Wazanzibai wakiamua wanaweza rudisha Jamhuri ya watu wa Zanzibar – Abubakar Khamis

miftaah

Member
May 31, 2012
30
5
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar leo imesema kuwa matumizi ya neno Jamhuri ya Watu wa Zanzibar inawezekana ikiwa wazanzibari wengi watatoa maoni ya kulirejesha jina hilo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakar Khamis Bakari wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Landu aliyetaka kujua kwa nini jina hilo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar lilifutwa.
Jussa aliuliza “Lini serikali ya Zanzibar itarudisha matumizi ya jina la jamhuri na kuyaweka mapinduzi ya Zanzibar katiak misingi yake iliyokusudiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume?” alihoji.
Waziri Bakari alisema jina la jamhuri lilikuwa likitumika katiak sheria ya katiba ya zanzibar nambari 5 ya mwaka 1964 kama ilivyotamka sheria namba moja ya mwaka 1964 lakini baada ya kufanyika muungano jamhuri ya watu wa zanzibar ikatoweka.
“Baada ya kufanyika muungano wa tanganyika na jamhuri ya watu wa zanzibar Aprili 26 mwaka 1964 na kuundwa kwa Tanzania matumizi ya jamhuri yalififia na kufutika” alisema Waziri.
Aidha alisema jina la jamhuri ya watu wa zanzibar lilifutika kutokana na sheria na katiba zilizokuwa zikitumika na kuacha kutumia jina hilo baada yake kubuni maneno ya Tanzania bara na Tanzania visiwani.
“ Kisheria jamhuri ya watu wa Zanzibar haikufutwa bali ilikuwa haitumiki na tanzania imekuwa ikitumika kwa muda mrefu bila malalamiko yoyote kwa maana hiyo basi matumizi ya Tanzania ni halali kwa sababu kisheria jina likitumika kwa muda mrefu inakuwa halali” alisema.
Waziri huyo alisema kwa sababu jina halikufutwa kisheria ni rahisi kulirejesha tena pale wazanzibari watakapoamua kulirejesha tena kwa hiyo ni jukumu la wananchi wenyewe wa Zanzibar kuamua na serikali itaheshimu maamuzi yao.
“Kwa kupitia wajumbe wa baraza la wawakilishi kazi ya kutafuta maoni kutoka kwa wananchi wao inaweza kuwa ni rahisi juu ya matumizi ya jina la jamhuri lakini pia nafasi iliyopo juu ya machakato wa maoni ya katiba ya jamhuri ya muungano wananchi wende muyaseme mnayoyataka na maamuzi yenu yataheshimiwa” aliahidi waziri huyo.
 
Back
Top Bottom