Wawekezaji wote wa Barick/ ACACIA kuondoka rasmi Tanzania mwezi februari 2018?

Mkuu,kama walivyo kwisha kurekebisha waliopita narudia kidogo.
1.GGM inamilikiwa na Anglo gold ashanti na si ACACIA /barrick.

2.makininikia au gold copper concentrate inazalishwa bulyanhulu na buzwagi na si kama ulivyoeleza hapo juu..

3.migodi inayomilikiwa na ACACIA ni buzwagi au pangea,bulyanhulu na north mara.

4.buzwagi itafungwa mwakani kutokana na life span ya mgodi kuisha na si kutokana na masharti ambayo umeeleza kwenye taarifa yako hapo juu.

5.mgodi unaofungwa kwa muda ni bulyanhulu as we speek now no any production activities going on in the site.kwa sababu makinikia bado yamezuiliwa kusafirishwa kwenda nje na wanavyodai ni kuendesha kwa hasara tangu zuio hilo lilipowekwa na serikali mwez march.

Nb.tayari baadhi ya kampuni za kandarasi zimeshaondoka bulyanhulu na mwez huu mwishoni wafanyakazi wote waliochini ya ACACIA wataondolewa kazin since mgodi unafungwa.na kwa mujibu wa taarifa yao ni kuwa mwakani watafungua mgodi na kua wanatumaini na mazungumzo yanayoendelea kati yao na serikali yatazaa matunda.

Asante.
mkuu hasipoelewa hayo maelezo najiondoa rasmi JF
 
Mwaka ujao utakuwa mwaka wa machungu sana kwa watanzania katika sekta ya madini, nimefahamishwa na menejiment ya Barick/ ACACIA ambao wameda kuwa watakuwa wameshaihama rasmi Tanzania kufikia mwezi februari mwaka 2018 kuiacha rasmi migodi yote ya GGM, North Mara, Bulyanghulu na Buzwagi. Wanadai kuwa wanapata vikwazo vipya kila uchwao kufuatia biashara yao ya uwekezaji wa madini nchini Tanzania.
wewe albadiri inakudhuru,mwaka utakuwa vipi mchungu kwani wanachukua madini yetu?ndio kwanza wameiba 5% ya akiba yote na waende tu ulisikia wapi nchi inakufa njaa kwa kukosa kuchimba dhahabu.
Tutawapa vijana vipande vya ardhi wachimbe na tutaweka mfumo bora wa kukusanya kodi kuliko kuibiwa kama sasa,waende zao
 
Hiyo ni habari njema kabisa kwamba tutaachiwa madini yetu. Hali ngumu itatoka wapi? waondoke wote
 
IMG-20170916-WA0014.jpg
 
unapoongelea ACACIA halafu unaiweka GGM unaonesha ni jinsi gani haujafahamishwa kitu chochote na menejimenti yyt,mkuu ni mgodi mmoja tu unafungwa mwakani sababu umefika mwisho
Nilikuwa nashindwa kumuelewa, mwanzoni nilidhani amekosea kwa bahati mbaya...hajui tofauti ya Anglogold Ashanti na Barrick/ACACIA...
 
Mwaka ujao utakuwa mwaka wa machungu sana kwa watanzania katika sekta ya madini, nimefahamishwa na menejiment ya Barick/ ACACIA ambao wameda kuwa watakuwa wameshaihama rasmi Tanzania kufikia mwezi februari mwaka 2018 kuiacha rasmi migodi yote ya GGM, North Mara, Bulyanghulu na Buzwagi. Wanadai kuwa wanapata vikwazo vipya kila uchwao kufuatia biashara yao ya uwekezaji wa madini nchini Tanzania.

Aidha imefahamika kuwa mazungumzo yanayoendelea kati ya serikali ya Tanzania na Barick ni kuhusu hatima ya kuzuia makinikia na uwekezaji katika migodi ha North Mara na GGM na siyo kuhusu Buzwagi na Bulyanghulu, migodi ambayo ACACIA wameshakata shauri kuachana nayo mwishoni mwa mwaka huu.

Ikiwa mazungumzo hayo yatakwama, basi Barick wataachana rasmi na biashara ya madini Tanzania ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2018 na taratibu za mwisho kumalizikia mahakamani.

Nimedokezwa kuwa tayari Barick wamepewa masharti mapya ya uwekezaji katika migodi miwili ya North Mara na GGM, masharti ambayo wamedai kuwa ni magumu kutekelezwa.

Aidha bado kuna sintofahamu kubwa katika uwekezaji wa madini ya Tanzanite yapatikanayo Mererani ambapo serikali inadaiwa kuweka mikakati ili kudhibiti uchimbaji wa madini hayo kutoka mikononi mwa wazawa " matajiri" wa Arusha. Rais Magufuli anatarajiwa kuzuru Arusha wiki ijayo ambapo atapeleka kilio kwa matajiri hao wanaodaiwa kukwepa mkondo wa serikali kwenye uuzwaji wa madini hayo

Tayari kumeibuka sintofahamu kubwa kwenye biashara ya Almasi baada ya serikali kutaifisha almasi iliyokuwa isafirishwe nje ya nchi, hali iliyoelezwa kukinzana na mikataba iliyopo ya uuzwaji wa madini hayo kati ya serikali na wawekezaji.
GGM sio mgodi wa acacia
 
Mkuu GGM haipo chini ya Acacia, wamiliki wa GGM ni AngloGold Ashanti...Pili migodi ya GGM na North Mara hawazalishi makinikia (concentrates). Siku nyingine ukileta taarifa jitahidi kutafiti na kuwa makini
 
Hahaha mnatia kinyaaa! Nyie si ndio wagonga madawati wazuri sana kwenye kupitisha sheria za hovyo kama hiyo itakayo pelekwa na nkamia hivi katibuni.
mimi sio mbunge...unataka kusema zile sheria za rasilimali za hivi majuzi zimepitishwa na ccm pekee?
 
Mkuu GGM haipo chini ya Acacia, wamiliki wa GGM ni AngloGold Ashanti...Pili migodi ya GGM na North Mara hawazalishi makinikia (concentrates). Siku nyingine ukileta taarifa jitahidi kutafiti na kuwa makini
Mleta mada aliko sasa hivi atakua anachimbachimba chini kwa kutumia kijiti jinsi alivyoaibika maana wote mmevamia
 
Ngoja tuendeel kuyaona haya!!
Mwaka ujao utakuwa mwaka wa machungu sana kwa watanzania katika sekta ya madini, nimefahamishwa na menejiment ya Barick/ ACACIA ambao wameda kuwa watakuwa wameshaihama rasmi Tanzania kufikia mwezi februari mwaka 2018 kuiacha rasmi migodi yote ya GGM, North Mara, Bulyanghulu na Buzwagi. Wanadai kuwa wanapata vikwazo vipya kila uchwao kufuatia biashara yao ya uwekezaji wa madini nchini Tanzania.

Aidha imefahamika kuwa mazungumzo yanayoendelea kati ya serikali ya Tanzania na Barick ni kuhusu hatima ya kuzuia makinikia na uwekezaji katika migodi ha North Mara na GGM na siyo kuhusu Buzwagi na Bulyanghulu, migodi ambayo ACACIA wameshakata shauri kuachana nayo mwishoni mwa mwaka huu.

Ikiwa mazungumzo hayo yatakwama, basi Barick wataachana rasmi na biashara ya madini Tanzania ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2018 na taratibu za mwisho kumalizikia mahakamani.

Nimedokezwa kuwa tayari Barick wamepewa masharti mapya ya uwekezaji katika migodi miwili ya North Mara na GGM, masharti ambayo wamedai kuwa ni magumu kutekelezwa.

Aidha bado kuna sintofahamu kubwa katika uwekezaji wa madini ya Tanzanite yapatikanayo Mererani ambapo serikali inadaiwa kuweka mikakati ili kudhibiti uchimbaji wa madini hayo kutoka mikononi mwa wazawa " matajiri" wa Arusha. Rais Magufuli anatarajiwa kuzuru Arusha wiki ijayo ambapo atapeleka kilio kwa matajiri hao wanaodaiwa kukwepa mkondo wa serikali kwenye uuzwaji wa madini hayo

Tayari kumeibuka sintofahamu kubwa kwenye biashara ya Almasi baada ya serikali kutaifisha almasi iliyokuwa isafirishwe nje ya nchi, hali iliyoelezwa kukinzana na mikataba iliyopo ya uuzwaji wa madini hayo kati ya serikali na wawekezaji.
 
Kuna mfalme wa Saudia aliwaambia wamarekani kama mnatupangia bei kwa mafuta yetu, ntayachoma moto yote haya mashine na sisi tutarudi kula Tende zetu mlizotukuta nazo.

Wasitutishe tangu wameanza kuchimba madini wanaweza kutuambia mwananchi wa kawaida amefaidika na nini.

Faida walioipata ni kubwa sana hapa wanatikisa kibiriti.

Raisi waambie hata Leo waondoke halafu utawasikia kilio chao
 
Nyie watanzania mmelaaniwa? Acacia/Barrick wanatuibia ma trillions, kwa miaka, sasa wakiondoka si ndio wakwende zao na tutawashtaki watulipe walichotuibia trillions over trillions tshs 408 trillions..

Yaani ww mwana Chadema unasikitika Acacia/Barrick kuondoka? Yaani nyie CDM mna laani kabisa, hivi mkoje? Mwizi anaondoka unalalamika? Hii ni laana kabisa... Hivi kwnn hamtaki kuelewa Acacia/Barrick ni wezi sana? Kwnn mna vichwa vigumu kama mawe?
 
Hakuna uhusiano baina ya Barrick/Acacia na GGM--nimeshindwa kuelewa!
Shida ya kujifungia ufipa kupika taarifa ka kujifanya "kupenyezewa"! Mtoa taarifa hajui lolote kuhusu hii migodi, ila kwa vile anadomo la kuropoka basi acha aendelee
 
Mwaka ujao utakuwa mwaka wa machungu sana kwa watanzania katika sekta ya madini, nimefahamishwa na menejiment ya Barick/ ACACIA ambao wameda kuwa watakuwa wameshaihama rasmi Tanzania kufikia mwezi februari mwaka 2018 kuiacha rasmi migodi yote ya GGM, North Mara, Bulyanghulu na Buzwagi. Wanadai kuwa wanapata vikwazo vipya kila uchwao kufuatia biashara yao ya uwekezaji wa madini nchini Tanzania.

Aidha imefahamika kuwa mazungumzo yanayoendelea kati ya serikali ya Tanzania na Barick ni kuhusu hatima ya kuzuia makinikia na uwekezaji katika migodi ha North Mara na GGM na siyo kuhusu Buzwagi na Bulyanghulu, migodi ambayo ACACIA wameshakata shauri kuachana nayo mwishoni mwa mwaka huu.

Ikiwa mazungumzo hayo yatakwama, basi Barick wataachana rasmi na biashara ya madini Tanzania ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2018 na taratibu za mwisho kumalizikia mahakamani.

Nimedokezwa kuwa tayari Barick wamepewa masharti mapya ya uwekezaji katika migodi miwili ya North Mara na GGM, masharti ambayo wamedai kuwa ni magumu kutekelezwa.

Aidha bado kuna sintofahamu kubwa katika uwekezaji wa madini ya Tanzanite yapatikanayo Mererani ambapo serikali inadaiwa kuweka mikakati ili kudhibiti uchimbaji wa madini hayo kutoka mikononi mwa wazawa " matajiri" wa Arusha. Rais Magufuli anatarajiwa kuzuru Arusha wiki ijayo ambapo atapeleka kilio kwa matajiri hao wanaodaiwa kukwepa mkondo wa serikali kwenye uuzwaji wa madini hayo

Tayari kumeibuka sintofahamu kubwa kwenye biashara ya Almasi baada ya serikali kutaifisha almasi iliyokuwa isafirishwe nje ya nchi, hali iliyoelezwa kukinzana na mikataba iliyopo ya uuzwaji wa madini hayo kati ya serikali na wawekezaji.

Yaani weye jamaa ni mwongo na unapenda sana kupotosha habari na kuziwekea chumvi.
 
Kwahiyo tunawaacha waondoke na Noah zetu au watakuwa washalipa mpaka Feb mwakani??
 
Back
Top Bottom