Wazanzibar hawatopokea Sumu na fitna zidi ya Kuisaliti Uamsho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibar hawatopokea Sumu na fitna zidi ya Kuisaliti Uamsho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 18, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]  KINACHO ISUMBUA ZANZIBAR NI HISHI CHAKUWA NA WANAFIKI WENGI KATIKA JAMII KULIKO WAKWELI.(DUWA ZA MAISARA ZITAWAFICHUWA NA KUWATESA).
  Katika machafuko ya hivi karibuni May 26 ya Polisi kutumia nguvu kubwa zidi ya raia wa Zanzibar ,Wazanzibar tulipata faraja ya M/Mungu kuzidi kutumainishia hazarani yupi ndie na yupi sie,hii yote likuwa ni Duwa za Maisara na ahadi za Allah kuto kuwafisha wanafiki.
  Tumeona watu wazito na ma Alhaji waki azirika na kuonyesha U-Alhaji wao akina Mwinyi na wenzake kujizihirishia kwa jamii ya Kizazi cha Wazanzibar kuwa wao ni watu wa aina gani.
  Na baado kuna vyama jaa vya siasa vyenye kutaka kupindisha ukweli halisi wa Wazanzibar nini wanataka na kuleta maneno ya fitna na uchechezi zidi ya Jumuia ya Maimamu Kislamu Zanzibar (Jumuki).
  Hawa ni watu wasio fahamu kitu na hutumiliwa kwa kurubuniwa ili kuzofisha harakati za Wazanzibar kujitowa katika Minyororo ya Muungano, hakuna shaka kuwa hawa ni vibarakaa wa kundi B la ccm Uvccm B.
  Lakini kucheza na Jumuia ya Uamsho ndio kujimaliza nikama vile Kuangamia Firauna na Watu wake , Nguvu ya Jumuia ya Maimamu ya JUMUKI incubate kuliko nguvu ya vyama vya kisiasa.
  Jumuia ya Uamsho ina Wafuasi wengi wakiwemo wenye vyama na wasio na vyama,viongozi na wasio viongozo na vyama wote imekumba na watu wote wa ambao wakazi na wananchi wengi wa Zanzibar ni Wausau.
  Kwa hio Jumuia ya Uamsho imekubalika katika jamii ya Kizanzibar na mwenye kutaka kutumia mbinu hila au sumu ya aina yoyote basi ni sawa na kuchokoza sega la Nyuki wakali na baada ya ubaya mwisho itakuwa niaibu na fezeha kwake.
  HISTORIA YA JUMUIA YA (MUAMSHO) NA KUFANANICHWA NA MAKUNDI YA KIGAIDI
  Jumuia ya
  UAMSHO ni kundi huru, linalofanya shughuli zake bila uficho likiwa Wazi kabisa na kuku Bali hoja na midahalo na lina usajili halali wa Serikali. Tofati na makundi kama BOKO HARAM au AL SHABAB au ALQIDA. Haya ni makundi yenye kufanya shuhuli zake kwa kujifisha na kwa siri na hata malengo yao yako tafauti na yale ya Jumuia ya Uamsho.
  Na hata Jumuia za Kimataifa zinajuwa na kufahamu hivyo kuwa madai ya Uamsho tokea awali ni madai halali na hata chaguzi nyingi zilopita nchini walijumuishwa kama mawakala, ukilinganicha uchaguzi wa 2001 Serekali ya Marekani iliwapigia kifua Uamsho kuwa mawakala .
  Inashangaza kuona Unafiki wa watu wenye kukataa ukweli na kupakaza fitna na Sumu juu ya madai ya Jumuia ya Jumuki (Uamsho) ambayo ni madai halali kwa wananchi wa zanzibar na yenye kufuataa sheria zote katika kudai.
  Jumuia ya Uamsho na ile ya Maimamu Zanzibar imekubalika na asilimia kubwa ya Wzanzibar kutokana na madai yao ya kutaka kura ya maoni kwanza ili kujadili Muungano ambao Wananchi wa pande zote mbili za Muungano kwa muda wa miaka 49 sasa hawakupewa fursa hio.
   
   
  Sasa madai ya Uamsho ni madai halali na yanakubaliki na wananchi wa Zanzibar , lakini chakushangaza ni Serekali zote mbili kuyapuuza na kuona kuwa ni madai yasio na mashiko .
  Na kubwa zaidi ni Serekali zote mbili kutumia nguvu za vyombo vya Dola na kuunda makundi na magegi ya checheaa fitna na machafuku zidi ya Jumuia ya Maimamu ya Jumuki na ile ya Mihazara ya Uamsho .
  Hali hii inaweza kusababisha maafa makubwa na kuleta chuki baina ya viongozi wa Serekali na wananchi wao ambao ndio walio wachagua kwa kupandikiza chuki za kidini na cachucha hasia za udini kwa lengo la kisasa.
  Tanzania haina dini lakini Wazanzibar 99% wanayo Dini yao na ni Waislamu na hawako tayari kuisaliti Dini yao na kusulubiwa katakana na wakazi wake ni waumini wa Dini ya Kislamu, na kwenda kinyuma na hivyo nikutafuta ugomvi na Wananchi wa Zanzibar na Allah.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,601
  Trophy Points: 280
  Tumekusikia!. Mke anapoichoka ndoa anajiombea talaka yake kwa ustaatabu. Ukiona mke anaanza visa ujue keshapata bwana!. Dawa yake sio kumpa talaka huko ni kumpatia anachokitaka!. Dawa yake ni kumfunza au kumshikisha adabu!.

  Talaka hatutoi na adabu mtafunzwa!.
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco,
  Tafadhali nitafsirie huu mchango wako.

  Umekusudia CCM ya Tanganyika imeioa CCM Zanzibar?
  Au CCM imeioa UAMSHO?

  Haya maajabu ya Nchi moja kuioa nchi nyingine yapo Tanzania tu?

  Duh, Pasco anaongelea ndoa na talaka, Mkandara anaongelea ndoa na Talaka.

  Huu mwaka CCM imeshikwa sehemu nyeti, "Muungano".

  Serikali mbili kuelekea serikali moja na nchi moja.

  Hili Limuungano hili litatuletea maendeleo kwa haraka sana. Kwa ari mpya, nguvu mpya na vifo dekedeke!
  Mmekusudia kuwafunza nini? Na vipi?

  Au mtawashikisha adabu kivipi? kwa style ipi? Referendum or bullet?

  Mkuu ," Ni vyema mruhusu mjadala wa wazi wa Muungano na muundo wake kulikoni kutoa vitisho" ... Nilikuwa nafikiri kwa sauti tu.
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mwana CCM anasema Muungano huu ni wa hadaa. ( Kolimba alisema CCM imepoteza dira)

  Huyu Raza mtamfanya nini?
  Ataitwa kujieleza mbele ya kamati kuu ya CCM kama Kolimba, au?

  Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/280244-baraza-la-wawakilishi-lafunguka-tusilazimishane-katika-muungano-huu-watanganyika-wanatuhadaa.html
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wazanzibar fungasheni virago vyenu mrudi kwenu
   
 6. Zux de

  Zux de JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hawa jamaa bora watuachie TG yetu"
   
 7. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uamsho ni Maalim Seif na CUF yake na Wapemba wenzake, ndio maana Shein anaogopa kusema kitu, nia hasa ya viongozi wa kundi hili ni kumweka Seif ikulu apate kufanya makubwa
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mume au mke ndiye anapoteza jina la ukoo kwa ndoa zenu?
   
 9. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Idd Amin tulimpiga kwa kuchukua mto tu je atakaegusa kisiwa chetu si tutamla kabisa? Zanzibar ni sehemu ndogo ya Tanzania daima, asietaka ahame
   
 10. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  jamani wapewe visiwa vyao hivyo viwili kwa moyo mweupeee halafu tahadhari zanzibar mkishakuwa na mamlaka kamili ningeishauri serikali ilichukulie suala la uzazi wa mpango maana tunakoenda sio sawa kabisa pande za zanzibar. sijajua serikali ya tanganyika itasemaje kuhusu wazanzibar wanaoishi huku na biashara zao je watarudi kwao?? yaani ninavyohisi baba mwanaasha alivyo anaweza kuwaacha waendelee kukaa na huku wametutukana sana sie tumekaa kimya tu.
   
 11. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  soma sheria za uhamiaji pindi ukivunjika muungano
   
 12. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni moja, Muungano ulikuwa enzi hizo
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wachina vipi, na nasikia kwao wanawala mkong'oto hapa wanawala mkong'oto, mkuu wa kituo cha polisi kuingilia na yeye kala mkong'oto! Au ndiyo "punda haendi bila mateke"?
   
Loading...