Wazalendo historia haiwakumbuki kwa kuwa haiwajui - 1

Ukisoma maandiko ya Mohamed Said, references zake ni za akina SYKES na wakina DOSSA mainly. Hivi Leo ukimuuliza atakwambia wazee walioijua TANU kwa kina ni wazee wa kiislam na wote hawapo, wametangulia mbele ya haki!!

Mohamed ukimchungaza utaona kuwa ni very selective katika watu aliowahoji kuhusu TANU nao wengi ni wa dini yake hakupoteza muda kuwahoji wazee waanzilishi ambao wengine wapo ambao sio waislamu!!

Hakupoteza muda kwenda kukaa na Mzee Job Lusinde kabla ya kifo chake bali alipata muda kuongea na ALLY Sykes!! Kuna watu ambao wako hai ambao angeweza, kama angeta kupata unbiased story kuhusu TANU lakini kwa vile hawakidhi matakwa yake hawezi kufanya hivyo!

Mohamed mtafute Katibu mwenezi wa kwanza wa Chama Cha TANU anaitwa ROWLAND MWANJISI ili akurekebishie mapungufu yako kwenye historia unayojaribu kuitengeneza. Huyu Mzee yuko hai somewhere in Tanzania.
 
Dunia ya leo watu wako kimslahai
Sasa mlitaka nyumba ya halima iwe
Kumbukumbu watoto,ndugu wataishije
Acha wachukue mikodi

Ova
 
Ukisoma maandito ya Mohamed Said, references zake ni za akina SYKES na wakina DOSSA mainly. Hivi Leo ukimuuliza atakwambia wazee walioijua TANU kwa kina ni wazee wa kiislam na wote hawapo, wametangulia mbele ya haki!! Mohamed ukimchungaza utaona kuwa ni very selective katika watu aliowahoji kuhusu TANU nao wengi ni wa dini yake hakupoteza muda kuwahoji wazee waanzilishi ambao wengine wapo ambao sio waislamu!!

Hakupoteza muda kwenda kukaa na Mzee Job Lusinde kabla ya kifo chake bali alipata muda kuongea na ALLY Sykes!! Kuna watu ambao wako hai ambao angeweza, kama angeta kupata unbiased story kuhusu TANU lakini kwa vile hawakidhi matakwa yake hawezi kufanya hivyo!

Mohamed mtafute Katibu mwenezi wa kwanza wa Chama Cha TANU anaitwa ROWLAND MWANJISI ili akurekebishie mapungufu yako kwenye historia unayojaribu kuitengeneza. Huyu Mzee yuko hai somewhere in Tanzania.
Ye kaegemea upande mmoja tu

Ova
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
WUkisoma maandiko ya Mohamed Said, references zake ni za akina SYKES na wakina DOSSA mainly. Hivi Leo ukimuuliza atakwambia wazee walioijua TANU kwa kina ni wazee wa kiislam na wote hawapo, wametangulia mbele ya haki!!

Mohamed ukimchungaza utaona kuwa ni very selective katika watu aliowahoji kuhusu TANU nao wengi ni wa dini yake hakupoteza muda kuwahoji wazee waanzilishi ambao wengine wapo ambao sio waislamu!!

Hakupoteza muda kwenda kukaa na Mzee Job Lusinde kabla ya kifo chake bali alipata muda kuongea na ALLY Sykes!! Kuna watu ambao wako hai ambao angeweza, kama angeta kupata unbiased story kuhusu TANU lakini kwa vile hawakidhi matakwa yake hawezi kufanya hivyo!

Mohamed mtafute Katibu mwenezi wa kwanza wa Chama Cha TANU anaitwa ROWLAND MWANJISI ili akurekebishie mapungufu yako kwenye historia unayojaribu kuitengeneza. Huyu Mzee yuko hai somewhere in Tanzania.
Bulesi,
Hakika umesema kweli rejea zangu kubwa ni Nyaraka za Sykes.

Sababu ya kutegemea Nyaraka za Sykes ni kuwa historia niliyoandika inahusu TANU kama chama cha kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hii TANU imetokana na African Asociation ambayo iliasisiwa mwaka wa 1929 Kleist Sykes akiwa katibu muasisi na Cecil Matola rais muasisi.

Waasisi wa African Association ni Kleist Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Katika kundi hili ni Kleist peke yake aliyeandika historia ya maisha yake, ''Kleist Sykes The Townsman (1884 - 1949).''

Unaweza kusoma seminar paper (1968) kuhusu maisha ya Kleist Sykes Maktaba ya Chuo Kikuu, East Africana iliyoandikwa na mjukuu wake Aisha ''Daisy'' Sykes.

Unaweza pia ukasoma maisha ya Kleist katika Modern Tanzanians (1973) kitabu alichohariri John Iliffe.

Unaweza pia ukasoma maisha ya Kleist Sykes, ''Kleist Sykes, Pioneer and Man of Ideas,'' katika ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) ''The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' (1998).

Unaweza pia ukasoma, Dictionary of African Biography utakuta historia ya Kleist Sykes (2011).

Ikiwa unatafiti historia ya TANU hizi rejea mbili mswada (baadae kitabu) kuhusu Kleist Sykes na kitabu cha Abdul Sykes na Dictionary of African Biography kitakupa yote kuhusu historia ya AA hadi TANU.

Hicho kitabu cha Abdul Sykes ndiyo nilichoandika kutokana na nyaraka za mbele baada ya kifo cha Kleist Sykes mwaka wa 1949.

Ikiwa wewe unazo rejea ambazo unadhani zina historia ya TAA na TANU zaidi ya hizi za Sykes tafadhali nifahamishe kwani nimezunguka kwingi sikufanikiwa kuzipata.

Rowland Mwanjisi bada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes alikwenda kwa Ally Sykes ili anipatie ''notes,'' zake nisome.

Mzee Mwanjisi anaishi Mikocheni.

Hizi notes ninazo katika Maktaba na hakusahihisha chochote katika kitabu changu ila jina la kaka yake Dr. Wilbard Mwanjisi.

Mimi nilimwandika kama, ''William Mwanjisi.''

Hizi notes zinaeleza ugomvi uliotokea baina ya kaka yake na Julius Nyerere.

Hizi notes nilimwonyesha Prof. Shivji na waandishi wa kitabu cha Julius Nyerere, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'wazi Kamatha.

Kuhusu Job Lusinde.
Huenda hujui.

Pale Dodoma watu waliokuwa mbele katika kuunda TANU ni Haruna Taratibu na Omari Suleiman na hawa nimezungumzanao.

Job Lusinde, Kanyama Chiume na wenzake ''Makererians,'' walimu Kikuyu Secondary School waliogopa kujitokeza wakifikiria kazi zao.

Historia yao hii imo ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.

Mzee Lusinde nimempa nakala ya kitabu changu lakini hadi anakufa alikuwa kimya.

Hiyo picha hapo chini niliwapiga siku nilipomkabidhi Mzee Job Lusinde kitabu cha Abdul Sykes.

Nakushukuru kwa ushauri wako.

1635443634633.png

1635439715943.png
 
,andika for pleasure ila usiandike kwa lengo la kubadili historia utakufa kwa pressure,kilichoandikwa kimeandikwa,sie tunaburudika kwa mastory ya kariakoo ila hayafai hata kujibia mtihani .utafeli
 
Mdukuzi,
Lengo limekamilika.
Alhamdulilah.

Sikujua itafika nitaalikwa kuzungumza kwenye vyombo binafsi na vya umma kuzungumza.

Vijana wetu si wajinga wanajibu maswali kama inavyohitajika.

Lakini wakute wanavyochambua "themes" utasuuzika roho yako.

Kitabu tunakwenda toleo la lano.

Picha nikifanya kipindi cha saa nzima kuhusu maisha ya Bi. Titi Mohamed.

Screenshot_20211028-224526_Photos.jpg
 
Mdukuzi,
Lengo limekamilika.
Alhamdulilah.

Sikujua itafika nitaalikwa kuzungumza kwenye vyombo binafsi na vya umma kuzungumza.

Vijana wetu si wajinga wanajibu maswali kama inavyohitajika.

Lakini wakute wanavyochambua "themes" utasuuzika roho yako.

Kitabu tunakwenda toleo la lano.

Picha nikifanya kipindi cha saa nzima kuhusu maisha ya Bi. Titi Mohamed.

View attachment 1990185
Ahaa sioni kizazi cha kusoma vitabu vya kiada watoto wanasoma vitabu kujibia mitihani,labda kiingizwe kwenye silabasi kitiu ambacho sitegemei
 
Ukisoma maandiko ya Mohamed Said, references zake ni za akina SYKES na wakina DOSSA mainly. Hivi Leo ukimuuliza atakwambia wazee walioijua TANU kwa kina ni wazee wa kiislam na wote hawapo, wametangulia mbele ya haki!!

Mohamed ukimchungaza utaona kuwa ni very selective katika watu aliowahoji kuhusu TANU nao wengi ni wa dini yake hakupoteza muda kuwahoji wazee waanzilishi ambao wengine wapo ambao sio waislamu!!

Hakupoteza muda kwenda kukaa na Mzee Job Lusinde kabla ya kifo chake bali alipata muda kuongea na ALLY Sykes!! Kuna watu ambao wako hai ambao angeweza, kama angeta kupata unbiased story kuhusu TANU lakini kwa vile hawakidhi matakwa yake hawezi kufanya hivyo!

Mohamed mtafute Katibu mwenezi wa kwanza wa Chama Cha TANU anaitwa ROWLAND MWANJISI ili akurekebishie mapungufu yako kwenye historia unayojaribu kuitengeneza. Huyu Mzee yuko hai somewhere in Tanzania.
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜ kuna aina fulani ya kuchanganyikiwa na kuabidiana. Hatujui hawa wazee walimfanyia nini au yeye na familia yake.
 
,andika for pleasure ila usiandike kwa lengo la kubadili historia utakufa kwa pressure,kilichoandikwa kimeandikwa,sie tunaburudika kwa mastory ya kariakoo ila hayafai hata kujibia mtihani .utafeli
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
Ahaa sioni kizazi cha kusoma vitabu vya kiada watoto wanasoma vitabu kujibia mitihani,labda kiingizwe kwenye silabasi kitiu ambacho sitegemei
Mdukuzi,
Alhamdulilah.

Mambo yamekaa vizuri wiki kuelekea Nyerere Day nimefanya mahojiano na karibu station nane za TV kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kitabu cha Abdul Sykes tunakwenda chapa ya tano In Shaa Allah.
 
Wazee hawakumbukwi kwasababu hawanamchango na walikua hawana mchango katika nchi na harakati za uhuru . Usilazimishe tukumbuke watu wasiokuwepo
 
Wazee hawakumbukwi kwasababu hawanamchango na walikua hawana mchango katika nchi na harakati za uhuru . Usilazimishe tukumbuke watu wasiokuwepo
Edwayne,
Hii ni nchi huru mtu unaweza kuamini historia unayoipenda hata kama imepikwa hakuna wa kukupeleka mahakamani.

Inawezekana ukaamini kama unavyoamini wewe kuwa wazee hawana mchango katika nchi na harakati za uhuru.

Ukaendelea kusema kuwa nisilazimishe kukumbukwa watu wasiokuwapo.

Ngoja nikupe mchango wa wazee wachache katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Naanza na Mzee Said Chamwenyewe.
Baada ya kuundwa kwa TANU July 1954 kilichofuata ni kusajili chama.

Nyerere Abdul Sykes na mdogo wake wakakubalianakuwa Nyerere akitoka kwa msajili aende moja kwa moja nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) ambako Abdul na Ally watakuwapo pale wakimsubiri.

Nyerere alipofika pale akawaeleza kuwa msajili amekataa kusajili TANU kwa kuwa yeye hakuwa na rejesta ya wanachama.

Abdul akamtafuta Mzee Said Chamwenyewe akamkabidhi rejesta na kadi za TANU na kumwambia kuwa aende Rufiji akalete wanachama wa TANU.

Hiki ni kisa kirefu lakini kwa kumalizia ni kuwa kazi hii Mzee Said Chamwenyewe aliifanya kwa mafanikio makubwa sana.

Ndipo niliposema kuwa nchi hii ni huru mtu anaweza kuamini lolote na hajafanya kosa.

Naweza nikakueleza historia ya Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU 1954 - 1958, Mzee Iddi Tulio Mwenyekiti wa baraza hili 1958 - 1963, Mzee Ali Migeyo, Mzee Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa TANU aliyepewa jukumu la kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955.

Naweza nikakueleza historia ya Mzee Thomas Plantan na nduguye Schneider Abdillah Plantan na mdogo wao Ramadhani Mashado Plantan nk. nk.

Sikulaumu.
Hujui na kama mtu hajui halaumiwi anafahamishwa.

Akifahamishwa anatoka katika ujinga na anakuwa mwerevu na mwenye kujua.

Ukweli ni kuwa historia hii imechoma nyoyo za wengi na wanatamani kama vile nisingeiandika.

Nakuwekea picha hapo chini kukuthibitishia kuwa wazee walikuwapo na walipigania uhuru wa Tanganyka.

1635476651698.png

Kushoto Iddi Faiz Mafungo b. 1905, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere na Haruna Taratibu.
 
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜ kuna aina fulani ya kuchanganyikiwa na kuabidiana. Hatujui hawa wazee walimfanyia nini au yeye na familia yake.
Father...
Babu yangu Salum Abdallah ni mmoja wa waliopigania uhuru wa Tanganyka.

Hapo chini ni clip ya dakika 2:16 nawaeleza waandishi waliokuja nyumbani kwangu kufanya mahojiano na mimi kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Hapa nawaeleza historia ya babu yangu kwa ufupi sana.
Sikiliza clip utaona kile ambacho alichonifanyia babu yangu na alichofanyia taifa letu:

Msangarufu,
Nakuomba soma hayo hapo chini kisha toa hukumu nani katumia imani yake kuwadhoofisha wale wasio kuwa wa dini yake:

Salamu,

Hivi karibuni Uongozi wa JF ulimpa tuzo mwandishi Mohamed Said ambaye ni maarufu Sana hapa JF kwa kuandika Historia ya TANU ,Tanganyikana Zanzibar.

Mzee Mohamed amekuwa akiandika historia hii kwa kile ambacho amekuwa akibainisha kuwa Historia ya TANU na Tanganyika imekuwa ikipotoshwa makusudi kwa kutowataja baadhi ya Waasisi ambao yeye anawaita wazee wake.

Bila woga wala hofu Mzee Mohamed amekuwa akieleza kuwa Historia hiyo imefutwa kwa kuwa hao Wazee ni Waislam.

Na katika maandishi hayo pia Mzee Mohamed ameeleza jinsi Waislam walivyodidimizwa Kielimu ambapo ameeleza kuwa ni kundi dogo tu la Waislam,wamekuwa\walikuwa wanachaguliwa kujiunga na Sekondari(yeye ameita 20:80)

Mzee huyu amediriki kuelezea (kwa Lugha ya kebehi) jinsi Mwalimu Nyerere alivosaidiwa ' na hao Wazee wake wakati anadai Uhuru. Kwa maneno mengine Nyerere hakulipa fadhira

Kimsingi ameandika mengi katika Uzi wake wa mwisho ambao umezua mjadala mkubwa ameeleza inakuwaje Mwenyekiti wa UWT, Mama G. Kabaka alipewa nafasi hiyo ,ilhali alishiriki kuwanyanyasa Waislam alipokuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Cha Dodoma kwa kukataa kujengwa kwa Msikiti eneo la Chuo.

Hizi no shutuma nzito kwa Serikali, CCM na Mama Kabaka Mwenyewe. Shutuma hizi zingetolewa na layman' zingewezwa kupuuzwa. Lakini zinapotolewa na Msomi,Inatia mashaka. Ilhali anaelewa kabisa namna Maamuzi ya Taasisi kama UDOM wanavyotolewa.

Lengo lake Nini!
Inawezekana Kuna kasoro katika Historia ya TANU, lakini kwa namna anavyoeleza Ndg Said kwa misingi ya Ubaguzi wa Kidini inakera.

Turudi kwenye mada, hivi Uonhozi wa JamiiForums haukuona Viashiria vya Ubaguzi vilivyomo kwenye simulizi zake hadi wakafumba macho Hadi kumpa Tuzo!? Au Viashiria hivi ni vidogo kulinganisha na Elimu anayoitoa kwa Jamii?

Mimi kwangu Viashiria hivi ni sumu katika Jamii.

Rejea mjadala katika Uzi wake kuhusu Mama Gaudensia Kabala katika jukwaa la Historia.
Lombo,
Nakushukuru sana kwa makala hii yako.

Hakika umenisaidia pakubwa kwa kujaribu kuwagutusha wenye mamlaka. juu yetu kuhusu wajibu wao katika yale ambayo mimi nimekuwa nikiyapigania.

Nakupinga kusema kuwa nimekuwa nikiandika kwa kebehi historia ya Mwalimu Nyerere na jinsi alivyopokewa na wazee wangu.

Katika hili naomba kama unao ushahidi uweke hapa hayo maneno ya kebehi kutoka kwenye kalamu yangu.

Nataka nikusaidie uelewe vizuri historia ya elimu na matatizo yaliyowafika Waislam kuanzia mwaka wa 1961 Tanganyika ilipopata uhuru wake:

1968 EAMWS ilivunjwa na serikali ili kuondoa uwezekano wa kuendelea na mipango ya elimu na ujenzi wa Chuo Kikuu.

Miaka ya 1970s Organisation of Islamic Conference (OIC)ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania serikali ikakataa kutoa kibali.

OIC ikajenga chuo hicho Mbale Uganda.

1981 Warsha wakiwa ndani ya BAKWATA kwa kujipenyeza waligeuza baadhi ya shule za Kiislam kuwa seminari ili kuboresha shule hizo.

Serikali iliingilia mchakato huu na shule zile zikarejeshwa katika hali yake ya zamani.

Mambo hayakuishia hapo.

Vijana wa Warsha waliojipenyeza BAKWATA wakafukuzwa BAKWATA kwa amri ya serikali na kupigwa marufuku kuongoza taasisi yeyote ya Kiislam nchini.

Mlezi wa Warsha Sheikh Hussein Malik akafukuzwa nchini.

Warsha haikuvunjika moyo wakajenga shule Masjid Quba serikali ikakataa kuipa tasjila.

Warsha wakaendesha shule hivyo hivyo bila tasjila hadi Prof. Malima akiwa Waziri wa Elimu alipoipa tasjila.

Mwaka wa 1987 Prof. Malima akiwa Waziri wa kwanza Muislam kuongoza Wizara ya Elimu aligundua yaliyokuwa yakifanyika ndani ya wizara hiyo na akamtaarifu Rais Ali Hassan Mwinyi.

Prof. Malima akaondolewa katika wizara hiyo baada ya kikao cha CCM Dodoma.

Miaka ya 1980s Darul Iman kutoka Saudi Arabia ilitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha.

Kama kawaida njama zikapita.
Darul Iman wakaufuta mradi na kuondoka nchini.

Yako mengi pamoja na matatizo ya NECTA nk. nk.

Nasikitika hukuwa unayajua haya kwa hiyo hukuweza kuyafikisha kwa wahusika.

Nakubaliana na wewe kuhusu sumu kwa jamii.

Lakini sumu hii haikorogwi wala kupikwa na Waislam.

Kuhusu tuzo ya JF hili naona limekuchoma sana maana umekuwa ukilirejea.

Nina tuzo mbili kabla, hii ya JF ni ya tatu.

Hayo mengine naona niyanyamazie kwa sasa.

Ikitokea fursa In Shaa Allah tutayazungumza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom