Zanzibar 2020 Wazanzibar nguvu yenu Dua, amkeni usiku Tahajjud mumshitakie Mwenyezi Mungu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,444
2,000
Wazanzibar mnaodhulumiwa, enyi mnaoonewa, mtume Muhammad alishafundisha, silaha ya muumini ni dua!. Amkeni usiku, Tajeni lile jina kuu la Mwenyezi Mungu ambalo mtume alifundisha kuwa ukiomba kwalo Mungu anajibu.

Amkeni usiku mswali Tahajjud, mumlilie Mwenyezi Mungu kwa dhulma hii mnayofanyiwa. Fanyeni visomo. Hamuhitaji Sheikh wa kuwaongoza, ewe Mzanzibar mmoja mmoja, amkeni usiku mlilieni Mungu. Fanyeni hivyo mfululizo kila siku kadri ya utakavyoweza, atakayeweza siku 90 na afanye, asiyeweza hizo basi hata kama ni siku moja au mbili, au tatu na kadhalika basi afanye!

Nyie hamna bunduki, hamna risasi, hata mgekuwa navyo hakuna silaha yenye nguvu kushinda dua, na wakati mzuri wa dua ni kuamka usiku na kumlilia Mungu, fanyeni hivyo.

Mshitakieni Mungu juu ya waliowatendea dhulma za wazi, katika dua tajeni Majina ya mnaowajua katika dhulma na mateso haya.

Kisha baada ya hapo kuweni na Subira kisha mje muone majibu ya Mwenyezi Mungu. Allah amesema katika dua ambazo huzijibu ni dua za aliyedhulumiwa!

Fanyeni visomo enyi Wazanzibar, kila mtu kwa uwezo na nafasi yake!
 
hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
786
1,000
Hakuna kitu kama hicho. Zanzibar hii hii iliyojaa uchafu.

Toka mwaka 1995 wanaibiwa kura , wangeshafanya hivo, ndio waje wafanye leo, walishindwa 2015 Jecha alipofuta matokeo ,ije Leo ? Watasahau maisha yataendelea.

Walishindwa kumpiga Albadiri Jecha Salumu , kadunda hadi kastaafu na kaja kugombea kupitia CCM
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,634
2,000
Hahaha dua tena?! Kwani Mungu hakuona uchaguzi unafanyika au alikuwa hayupo?!

Dawa waseme sasa basi.
Je, hukumuona yule aliyepinda mdomo na yule aliyepofuka? Walikuwa wakisema sana na kujitapa hii leo kimyaaa kama hawakuwahi kuwapo.

Nguvu ya Muumba haidhihakiwi na dua ya aliyedhulumiwa haianguki.

Kuweni na busara watu wasifike huko kwa dhihaka zenu na usafihi wenu
 
babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
7,145
2,000
Waache kula tende halua na gahawa wabaki kukesha na swala,
Halafu mwenyewe wanayemuombea mabaya ndo kwanza na anashinda huko huko church na maaskofu kuomba na nyie awabebe tu na mbeleko baas muendele kunywa kahawa maana kwa uvivu nyie ni nambari uno.
Kaeni hapo sindano iwaingie ni NYWIIIII mpaka mseme mama nangai
 
Mangobase

Member
Sep 3, 2020
20
45
Ndo milaana itawarudia chezeeni Mungu Mungu hapendi ujinga mlikua mnadanganywa, kutukana majukwaani wawe ok nawalicho panda...๐Ÿ˜ndo hvyo mwiyi ndo Rais 5 tena ndo imetoka hiyo
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
26,910
2,000
Usikariri
Hakuna kitu kama hicho. ,Zanzibar hii hii iliyojaa uchafu

Toka mwaka 1995 wanaibiwa kura , wangeshafanya hivo, ndio waje wafanye leo, walishindwa 2015 Jecha alipofuta matokeo ,ije Leo ? Watasahau maisha yataendelea

Walishindwa kumpiga Albadiri Jecha Salumu , kadunda hadi kastaafu na kaja kugombea kupitia CCM
 
Abuu Dharr

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
2,499
2,000
Chief
Kwani Allah hakutuwekea utaratibu wa maisha....mpaka leo tunatafuta nguvu kupitia utaratibu uliowekwa na Binaadam ....

Chief
Zanzibar ya leo,Mashoga ndio nambari 1 kwa Tanzania
Zanzibar leo,Madawa ndio soko kuu

Tumeacha mafundisho ya Mola wetu
Tumeacha mafundisho ya Mtume wetu

Tukaona yamepitwa na wakati
Tukaikumbatia Dunia na Watoto wake

Kwa haya na mengine meeengi
Hivi nusra ya Allah,itakuja kweli

Hivi!unasemaje,ikiwa haya matatizo,ni adhabu itokayo kwake....kwa makosa tuliyoyafanya na tunayoyafanya...!!!

Hivi tumeisahau aya hii

ูˆูŽุฃูŽู†ู‘ูŽ ู‡ูŽุฐูŽุง ุตูุฑูŽุงุทููŠ ู…ูุณู’ุชูŽู‚ููŠู…ู‹ุง ููŽุงุชู‘ูŽุจูุนููˆู‡ู ูˆูŽู„ุง ุชูŽุชู‘ูŽุจูุนููˆุง ุงู„ุณู‘ูุจูู„ูŽ ููŽุชูŽููŽุฑู‘ูŽู‚ูŽ ุจููƒูู…ู’ ุนูŽู†ู’ ุณูŽุจููŠู„ูู‡ู

NA HAKIKA HII NDIO NJIA YANGU ILIYO NYOOKA,BASI IFUATENI,NA WALA MSIFUATE NJIA(NYENGINE),MKATOFAUTIANA(MKAPOTEA)NA NJIA YANGU.........

SWALI
Hivi,Njia ya Mtume wa Allah,ni Demokrasia na Maandamano......?!!!

Na njia zipi hizo,tukizifuata,tutapotea na kuachana na njia ya Mtume wetu ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู…....?!!!

Embu Msikilize Omar Ibn Khataab

anasema

ุฅู†ุง ูƒู†ุง ุฃุฐู„ ู‚ูˆู… ูุฃุนุฒู†ุง ุงู„ู„ู‡ ุจุงู„ุฅุณู„ุงู… ูู…ู‡ู…ุง ู†ุทู„ุจ ุงู„ุนุฒุฉ ุจุบูŠุฑ ู…ุง ุฃุนุฒู†ุง ุงู„ู„ู‡ ุจู‡ ุฃุฐู„ู†ุง ุงู„ู„ู‡ .

HAKIKA YA SISI,TULIKUWA WATU MADHALILI MNO,ALLAH AKATUPA UTUKUFU KUPITIA UISLAM

VYOVYOTE VILE,TUKITAFUTA UKUKUFU KINYUME NA NJIA TULIYOTUKUZWA NAYO(KINYUME NA UISLAM),BASI ALLAH ATATUDHALILISHA..

SWALI
Sisi tunafuata Uislam kweli....?!
au
Sisi tunafuata matamanio ya nafsi zetu?!!!

Turuduni kwa Allah kwa kufuata Uislam Sahihi

Tuachane na ujanja ujanja huu tunaoufanya

Kinyume na hivyo
Tutatadhibiwa kila siku,huku tukipiga kelele
Tutaadhibiwa kila siku,huku tukiomba Dua asubuhi na jioni,bila ya kujibiwa

Tunamuomba Allah atuonyeshe njia ya sawa,na atupe nguvu ya kuifuata
 
Kama uislamu hautaki demokrasia basi unataka aina gani ya utawala?

naomba mfano mmoja tu wa aina ya utawala ambao inapaswa watu wafuate uliopo katika nchi yoyotehapa duniani.

Ngoja nikwambie kitu: Mungu anaheshimu mikataba ambayo wanadamu wamefunga baina yao ambayo si ya kumuasi, vitu kama Katiba ya namna nchi iongozwe ni mikataba baina ya watu wa nchi husika. Sasa ukiapa kuwa fair kwa mujibu wa katiba halafu ukaiba kura na kumtangaza asiyeshinda umevunja mkataba na Mungu atakuhukumu kwa kuvunja mkataba huo.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,744
2,000
Je hukumuona yule aliyepinda mdomo na yule aliyepofuka? Walikuwa wakisema sana na kujitapa hii leo kimyaaa kama hawakuwahi kuwapo.
Nguvu ya Muumba haidhihakiwi na dua ya aliyedhulumiwa haianguki.
Kuweni na busara watu wasifike huko kwa dhihaka zenu na usafihi wenu
Nani kapinda mdomo na nani kapofuka?!
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,920
2,000
Mimi nilikuwa namuona Mwinyi kama mtu muungwana lakini ajabu kwa sasa kila nikimsikia sauti yake anaongea kwenye Radio nahisi kama kutapika nahisi sauti ni mbaya na hili naongelea kwa ukweli nahisi kama shetani anaongea sasa sijui ni mimi tu na wengine wanapata hisia kama zangu.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,276
2,000
Zanzibar ni koloni la Mtanganyika.Heri ya aliekuwa Sultan kuliko Mtanganyika mweusi.Tafuteni uhuru wenu kwa jasho na damu.
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
908
1,000
Uzuri wa Mungu sio mwanadamu maombi ya wenye hila ni kelele mbele zake.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,444
2,000
Mimi nilikuwa namuona Mwinyi kama mtu muungwana lakini ajabu kwa sasa kila nikimsikia sauti yake anaongea kwenye Radio nahisi kama kutapika nahisi sauti ni mbaya na hili naongelea kwa ukweli nahisi kama shetani anaongea sasa sijui ni mimi tu na wengine wanapata hisia kama zangu.
Hussein Mwinyi ni dhalimu, Kibaraka aliyewekwa na Tanganyika kuwakalia watu wa Zanzibar
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom