Wazabuni wa vyakula vya wanafunzi wa shule za bweni pia waangaliwe kwa jicho la tatu

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,071
Nakumbuka ni kipindi kifupi tu kimepita tangu shule nyingi za bweni nchini Tanzania kuwa katika matatizo makubwa ya kukosa chakula na pengine hadi kuzifunga.

Mind set za watumishi wa serikali katika awamu zilizopita ilikuwa ni lazima use me uongo ipi uonekane kuwa wewe ni muadilifu has a kwa kuficha uovu hata kama unawatesa wananchi.

Nakumbuka wakuu wa wilaya walidiriki kuidanganya ikulu kuwa wilaya Fulani haina njaa wakati watu wao wana utapiamlo kwa kukosa chakula.

Turudi kwa suala la WAZABUNI, hawa ni wafanya biashara walioachwa huru kufanya biashara hii ya kusambaza chakula mashuleni huku makubaliano ya gharama(bei) ya chakula ni ya makubaliano kati ya mzabuni na Mkuu wa shule na mhasibu wake.

UZABUNI ni biashara ya kupiga hela na faida yake huzaa Mara mbili, yaani ukisupply chakula cha million 20, utaidai serikali million 40.

Kwa kuwa tuna Imani sana na Mh. Rais Magufuli, wadau wa elimu ambao tunaitaka nchi hii isonge mbele, tusingependa kuona shule zetu zikikosa chakula tena kwa sababu ya madeni makubwa ya hawa wazabuni.

Kwa mfumo wa serikali iliyopita, naamini kabisa madeni Yale ya wazabuni yapo ambayo ni HEWA, lakini walioteseka ni wanafunzi na hata baadhi ya wakuu wa shule ambao walisimamishwa kazi kwa kusema UKWELI kuwa shule ina deni kubwa (kitu ambacho kilikuwa ni kosa kwa serikali ya awamu ya nne kusema ukweli)
 
Ninavyojua mimi kuna bei elekezi ya serikali. Mfano Michele kilo 2500, nyama 7500 nk. Kiukweli kuna maeneo vitu bei chini mfano mwanza kuna shule nafundisha. Mtaani mchele kilo buku, nyama 3500 ila mzabuni analeta kwa bei elekez. Bei elekez iliangalia bei ya juu ya vitu ktk tz nzima. Labda serikali ifanye utafiti kwa kila mahali kuwe na bei tofauti kuendana na mahala ila hapo itabidi iwalipe wazabuni kwa wakati. Maana huwa wanapata faida ila ni wavumilivu Sana kwenye kulipwa
 
serikali ihamie hapa.wakuu wengi wa shule na wazabuni wanaihujumu serikali kwa kutokuwa waaminifu.kuna mijizi mingi.
 
Rafiki Kwa sasa hii biashara Kati ya halimashauri ya wilaya Na wazabuni, wakuu wa shule hawasimamii kivile....!
 
Huo upgaji unasababishwa na ukiritimba na mianya ya sheria ya manunuzi iliyopo.
Ila pia hawa wazabuni wanaosambaza vyakula shuleni waangaliwe katika malipo yao. Mtu anaweza akapeleka chakula mwaka mzima halafu asilipwe hata shilingi. Hapo ni sawasawa kaikopesha serikali bila riba.
 
Back
Top Bottom