Way forward for tz - cuf, cdm, ccm equation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Way forward for tz - cuf, cdm, ccm equation

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by amanibaraka, Mar 30, 2011.

 1. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kuwa wote tunakubaliana kuwa Tanzania ina matatizo makubwa ya maendeleo kisiasa, kiuchumi na kijamii, na hivyo basi inahitaji mapinduzi/mabadiliko makubwa.

  Kwa kuwa vyama vya siasa vya Cuf na Chadema ambavyo vimekuwa vikitoa mwelekeo wa kuwa mbadala wa CCM katika kuleta kuleta mapinduzi hayo vimeingia madoa ya udini (haijalishi kama ni kweli au uongo- muhimu fikra hiyo ipo katika jamii).

  Kwa kuwa udini (hata katika kiwango cha kudhaniana) ni jambo la hatari na linaloweza kuleta fujo na kuhatarisha amani Tanzania, AMANI ambayo wote tunaithamini kama tunu muhimu.

  Je wana Jamii Forum hamuoni kuwa ni muhimu CCM iendelee kupewa nafasi ya kwanza kuendelea kutawala kuliko kushabikia vyama hivi ambavyo vinaweza kutuletea machafuko?

  Kwa hali hiyo hamuoni umuhimu wa kuendelea kushinikiza mapinduzi ndani ya CCM ikiwemo kuondoa mafisadi ndani ya chama, kukirudisha chama kwa wafanyakazi na wakulima, kurejesha maadili ya uongozi nk?
   
Loading...