Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,470
Habari kutoka Israeli Agency of Ethiopia zinasema kuwa kundi la mwisho la Wayahudi wa Ethiopia linatarajiwa kuondoka ndani ya miezi 18 kuanzia January 2013. Tangu mwaka 1991 Wayahudi hao ambao wanafahamika kama Falash Mura (Lost kinsmen) wamekuwa wakirudi kidogo kidogo kadiri ya taratibu za utambuzi zikiendelea lkn sasa inaonekana msukumo mkubwa umefanywa kuhakikisha Falash Mura takriban 200,000 waliosalia wawe wamekwishaondoka Ethiopia ifikapo July 2014.
Wengi wa Wayahudi hao wameishi Ethiopia kama Wakristo wakiogopa kufuata Judaism kwa hofu ya mashambulizi toka kwa Waarabu. Kurejea kwao kumefungua milango ya uhuru wa kuabudu kwani wengi wao wameshaanza ku-practise Judaism wakiwa Ethiopia mara tu baada ya vibali vyao vya kuingia Israel vilipokamilika.