Wazalendo kuweni macho..safari hii tusikubali !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazalendo kuweni macho..safari hii tusikubali !!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mag3, Mar 13, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 8,611
  Likes Received: 4,713
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi kuwa mitambo chakavu ya Dowans/Richmond huenda ikanunuliwa kinyemela na ingawa jambo kama hili si rahisi kwa nchi inayozingatia sheria, Tanzania chochote chawezekana.

  Natoa ombi kwa watanzania popote walipo na kwa nafasi zao mbali mbali toka mkulima hadi mbunge, hili tulikatae kabisa - tuwe vigilant kisawasawa. Jamaa tumewashika pabaya na haijulikani watatumia mbinu gani safari hii maanake naona hata baadhi ya wanaojiita wasomi kutoka mlimani wanaanza kuingizwa kwenye dili kinyemela.

  Tuseme big NO - tuanze kuibomoa hili kambi la MAFISADI, yes we can.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 160
  Msishindane na serikali kwani wanalindwa na kila kitu. Kuanzia sheria mpaka katiba hivyo ikiwa wameamua kununua watanunua na hakuna yeyote yule atakaeweza kuwasimamisha mahakamani ni ubabe tu.
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,487
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Wewe ni mmoja kati ya watu waliokubali kutawaliwa mpaka kufa. Umeshakuwa na feeling negative basi huna ujanja. Lakini sisi tulio wengi tunasimama imara kabisa na kusema big NO. YES WE CAN
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 160
  Mimi sijakubali kutawaliwa maana ni ntu kutoka Pemba si unasikia valangati zetu ,tina usongo na Sultani CCM ile mbaya.

  Ila huko Tanganyika mnaogopa kufa ndio mtakaobakia kutawaliwa na kubebeshwa madeni mpaka kiyama na wafuasi wa Sultani CCM.

  Mkishauriwa muidai Katiba mnagoma ,mkiambiwa muidai tume huru ya Uchaguzi hamtaki ,sasa mnataka kusukumana na mafisadi wakati wao ndio wenye kila kitu ,maana hata wakiondoana inakuwa ni kubadilishana wenyewe kwa wenyewe ,na walipohisi kuwa kuna hatari ya wenzetu kuishi jela wakatayarisha vyumba safi kama hoteli kwa ajili ya wenzao ambao hawatakuwa na njia nyingine ile kuwaweka jela.
   
 5. T

  Tumbe New Member

  #5
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pole Mwiba, nadhani ni 'matter of principles' si sultani si mfalme nani ni dhambi kutumia kodi ya wananchi vibaya.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,575
  Likes Received: 35,449
  Trophy Points: 280
  CCM coffers are empty, therefore they are worried about financing of next year's election. It seems RA has promised CCM a big percentage from the sale price of 60 billion shillings.
   
Loading...