TLAWI AKONAAY
Senior Member
- Sep 16, 2016
- 110
- 62
Ndugu zangu wana JF nimeleta huu uzi kuwa wilaya yetu ya Hanang ina takribani eka 63000 ambazo ni mali ya serikali kuu. Haya mashamba yapo kwa wawekezaji mbalimbali ambavyo inasemekana wamekodisha kwa tshs 1500 kwa eka kama ifuatavyo:
1. NGANO LTD
Wawekezaji hawa ni raia wa India wamewekeza ndani ya mashamba matatu ambayo ni
a. Gidagamoud wana eka 12000 wamelima eka 6000 na eka 6000 zimelala bila kulimwa
b. Shamba setchet wana eka 16000 wamefanikiwa kulima eka 5000 wameshindwa kulima eka 11000 zimelala
c. Shamba la Murjanda wana eka 11000wamelima eka 4000 eka zilizolala bila kulimwa ni 7000
MAPATO KWA SERIKALI
Hawa wawekezaji wamekodisha eka 39000 ambapo ni sawa na shs 58500000 kwa mwaka. Katika eka hizo 15000 ambazo wanalima ngano wanapata wastani wa gunia 3 kwa mavuno ya mwaka 2015 na 2016 kwa eka ambapo kwa eka zote 15000 wanapata kiasi cha gunia 45000. Katika hizo gunia halmashauri inatoza ushuru wa mazao ambapo kwa gunia ni shs 1000 kwa hiyo wanapata kiasi cha shs 45,000,000 kwa mwaka.
HASARA
Kwa eka 24000 zinalala bila kulimwa serikali inapata hasara kubwa sana . Haya mashamba wangeyalimwa hawa wawekezaji wangepata gunia 72000 kwa wastani wa gunia 3 ambapo halmashauri wangekusanya ushuru wa mazao kiasi cha TSHS 72,000,000 hii ni kwa mashamba zilizolala. Haya mashamba yote yangelimwa halmashauri wangeweza kupata ushuru wa mazao kiasi cha 117,000,000 hivyo basi halmashauri inapoteza fedha nyingi sana kiasi cha asilimia 62. Hii ni hasara kubwa kwa halmashauri ya wilaya ya Hanang kwa upande wa ushuru wa mazao.
SHAMBA MULBADAW
Hawa ni wawekezaji wa Hydom hospital wamewekeza kwenye eka 15000 ambapo kati ya hizo wanalima eka 14000 ndio zinazolimwa na kusalia eka 1000
MAPATO KWA SERIKALI
Wanakodisha kwa shs za kitanzani kiasi cha 22500000 @ eka ni shs 1500. Hawa wawekezaji wanalima zao la ngano na mapato yao yapo juu kidogo kwa sababu wanaweka mbolea ya kukuzia aina ya booster kipindi cha kupiga dawa. Wanapata wastani wa gunia 9 kwa eka kwa kipindi cha kilimo cha mwaka 2015 na 2016 ambapo wanavuna kiasi cha jumla ya gunia 126000 kwa mwaka halmashauri inakusanya mapato ya ushuru wa mazao kiasi cha shs126,000,000 kwa kwa mwaka
HASARA
Wawekezaji hawa hawana hasara yoyote serikalini ambapo eneo la eka 1000 zilizobaki wamewapa wazawa walime kwa kipindi cha miaka 3 baada ya hapo wanaacha kulima.
SHAMBA LA BASUTU
Hii ina takribani eka 9000 ambapo inalimwa na wazawa mmoja moja kwa kukodi. Wanalima eka zote 9000
MAPATO SERIKALINI
Shamba hili linakodishwa kwa mzawa shs 70,000 kwa eka tofauti na hizo 1500. Wanailetea serikali mapato ya kiasi cha shs 630,000,000. Hawa wazawa wanalima mazao mseto mahindi, maharage, ngano, dengu, gilgilani. Hawa wawekezaji wanaipatia serikali faida kubwa mno.
MIGOGORO
Kunatokea migogoro mikubwa kati ya hawa wawekezaji na wafugaji kwani mfugaji yeye anafuata pori kwa ajili ya malisho ya mifugo yake sasa hawa wawekezaji hawataki kuchungwa maeneo hayo walioyaacha. Nilikuwa namhoji mfugaji moja ambaye mifugo yake 700 wamekamatwa na wawekezaji wa ngano LTD alisema yeye amefuata malisho na siyo kingine na kama angeweza kulima mashamba yote asingeweza kuchunga humu
Swali langu ni kwamba kwanini wasipewe wawekazaji wazawa wakalima hayo mashamba yote na serikali ikapata mapato makubwa, mwananchi akapata mazao ya chakula tukaondokana na janga la njaa? Pia ukamwezesha huyu mwananchi akapata pato na akawa anachangia hata michango mbalimbali ya maendeleo ya vijiji vyao?
Mbona hawa wawekezaji ndio chanzo cha migogoro kwa wafugaji hapa Hanang? Kwanini wasilime mashamba yote angalau hata serikali ikapumzika kusuluhisha migogoro ya wawekezaji na wafugaji?
Kama mwekezaji hawezi kulima mashamba yote kwa mkataba waliowekeana na serikali kwani serikali isiwanyang'anye mashamba hawa wawekezaji wazembe?
Tunategemea kuwa na ugeni wa Waziri Mkuu hapa Hanang siku za hivi karibuni. Watutatulie tatizo hili la mashamba.
WanaJF tusaidieni kuchangia ili tuishauri serikali yetu