Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,491
- 51,073
Wazanzibar mnaodhulumiwa, enyi mnaoonewa, mtume Muhammad alishafundisha, silaha ya muumini ni dua!. Amkeni usiku, Tajeni lile jina kuu la Mwenyezi Mungu ambalo mtume alifundisha kuwa ukiomba kwalo Mungu anajibu.
Amkeni usiku mswali Tahajjud, mumlilie Mwenyezi Mungu kwa dhulma hii mnayofanyiwa. Fanyeni visomo. Hamuhitaji Sheikh wa kuwaongoza, ewe Mzanzibar mmoja mmoja, amkeni usiku mlilieni Mungu. Fanyeni hivyo mfululizo kila siku kadri ya utakavyoweza, atakayeweza siku 90 na afanye, asiyeweza hizo basi hata kama ni siku moja au mbili, au tatu na kadhalika basi afanye!
Nyie hamna bunduki, hamna risasi, hata mgekuwa navyo hakuna silaha yenye nguvu kushinda dua, na wakati mzuri wa dua ni kuamka usiku na kumlilia Mungu, fanyeni hivyo.
Mshitakieni Mungu juu ya waliowatendea dhulma za wazi, katika dua tajeni Majina ya mnaowajua katika dhulma na mateso haya.
Kisha baada ya hapo kuweni na Subira kisha mje muone majibu ya Mwenyezi Mungu. Allah amesema katika dua ambazo huzijibu ni dua za aliyedhulumiwa!
Fanyeni visomo enyi Wazanzibar, kila mtu kwa uwezo na nafasi yake!