Zanzibar 2020 Wazanzibar nguvu yenu Dua, amkeni usiku Tahajjud mumshitakie Mwenyezi Mungu

Chief
Kwani Allah hakutuwekea utaratibu wa maisha....mpaka leo tunatafuta nguvu kupitia utaratibu uliowekwa na Binaadam ....

Chief
Zanzibar ya leo,Mashoga ndio nambari 1 kwa Tanzania
Zanzibar leo,Madawa ndio soko kuu

Tumeacha mafundisho ya Mola wetu
Tumeacha mafundisho ya Mtume wetu

Tukaona yamepitwa na wakati
Tukaikumbatia Dunia na Watoto wake

Kwa haya na mengine meeengi
Hivi nusra ya Allah,itakuja kweli

Hivi!unasemaje,ikiwa haya matatizo,ni adhabu itokayo kwake....kwa makosa tuliyoyafanya na tunayoyafanya...!!!

Hivi tumeisahau aya hii

وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ

NA HAKIKA HII NDIO NJIA YANGU ILIYO NYOOKA,BASI IFUATENI,NA WALA MSIFUATE NJIA(NYENGINE),MKATOFAUTIANA(MKAPOTEA)NA NJIA YANGU.........

SWALI
Hivi,Njia ya Mtume wa Allah,ni Demokrasia na Maandamano......?!!!

Na njia zipi hizo,tukizifuata,tutapotea na kuachana na njia ya Mtume wetu صلى الله عليه وسلم....?!!!

Embu Msikilize Omar Ibn Khataab

anasema

إنا كنا أذل قوم فأعزنا الله بالإسلام فمهما نطلب العزة بغير ما أعزنا الله به أذلنا الله .

HAKIKA YA SISI,TULIKUWA WATU MADHALILI MNO,ALLAH AKATUPA UTUKUFU KUPITIA UISLAM

VYOVYOTE VILE,TUKITAFUTA UKUKUFU KINYUME NA NJIA TULIYOTUKUZWA NAYO(KINYUME NA UISLAM),BASI ALLAH ATATUDHALILISHA..

SWALI
Sisi tunafuata Uislam kweli....?!
au
Sisi tunafuata matamanio ya nafsi zetu?!!!

Turuduni kwa Allah kwa kufuata Uislam Sahihi

Tuachane na ujanja ujanja huu tunaoufanya

Kinyume na hivyo
Tutatadhibiwa kila siku,huku tukipiga kelele
Tutaadhibiwa kila siku,huku tukiomba Dua asubuhi na jioni,bila ya kujibiwa

Tunamuomba Allah atuonyeshe njia ya sawa,na atupe nguvu ya kuifuata
Haohao waajiitao WANAMAPINDUZI DAIMA NDIO WAMEIFIKISHA ZANZIBAR HAPO.
Ole wao wanaojiunga na waovu...
 
Sifahamu ni vipi Seif ang'ang'ania madaraka, wakati wazanzibari wanamchangua awe kiongozi wao badala yake kigurupu kidogo kikisaidiwa na watanganyika kikifanya mapinduzi.

By the way, CCM hawajahi kushinda uchaguzi si leo pekee tokea kwenye historia. Ulifanyika uchaguzi kabla ya uhuru wakashindwa, wakasaidiwa na Nyerere kutoka Tanganyika kupindua. Mara pekee Zanzibar wameshinda uchaguzi ni wakati wa chama kimoja.

Haya basi mshashinda, leteni ayo maendeleo tuyaone!
Maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa bro.
Atakuwa amekuwa akishinda ndotoni sio kwenye box la kura. Msiongee kwa maneno kwamba kila mwaka anashinda bila ushahidi?? Anang'ang'ania uongozi sababu hataki kuwaachia vijana hyo nafasi yake. Wapiga kura tukiona sura ya mtu yuleyule muda wote obvious tunampuuza tunaona bora kuchagua sura mpya.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Msimamo wangu ni mmoja tu, ni haki!

Siangalii utaifa, udini, rangi ya mtu au ukabila. Au awe mtu wa namna yoyote atakavyokuwa, itakapothibiti kwa vipimo vyangu kuwa hii ni haki yake anapaswa apewe basi nitasimama nae. Sitojali anayetenda hiyo dhulma awe mtu wangu wa karibu au ni nani! Mimi nitasimama na aliyedhulumiwa. Labda vije vipimo vyengine vilivyothibiti na kubadili vipimo vya awali.

Kilichofanyika Zanzibar ni dhulma! Na kilichofanyika Tanganyika ni dhulma. Na aliyefanyiwa dhulma ni haki yake kuidai. Kama anavyosema Malcolm X by any means necessary.

Huo ndio msimamo wangu.
Ingia BARABARANI... kama huwez tuliza kende
 
Hahaha dua tena? Kwani Mungu hakuona uchaguzi unafanyika au alikuwa hayupo?

Dawa waseme sasa basi.
Dawa waache kumtumia mtu mmoja agombee toka sijazaliwa mpaka naanza kupata mvi. Kachoka na haaminiki
 
Hakuna kitu kama hicho. Zanzibar hii hii iliyojaa uchafu.

Toka mwaka 1995 wanaibiwa kura , wangeshafanya hivo, ndio waje wafanye leo, walishindwa 2015 Jecha alipofuta matokeo ,ije Leo ? Watasahau maisha yataendelea.

Walishindwa kumpiga Albadiri Jecha Salumu , kadunda hadi kastaafu na kaja kugombea kupitia CCM
Yaani bado hamtosheki na mliyoyafanya mnawazuia wasiombe kwa HAKIMU MUADILIFU,sasa kama ALLAH hatoweza kijibu dua zao pindi wakiomba nyie inawababaisha nini?
 
Wazanzibar mnaodhulumiwa, enyi mnaoonewa, mtume Muhammad alishafundisha, silaha ya muumini ni dua!. Amkeni usiku, Tajeni lile jina kuu la Mwenyezi Mungu ambalo mtume alifundisha kuwa ukiomba kwalo Mungu anajibu.

Amkeni usiku mswali Tahajjud, mumlilie Mwenyezi Mungu kwa dhulma hii mnayofanyiwa. Fanyeni visomo. Hamuhitaji Sheikh wa kuwaongoza, ewe Mzanzibar mmoja mmoja, amkeni usiku mlilieni Mungu. Fanyeni hivyo mfululizo kila siku kadri ya utakavyoweza, atakayeweza siku 90 na afanye, asiyeweza hizo basi hata kama ni siku moja au mbili, au tatu na kadhalika basi afanye!

Nyie hamna bunduki, hamna risasi, hata mgekuwa navyo hakuna silaha yenye nguvu kushinda dua, na wakati mzuri wa dua ni kuamka usiku na kumlilia Mungu, fanyeni hivyo.

Mshitakieni Mungu juu ya waliowatendea dhulma za wazi, katika dua tajeni Majina ya mnaowajua katika dhulma na mateso haya.

Kisha baada ya hapo kuweni na Subira kisha mje muone majibu ya Mwenyezi Mungu. Allah amesema katika dua ambazo huzijibu ni dua za aliyedhulumiwa!

Fanyeni visomo enyi Wazanzibar, kila mtu kwa uwezo na nafasi yake!
Mungu hana muda na wajinga na wapumbavu
 
Siku zoote awaswali wala kumuomba Mungu alafu leo ndo unawaambia waswali na kuomba?
wakati wa mikutano yao yasiasa hawakumtanguliza wala kumuomba Mungu leo ndo wanajua kuna Mungu wa kumuomba?
 
Wazanzibar mnaodhulumiwa, enyi mnaoonewa, mtume Muhammad alishafundisha, silaha ya muumini ni dua!. Amkeni usiku, Tajeni lile jina kuu la Mwenyezi Mungu ambalo mtume alifundisha kuwa ukiomba kwalo Mungu anajibu.

Amkeni usiku mswali Tahajjud, mumlilie Mwenyezi Mungu kwa dhulma hii mnayofanyiwa. Fanyeni visomo. Hamuhitaji Sheikh wa kuwaongoza, ewe Mzanzibar mmoja mmoja, amkeni usiku mlilieni Mungu. Fanyeni hivyo mfululizo kila siku kadri ya utakavyoweza, atakayeweza siku 90 na afanye, asiyeweza hizo basi hata kama ni siku moja au mbili, au tatu na kadhalika basi afanye!

Nyie hamna bunduki, hamna risasi, hata mgekuwa navyo hakuna silaha yenye nguvu kushinda dua, na wakati mzuri wa dua ni kuamka usiku na kumlilia Mungu, fanyeni hivyo.

Mshitakieni Mungu juu ya waliowatendea dhulma za wazi, katika dua tajeni Majina ya mnaowajua katika dhulma na mateso haya.

Kisha baada ya hapo kuweni na Subira kisha mje muone majibu ya Mwenyezi Mungu. Allah amesema katika dua ambazo huzijibu ni dua za aliyedhulumiwa!

Fanyeni visomo enyi Wazanzibar, kila mtu kwa uwezo na nafasi yake!
Acha kuchanganya watu mkuu. watafute mbinu ya kuzuia wizi. Kama vyama vya upinzani wekeni wapelelezi serikalini ,muwalipe wawafanyie kazi ya kujua kuiba kura inafanyikaje, kisha mtafute mbinu ya kuzuia na siyo kumtumia huyo mungu wa muhamad. eti dua acha ujinga mkuu
 
Unamkumbuka vile vile Hajjaj Ibn Yusuf Ath-Thaqaani?

Alikuwa ni gavana huyu wa dola ya Kiislamu. Lakini alikuwa ni mmwagaji damu mkubwa! Kachinja sana waislam na wasio waislam. Aliivamia mpaka masjidi haraam ya Makka na kuiharibu. Maeneo aliyovamia na Umma kipindi hicho ulikuwa na wana wa zuoni wakubwa! Ulikuwa na maswhaba pia na Tabiina, ni zama za watu wema.

Ikiwa kama utaihukumu Zanzibar kuwa haifuati Usilam stahiki na kuwa dhahma inayowakuta ni kwa hilo je, vipi zama za Hajjaj Ibn Yusuf Ath-Thaqaani? Waislam wa zama hizo walimkosea nini Mungu? Hajjaj amechinja wana wazuoni wakubwa wa umma wa kislam. Nao walimkosea nini? Na zama hizo Nabiyyuna alisema ni zama bora!

Aliloshauri Missile of the Nation ni zuri! Dua ni ibada na kama ni ibada ina taratibu na Habibinaa Mtume Muhamma s.a.w ameshasema "Dua ya aliyedhulumiwa haina pazia". Usiwakatishe watu tamaa kwenye rehma ya Mungu.

Maandamano ni ikhtilaf kwa wanawazuoni. Wapo wanaopinga na kutoa dalili zao na wapo wanaikubali kwa kutoa dalili zao. Kwa hilo kila mtu atafanya lisilomtia shaka na ataacha linalomtia shaka.

Demokrasia ni utaratibu wa kisheria kwa wasio na sheria. Sisi Waislam tuna utaratibu wetu tuna sheria zetu. Licha ya hivyo tunaishi kwenye nchi isiyofungamana na dini ya upande wowote, ina taratibu zake zinazofungamana na watu wa itikadi zote. Hawakuzii kutimiza nguzo zako za Uislam wala nguzo zako za Imani na wala huzuiliwi kutenda mema kufika daraja ya uchamungu.

Kuhusu suala la Mikataba Mtume aliingia na kuheshimu mkataba na mliokubaliana nao ni suala tulilotakiwa Waislamu tuliheshimu. Mafungamano ya mkataba wanaoidai wa Zanzibar ni yamewekwa kwa mfumo wa Katiba ya kwamba maamuzi ya raia ya kumchagua kiongozi wamtakaye aliyechaguliwa kwa taratibu iliyowekwa yaheshimiwe. Maamuzi yao yamevunjwa! Kwa lugha nyengine wamedhulumiwa kile kilicho haki yao! Je, wasidai haki yao!?

Bw. Missile of the Nation ameshauri basi mlilieni Mungu nalo unaliona kosa? Pengine hili aliloshauri ndiyo linaweza likawa asbab ya wao kumrudia Mungu kindaki ndaki.
Acheni utani na Dini kwa matamanio yenu yaliyofunikwa na Ujinga wa hali ya Juu

Tusomeni Dini yetu
Uislam,haukuacha kubwa wala dogo,isipokuwa umelisema na kulitolea maelezo

Tuweni makini mno

Hammaz Allah akuhifadhi na kila shari Bro
 
Naomba unijibu, je ni halali au haramu kwa muislamu kupiga kura katika chaguzi za vyama vya kisiasa, na Je ni halali au haramu kwa muislamu kugombea nafasi yoyote ya kisiasa kupitia vyama vya siasa?

Ukijibu hayo maswali basi unaweza kujua kama unachokisema kina mashiko au la!
 
Wazanzibar mnaodhulumiwa, enyi mnaoonewa, mtume Muhammad alishafundisha, silaha ya muumini ni dua!. Amkeni usiku, Tajeni lile jina kuu la Mwenyezi Mungu ambalo mtume alifundisha kuwa ukiomba kwalo Mungu anajibu.

Amkeni usiku mswali Tahajjud, mumlilie Mwenyezi Mungu kwa dhulma hii mnayofanyiwa. Fanyeni visomo. Hamuhitaji Sheikh wa kuwaongoza, ewe Mzanzibar mmoja mmoja, amkeni usiku mlilieni Mungu. Fanyeni hivyo mfululizo kila siku kadri ya utakavyoweza, atakayeweza siku 90 na afanye, asiyeweza hizo basi hata kama ni siku moja au mbili, au tatu na kadhalika basi afanye!

Nyie hamna bunduki, hamna risasi, hata mgekuwa navyo hakuna silaha yenye nguvu kushinda dua, na wakati mzuri wa dua ni kuamka usiku na kumlilia Mungu, fanyeni hivyo.

Mshitakieni Mungu juu ya waliowatendea dhulma za wazi, katika dua tajeni Majina ya mnaowajua katika dhulma na mateso haya.

Kisha baada ya hapo kuweni na Subira kisha mje muone majibu ya Mwenyezi Mungu. Allah amesema katika dua ambazo huzijibu ni dua za aliyedhulumiwa!

Fanyeni visomo enyi Wazanzibar, kila mtu kwa uwezo na nafasi yake!

Ndugu yangu ulicho usia ni kizuri.lakini mtu hawezi kumshitakia Mola tu na kukaa kusubiri. Tumefunzwa na Mtume (S. A. W.) kuwa mwenye
mwenye kujitahidi hufuzu. Pia kuna kisa ambapo mtu alikwenda kwa Mtume (S. A. W.) na alipofika hakumfunga kamba myama wake alomtumia kwa safari yake, alipoulizwa kwa nini hakumfunga, akajibu kuwa Mola atamlindia, Mtume Muhammad (S.A.W) akamwambia umfunge kwanza halafu ndio utawakal kwa Allah kuwa atakulindia. Point yangu ni kuwa katika mafunz ya dini yetu tunaambiwa tuombe na tufanye jitihada ya kupata tulichokiomba. Huwezi kuwa unaumwa halafu ukakaa tu kwenye msala kuomba lakini hufanyi jitihada yeyote ile ya kuepukana na maradhi uliyonayo kuanzia usafi wa mazingira, kutumia dawa n.k. Tumeambiwa kabisa mola anamsaidia yule anaejisaidia.

Hatuwezi tu kukaa na kuomba dua bila ya kufanya jitihada za vitendo kuzuia dhuluma zinazoendelea visiwani. Tuombeni dua halafu tuinuke na kudai haki zetu kwa njia yeyote ile ambayo tunaamini tutaweza kufanikiwa. Dua ni lazima lakini ni lazima zifuatwe na vitendo.

Mtume Muhammad (S.A.W.) amesema mwenye kujitahidi na kujipinda (kujituma kikweli katika kutatua haja yake) hufanikiwa. Kwa hiyo kama kweli tunataka mabadiliko zanzibar basi dua pekee haitoshi kunahitajika vitendo. Vitendo gani? hapo nawaachia walioamua kuwa viongozi katika harakati za mabadiliko visiwani.
 
Swadakta vyote vifanyike.

Mpaka sasa Wazanzibar wamekuwa na subira sana, wamefuata mifumo yote tuliyokubaliana ya kinchi kupata haki zao lakini bado dhulma inazidi. Jitihada ziendane na Dua
 
Ni kweli dua ni silaha kubwa, lakini je dua ya mnafiki inakubaliwa? Maana ukweli ni kwamba ukimuondoa Maalim Seif na kikundi kidogo cha watu, walio baki wote ni wanafiki/wasaliti.
Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu tulimuaminisha Maalim Seif kwamba "alipo tupo" nae akatuahidi kwamba ikitokea dhulma kwenye kura yeye atakuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano adi kieleweke. Na kweli ametekeleza ahadi yake kama alivyo ahidi. "kama wanataka kutu uwa watuuwe, kama wanataka kutukamata watufunge acha watufunge, tunakwenda kuandamana na mimi nitaongoza".

Je tuliitikia wito?
Je ni kweli alipo na sisi tupo?

Tulicho mfanyia Maalim na nchi ni usaliti na unafiki.
Unafiki ni dhambi mbaya sana. Je kwa unafiki huu dua zetu zitakubalika?
 
akili mseto

Yaani Allah na Mtume wake,hakuwafunzeni njia ya kufanya....mpaka leo unasema tutumie njia yoyote ile...?!!!

Unataka uondoshe munkar kwa kutumia Munkar

ni sawa na anaejisafisha haja kubwa kwa haja kubwa......
Ndugu yangu ulicho usia ni kizuri.lakini mtu hawezi kumshitakia Mola tu na kukaa kusubiri. Tumefunzwa na Mtume (S. A. W.) kuwa mwenye
mwenye kujitahidi hufuzu. Pia kuna kisa ambapo mtu alikwenda kwa Mtume (S. A. W.) na alipofika hakumfunga kamba myama wake alomtumia kwa safari yake, alipoulizwa kwa nini hakumfunga, akajibu kuwa Mola atamlindia, Mtume Muhammad (S.A.W) akamwambia umfunge kwanza halafu ndio utawakal kwa Allah kuwa atakulindia. Point yangu ni kuwa katika mafunz ya dini yetu tunaambiwa tuombe na tufanye jitihada ya kupata tulichokiomba. Huwezi kuwa unaumwa halafu ukakaa tu kwenye msala kuomba lakini hufanyi jitihada yeyote ile ya kuepukana na maradhi uliyonayo kuanzia usafi wa mazingira, kutumia dawa n.k. Tumeambiwa kabisa mola anamsaidia yule anaejisaidia.

Hatuwezi tu kukaa na kuomba dua bila ya kufanya jitihada za vitendo kuzuia dhuluma zinazoendelea visiwani. Tuombeni dua halafu tuinuke na kudai haki zetu kwa njia yeyote ile ambayo tunaamini tutaweza kufanikiwa. Dua ni lazima lakini ni lazima zifuatwe na vitendo.

Mtume Muhammad (S.A.W.) amesema mwenye kujitahidi na kujipinda (kujituma kikweli katika kutatua haja yake) hufanikiwa. Kwa hiyo kama kweli tunataka mabadiliko zanzibar basi dua pekee haitoshi kunahitajika vitendo. Vitendo gani? hapo nawaachia walioamua kuwa viongozi katika harakati za mabadiliko visiwani.
 
Labda niwaambie kitu kimoja ndg zangu Wazanzibar

Ikiwa mnataka Zanzibar ijitoe katika Serikali hii...na mpate Serikali nyengine itakayowapa Dunia yenu....bila ya kuchunga Mipaka ya Allah na maamrisho yake.....Basi ni sawa kutumia njia hizi mnazotumia kwasasa

Ila
Tahadhari sana
Msitumie kivuli cha Dini kwa lengo la kuipata Dunia

Wallah hamtofanikiwa hata siku moja

Dunia huletwa na Dunia yake
Mbele ya Dunia....Hakuna Halali wala Haramu...Vyote ni sawa

Lkn Dini
inahitaji ufuate kanuni zake...ikiwa mnakusudia Dini

Bila ya hivyo
mnampigia mbuzi gita
 
Back
Top Bottom