ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 19,707
- 28,253
Mtanikumbuka....Jeshi la Polisi kikosi cha viwanja vya Ndege Tanzania (JNIA) limewakamata watu wawili wakiwa na dawa za kulevya kilo13.4 aina ya heroin walizokuwa wakisafirisha katika jiji la Bombay nchini India.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Aprili 9,2021 Kamanda wa Polisi Viwanja vya JNA, Jeremia Shila watuhumiwa hao Maria Tumbuka (29) mkazi wa Kivule na mwanaume (jina wamelihifadhi) walikamatwa Aprili 4,2021 saa 1:50 usiku katika uwanja huo wa ndege eneo la ukaguzi wa mizigo ya abiria wanaosafiri kwenda nje ya nchi.
Shila amesema mtuhumiwa Maria alikamatwa akiwa na pakiti tatu za dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo6.65 alizokuwa amezificha ndani ya begi lake la kusafiria.
Kamanda Shila amesema watuhumiwa hao waliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Harare Zimbabwe na walikuwa wanatarajia kuunganisha safari yao kuelekea Bombay India kwa ndege nyingine ya Air Tanzania (ATCL).
"Watuhumiwa hawa walikamatwa kutokana na umahiri wa askari polisi wa viwanja vya ndege kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tulipokagua mabegi yao tulibaini dawa za kulevya wamezificha pembeni ya begi kwa ndani huku katikati wakiweka nguo kwa lengo la kukwepa mashine ya ukaguzi,"amesema Shila.
Shila ametoa onyo watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirishaji binadamu, dawa za kulevya na nyara za serikali kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Chanzo: Mwananchi