Wazanzibar na Uamsho wa Kuchoma Makanisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibar na Uamsho wa Kuchoma Makanisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chechetuka, May 29, 2012.

 1. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi kumalizika Tanzania Bara na Visiwani mwaka 2010, Dunia ilishuhudia zoezi la kihistoria la kupiga kura ya maoni iliyopelekea mabadiriko ya Katiba yaliyotoa ridhaa ya Serikali ya Mseto ktk visiwa vya Zanzibar. Tukio hili la Kihistoria lilitokea baada ya wananchi ktk visiwa hivyo kukaa kwa muda mrefu wakisubiri kwa hamu kushirikishwa kwa vyama vyote hasimu ktk ujenzi wa Taifa lao.

  Kukamilika kwa zoezi hili kulitoa matumaini makubwa sana ya amani ktk visiwa vya Zanzibar, kwani Serikali iliyopo sasa inaundwa na vyama vikuu viwili, yaani CCM na CUF. Vyama hivi vimekuwa ktk ushindani mkubwa wa kutawala Dola toka mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa rasmi mwaka 1992 na kuingia ktk uchaguzi Mkuu wa kwanza Mwaka 1995.

  Hivi karibuni tulisikia kuwa visiwani Zanzibar kuna kikundi kimenzishwa chenye malengo ya kuwafikishia watu habari njema za dini ya Kiislamu. Kikundi hicho si kingine bali ni, Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara. Viongozi wote wa kikundi hiki ni wanachama wa CUF.

  Wana Uamsho hao waliomba kibali cha kufanya maandamano ya kupinga zoezi la mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati jeshi la Polisi likijadili kwa kina maombi hayo ambayo yameombwa na Jumuiya ya KIDINI, Ijumaa iliyopita (25 May 2012) kikundi hiki kilifanya "KAFARA" ktk eneo la Maruhubi mjini Unguja. "Inasemekana" ktk "KAFARA" hiyo Maalim Seif alihudhuria.

  Katika "KAFARA" hiyo, Jumuiya hiyo iliamua kufanya maandamano siku ya Jumamosi hata kama kibali walichoomba hakijatoka. Waliazimia kuandamana kwa malengo mawili makubwa:

  1. Kupinga mchakato unaoendelea wa kuunda Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Kupinga Muungano uliofanywa mwaka 1964 kati ya Tanganyika na Zanzibar

  Ikumbukwe kuwa, siku zote vyama vya Siasa vinaposhindwa katika chaguzi mbali mbali vimekuwa vikilalamika kuwa Katiba ya Nchi HAIFAI. Leo hii Rais Jakaya Kikwete AMEAMUA KUWAPA WATANZANIA KATIBA MPYA kwa kuwashirikisha WATANZANIA wote. Hivi ni kweli tunahitaji kumpinga ktk hili au kumpongeza?

  Baada ya Jeshi la Polisi kumkamata kiongozi wa Jumuiya hiyo, wanachama wake walianzisha vurugu mitaani na kusababisha kutoweka kwa amani ktk visiwa hivyo. Kama hilo halikutosha, wanachama hao walihamasishwa kuchoma Magari, maskani za CCM na Makanisa.

  Zanzibar ni moja kati ya sehemu nne duniani ambazo zilichaguliwa kuwa vituo vya kufundishia DINI ya Kiislamu karne nyingi zilizopita, ukitoa kile cha Jeddah-Saudi Arabia na Cairo-Misri. Kituo hiki kipo maeneo ya KIKUTANI mjini Unguja, hapa ndipo walipokuwa wanafundishwa MASHEIKH toka sehemu mbali mbali duniani, ambapo karibu yake kuna Msikiti wa Jibril. Kutoka ktk kituo hicho mpaka MKUNAZINI lilipo Kanisa la Kianglikani lililojengwa miaka ya 1860 ni mita zinazokisiwa kuwa kati ya 200 na 300.

  Nimejaribu kuchimba historia ya DINI ktk visiwa hivyo, wallah sijapata kusoma sehemu inayoonesha kuwa kuna siku Waislamu waligombana na Wakristo ktk visiwa hivyo.

  Baada ya hapo nilianza kujiuliza maswali yafuatayo:

  - Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ni kikundi cha kueneza DINI au SIASA?
  - Kuna Uhusiano gani kati ya shughuli zao za kidini na Chama Cha Siasa cha CCM?
  - Kuna Uhusiano gani kati Makanisa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioizaa Tanzania?
  - Kuna Uhusiano gani kati ya Makanisa na Katiba ya Mpya?

  Wana Jamii Forum, tunahitaji kulijadili suala hili kwa kina ili tusije kusomeka vibaya ktk historia ya nchi hii.
   
 2. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Waachiwe wajitenge uone watatakavyo chapana wenyewe kwa wenyewe.
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hivi mbona kila thread kanis kanisa kanisa tu?
   
 4. ma2mbo

  ma2mbo JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  sababu mnayachoma,na hamsemi kwa nini mnayachoma.
   
 5. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hao ndio wazanzibar uwa wanatenda sio wapiga longolongo...!hawadanganyiki kwa vijisent
   
 6. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ismael anamchukia Isaka kwa sababu Mungu alimpa Isaka mamlaka ya kumtawala Ismail, Mungu alishasema hivyo.
   
 7. R

  RMA JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iwapo wazanzibari hawautaki muungano mbona dawa ni ndogo tu!!! Hivi ndio kusema Wanzanzibari hawana habari kwamba kati ya vyama vyote vya siasa ni Chadema tu ndio walio na sera za kutaka wazanzibari wenyewe wajadili aina ya muungano wanaoutaka?? Hivi hawa ndugu zetu waislamu wanaliona hilo? Mbona hata punguani anajua muungano ni wa ccm na cuf kwa maslahi ya wachache? Kazi ndogo sana hapo!! Vurugu za nini? Ipeni kura Chadema kupambazuke!!
   
 8. F

  FUNGO jr JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ko wataweza kukaa bila kuchoma makanisa tena!
   
 9. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkulu

  Lengo limetimia..
   
 10. a

  abu alfauzaan Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa Mada,
  wewe ni muongo mutlaq,viongoz wa uamsho c wafuac wa cuf,iyo uamsho ina wafuac wa vyama vyote,
  tatzo nyiny wanyamwez vinganganizi,
  lkn zenj itawatokeeni puani,mana nyiny hamtaendelea na ce ha2toendelea,2meanza zenj yanafutia kwen bara,au mu2achie nchi ye2,
  nyie wenyewe hamuoni miaka 50 mumekua maskini,kisa nguvu zenu mumezielekeza zanzibar
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. S

  Simba wa ukweli Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aisee nahisi kama wataanza kujitoa muhanga
   
Loading...