Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Jarida la Sani, maduka ya Bora, Majumba ya Sinema, NBC walikuwa wanakuja wilayani kwetu kuonesha Sinema jinsi ya kutunza fedha benki kuliko kwa wahindi.
 
tulikuwa tunatoka ilala mchikichini, mob tena kwa mguu tunaenda kuangalia sinema bubu!!!
Mkuu ukiwaambia vijana wa sasa kwamba pale ulipo ubalozi wa USA ndio kulikuwa na Drive-in cinema hawatakuelewa....enzi hizo kama huna hela unakaa pale nje unacheki Bruce lee na akina Fred Williamson bila sauti. Tulikuwa tunaita kiingilio mbu!
 
kipindi tunakua mtaani hakukuwa hata na nyumba moja yenye fensi, yaani mtaani watoto wote tulikuwa tunajuana kama ndugu, mkirudi shule na wakati wa likizo wote mko pamoja ni kucheza kwa kwenda mbele.
nawahurumia watoto wangu, maana they will never experience that kind of socialization. full time wako ndani ya geti na mtaa wote ni mageti tu.
style ya maisha imebadilika sana.
nikiwa shule ya msingi nilikuwa natumwa hadi sokoni kariakoo au ilala. lakini kwa sasa mtoto wangu wa form II nasita kumtuma sehemu za namna hiyo na kwanza siamini kama anaweza manage hizo hussle.
all in all zamani ilikuwa ni tamu sana. labda tu tulimiss social media kama jf,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom