Wawekezaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawekezaji

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Semilong, Apr 2, 2009.

 1. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Katika siku za karibuni nilimsikia mwenyekiti wa kamati ya mahesabu zito kabwe akisema sababu ya kutaka tanesco inunue mitambo ya dowans ni capacity charges ambazo wamekuwa wakiwalipa wawekezaji. Na watu mbalimbali na tanesco wamekuwa wakisema capacity charges inakula 85% ya mapato.

  Kikwete kwenye hotuba yake mwezi huu, juu ya umeme amesema wawekezaji wamechelewa kuwekeza kiwira na kwingineko kwenye secta ya nishati.

  1. Zito/tanesco wametumia gharama za wawekezaji ndio sababu ya kutaka kununua dowans.

  2. Kikwete sijui aogopi gharama, nae ametumia neno wawekezaji wamechelewa kuwekeza kiwira na kwingineko ndio sababu ya upungufu wa umeme.

  3. Viongozi wengi wamekua wakitumia wawekezaji kama sababu ya kila kitu

  4. Je serikali hii haiwezi kufanya tena mradi wowote bila wawekezaji? ,naongelea miradi ya wastani tu, tafadhali simahanishi tazara

  5.je wawekezaji ndio chance ya wao kupata kamisheni?

  6. Je hamuoni kwamba mambo ambayo serikali ingeyafanya yenyewe, kwa maksudi kabisa inangojea wawekezaji ili ipate kamisheni, mfano tanesco kununua mitambo mapema badala yake kuja kutaka kununua dowans.

  7. Mradi wa songas umegarimu $300m. Hela zilizoliwa epa na twin towers ni ($150m +$200m= $350m). Kama serikali ingetumia $350m kwenye songas si wao wenyewe ndio wangekuwa wanapata capacity charges na hela yao ingekua imerudi.

  8. Hao wawekezaaji kwenye migodi ndio wanaacha mashimo na hatupati kitu, $3bn in sales, eti tax $1m kwa ajili hawajapata faida mbona hawaondoki, ndio kwanza wamepanga foleni.

  9. Hawa viongozi wananikera wanavyotumia neno wawekezaji ndio sababu ya kuhalalisha kila kitu.

  10. Je wawekezaji ndio kasi mpya nguvu mpya hari mpya????
   
Loading...