Wawili Wadungwa Sindano za Sumu Kwa Kuuza Maziwa yenye Sumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawili Wadungwa Sindano za Sumu Kwa Kuuza Maziwa yenye Sumu

Discussion in 'International Forum' started by Mbonea, Nov 26, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  [​IMG]
  Mojawapo ya vitanda vinavyotumika kuua watuhumiwa kwa kuwadunga sindano za sumu
  Watu wawili wamedungwa sindano za sumu nchini China kwa kujihusisha na biashara ya kutengeneza na kuuza maziwa ya unga ya watoto yenye kemikali za viwandani ambayo yalisababisha vifo vya watoto sita na kusababisha maelfu ya watoto kuwa wagonjwa.Mtuhumiwa wa kwanza aliyejulikana kama Zhang Yujun aliuliwa kwa kudungwa sindano ya sumu kwa kuhatarisha maisha ya watu na mtuhumiwa mwingine aliyejulikana kama Geng Jinping aliuliwa kwa staili hiyo hiyo kwa kuzalisha na kuuza maziwa ya unga ya watoto yenye sumu.

  Watuhumiwa hao walihukumiwa adhabu ya kifo mwezi machi mwaka huu na mahakama ya mji wa Shijiazhuang kaskazini mwa China.

  Hukumu zote za adhabu ya kifo zinazotolewa na mahakama za chini hutakiwa kuidhinishwa na mahakama kuu ya China ya mjini Beijing.

  Mahakama kuu iliidhinisha adhabu hiyo na watuhumiwa hao wawili waliuliwa kwa kudungwa sindano za sumu.

  Watuhumiwa hao pamoja na wenzao 21 walishiriki kutengeneza maziwa ya unga ya watoto ambayo waliyaweka kemikali zinazotumika viwandani zinazoitwa melamine ili kuyafanya maziwa hayo yaonekane yana protini za kutosha na hivyo kupasishwa katika viwango vya ubora wa chakula.

  Kemikali ya melamine iliwasababishia watoto waliotumia maziwa hayo kuwa na ugonjwa wa kidole cha tumbo na figo zao kushindwa kufanya kazi.

  Watoto sita walifariki na watoto wengine 300,000 waliugua ghafla na kulazimika kupatiwa matibabu.

  Watuhumiwa wengine 21 wa kesi hiyo walihukumiwa adhabu mbali mbali kutokana na ushiriki wao katika kutengeneza maziwa hayo feki.

  Baadhi yao walihukumiwa vifungo vya maisha jela na wengine walitupwa jela kwa vifungo vya kati ya miaka mitano na 15.

  Source: Xinua
   
 2. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh!
   
Loading...