Wawekezaji zaidi ya 140 kutoka Italia wawekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
Wawekezaji zaidi ya 140 kutoka Italia wamewekeza katika miradi
mbalimbali nchini Tanzania
Takwimu hizo zimetolewa na Naibu Waziri Wizara ya Madini, Prof.
Shukrani Manya alipokuwa akifungua jukwaa la biashara na
Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lilifanyika Jijini Roma, Italia
leo.
Prof. Manya amasema kuwa miradi hiyo inathamani ya Shilingi
bilioni 5 inayotoa ajira kwa watanzania zaidi ya 4000.
“Jukwa hili tunataka liendelee kuwa sababu ya kuchagiza
uwekezaji mwingine kutoka Italia kwa kutumia teknolojia
waliyonayo, kwa kutumia utalaamu walionao wa designing na
…….na sasa waone kuwa Tanzania ni sehemu salama ya
kuwekeza na Tanzania inaendelea kuweka mazingia wezeshe ya
kukuza sekta ya uwekezaji na biashara,” Amesema Prof. Manya
Ameongeza kuwa kupitia jukwaa la biashara na uwekezaji
biashara na uwekezaji utaendelea kuongezeka na kuongeza zaidi
na hasa katika maeneo ambayo tumawaeleza hapa kupitia
jukwaa hili.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe.
Mahmoud Thabiti Kombo amesema kuwa kufanyika kwa
kongamano hili la biashara na uwekezaji lengo lake kubwa ni
kuwavutia wafanyabiashara na wewekezaji wa sekta mbalimbali
kutoka Italia kuwekeza zaidi Tanzania.
“mwitukio ni mkubwa na tumeitikiwa na jumuiya za kibiashara na
wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 250 kutoka nchi zote
mbili wameshiriki katika kongamano hili,” amesema Balozi Kombo
Balozi Kombo ameongeza kuwa, Wafanyabiashara kutoka italia ni
wabobezi katika sekta ya madini lakini pia katika utalii hivyo ni
matumanini yake kuwa mara baada ya kumalizika kwa

kongamano hilo wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Italia
wataongezeka zaidi Tanzania.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Wawekezaji katika
Hoteli Zanzibar, Bw. Paulo Rosso amewasihi wawekezaji kutoka
Italia kuwekeza kwa wingi Tanzania kwa kuwa mazingira ya
biashara na uwekezaji ni tulivu na salama.
“Tanzania ni sehemu salama kuwekeza…..nawahakikishia mimi
nimewekeza Tanzania na ninaona ni sehemu salama ya kuwekeza
karibuni sana kuwekeza kwa maendeleo ya Tanzania na Italia,”
amesema Bw. Rosso
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Edwin Rutageruka ameongeza kuwa katika kutekeleza
maelekezo ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan Wizara ya Mambo ya Nje inatekeleza
diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kuhakikisha uchumi
unaongezeka.
Jukwa hilo la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia
limehudhuriwa na Wafanyabiashara na Wawekezaji takribani 250
kutoka nchi zote mbili.
Wafanyabiashara na wawekezaji hao ni wa sekta za utalii, kilimo,
madini, na ujenzi.
Pamoja na mambo mengine, jukwaa hilo limewawezesha
wafanyabiashara na wawekezaji kujadili fursa, uwezekano wa
ubia, changamoto zinazokabili mazingira ya biashara na njia ya
kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia
limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa
kushirikiana na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Mamlaka ya Taifa ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).
 
Kitu cha pekee kwa serikali yangu chini ya CCM na wasaka teuzi ni propaganda za kiwango cha lami. Kila awamu wao huja na proganda na mabango ya kupamba uongozi ulio madarakani hadi wanapiga offside.
Ukitazama toka zama za ruksa, ukweli na uwazi, maisha bora kwa kila mtanzania, hapa kazi na sasa kazi iendelee unaweza amini kuwa sasa tungekuwa tunakaa meza moja na akina China, USA linapokuja suala la maendeleo na maisha bora ila cha kushangaza mambo ni tofauti kabisa.
Tangu kelele za kuandikwa habari za wawekezaji kumiminika nchini hakuna hata sehemu moja walipoanza japo kuonesha dalili za mradi kuanza.
Wako wapi wale waisrael 1000 kuwekeza Tanzania?
Wako wapi wanunua ndizi zetu kule Kagera?
Wako wapi akina Antonio Guteres na PM wa Uingereza na kiwanda chao cha kuunganisha magari (NISSAN) kama msaka teuzi mmoja alivyoutangazia umma wa JF siku chache zilizopita?
Wako wapi wanunua korosho zetu kule kusini?
 
Back
Top Bottom