanzibar watakuwa nayo haya basi hakuna sababu wasipate ukombozi wao.
Akiendelea kufafanua Mh,Katani alilitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kutokukubali kutumiwa na CCM na wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria za kazi na sio kukubali kutumiwa.
Mazrui Media
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom