Wawekezaji wanashikilia uchumi kwa asilima 90 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawekezaji wanashikilia uchumi kwa asilima 90

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by FJM, May 27, 2012.

 1. F

  FJM JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  PAMOJA na Tanzania kupanua wigo wa ukuaji wa uchumi, imebainika kwamba asilimia 90 ya ukuaji huo umeshikiliwa na wawekezaji kutoka nje ya nchi.

  Hayo yalibainishwa juzi jijini Dar es Salaam na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Diplomasia, Abdallah Majura, alipozungumza na Tanzania Daima wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Uchumi na Jamii (ESRF).

  Alisema wawekezaji hao wameshikilia sekta muhimu kama sekta ya madini, ujenzi, ardhi, mabenki pamoja na mawasiliano na kusema kuwa ili uchumi ukue kuna haja ya wazawa kushikilia au kusimamia sekta muhimu nchini. Alisema kutokana na wawekezaji kushikilia sekta hizo kwa kigezo cha kuwekeza, wamesababisha uchumi kuendelea kuporomoka huku maisha ya wananchi nayo yakizidi kudidimia.

  "Uchumi wa Tanzania unamilikiwa na wageni kutoka nje ya nchi hasa kwa kuzishika sekta muhimu ambazo zingetumiwa vizuri na wazawa kwa kutumia wataalamu wa ndani zingeweza kuongeza pato la taifa," alifafanua Majura.

  Source: Tanzania Daima 27 May 2012

  My take: CCM kupitia tamko lake na NEC siku chache zilizopita walisema kuwa serikali iendelee kumiliki njia kuu za uchumi! Sasa kama 90% ya ukuwaji wa sekta muhimu kama madini, matumizi ya ardhi, mabenki na mawasiliono yamo mikononi mwa wageni serikali inamiliki nini?

  Hii ni hatari kwa uhai wa taifa na ningeshauri kwenye bunge linalokuja wabunge wazalendo wanaoona hili balaa wapige kelele. Hapa uhuru wa Tanzania hakuna.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  conditions will be ripe for another Arusha Declaration...
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,608
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  ...Faida yote wanayovuna nchini badala ya kutumika katika kuinua viwango vya maisha ya Watanzania na hivyo kuleta maendeleo ya haraka nchini wanahamishia nchi zao kuneemesha makampuni yao, wafanyakazi wao wa ngazi za juu na shareholders wao. Eti wachimba dhahabu (Barrick & Co) ndio wameongeza kulipa royalties kwa mwaka toka 3% kufikia 4% ya mapato yao!!!!!
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Tatizo namba moja hapa ni Mkapa; Kikwete ana upungufu mkubwa uliomfanya asiwe na initiative yoyote kiuongozi na hivyo amekuwa anajaribu kuvaa viatu vya mkapa tu.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Asilimia 90 Ya Uchumi Wa TZ Unamilikiwa Na Wageni  [​IMG]
  Takriban nusu karne tangu tupate uhuru tunakutana na takwimu zinazopaswa kuchochea mjadala wa umuhimu wa kumuondoa mkoloni.Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi,zaidi ya asilimia 90 ya uchumi wa Tanzania unamilikiwa na wageni.Kwa bahati mbaya (au makusudi) habari hiyo haikuingia kwa undani kujadili impacts zinazosababishwa na hali hiyo lakini kilicho wazi ni kwamba uhuru wetu uko mashakani.Katika zama hizi ambapo nguvu za kiuchumi zina athari kubwa kwenye siasa,ni dhahiri kuwa hata huo uhuru wetu wa kisiasa unabaki kuwa wa kinadharia zaidi kuliko uhalisia..Habari husika ni hii hapa
  Na Ramadhan Semtawa
  ZAIDI ya asilimia 90 ya uchumi wa Tanzania unaendelea kumilikiwa watu wenye asili ya Asia na Ulaya, takwimu zinaonyesha.

  Takwimu hizo zimetolewa huku kukiwa na kilio kikubwa cha Watanzania wazawa, kutaka wajengewe mazingira mazuri ya uwezeshaji ili kumiliki uchumi wa nchi kupitia migodi mikubwa ya madini na maeneo nyeti ya kiuchumi.

  Lakini wakati kilio hicho kikiwa hakijapata ufumbuzi, Taarifa ya Utendaji ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, iliyowasilishwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi jana, ilisema watu wenye asili ya mabara ya nje wanaomiliki uchumi wa Tanzania ni sawa na asilimia moja ya Watanzania.

  Takwimu hizo zilifafanua kwamba, asilimia hiyo 90 ya uchumi wa nchi umeshikwa na watu wenye asili ya Asia na Ulaya, wakati asilimia 99 ya Watanzania wazawa, hawana kitu.

  Kwa mujibu wa takwimu hizo zilizowasilishwa katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yusuph Mzee, tatizo la Watanzania weupe kumiliki uchumi, lilianza tangu wakati wa ukoloni.

  "Wakati wa enzi za ukoloni na hata baada ya uhuru Watanzania wengi hawakuwa wakishiriki kikamilifu katika kumiliki uchumi wa nchi yao. Uchumi wa nchi umeendelea kutawaliwa na wageni wakishirikiana na Watanzania wachache," inasema sehemu ya ripoti hiyo.

  Ripoti hiyo inasema "asilimia 99 ya wananchi ni Watanzania weusi na asilimia 1 iliyobaki inajumuisha Waasia na Wazungu ambao wana miliki zaidi ya asilimia 90 ya uchumi wa nchi hii (Msambichaka, 2008).

  "Hii ina maana asilimia 99 ya Watanzania halisi wanamiliki asilimia 10 tu ya uchumi wa taifa lao," inasisitiza ripoti.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kurekebisha kasoro zilizoko, ikiwa ni pamoja na kuanzisha (lililokuwa) Azimio la Arusha, Vijiji vya Ujamaa, Elimu ya Kujitegemea, Serikali za Mitaa, Vyama vya Ushirika, Sera ya Uwekezaji na Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.

  Inasema hata hivyo,juhudi hizo hazijazaa matunda yaliyotarajiwa na kwamba na kwamba kushindikana kwa juhudi za kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao, ndilo chimbuko la kubuniwa kwa mkakati wa kuwawezesha wananchi kiuchumi, katika ilani ya CCM ya mwaka 2000."


  CHANZO: Mwananchi

  Asilimia 90 ya Uchumi Wa TZ Unamilikiwa na Wageni ~ Kulikoni Ughaibuni
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kumbe wahindi wamepinduliwa kwenye kushika uchumi wa Tanzania! Maana tuliambiwa kuwa wahindi kumi tu walikuwa wanashikilia uchumi wote wa Tanzania. Tunabadili wahindi na kuweka wawekezaji ambao kimsingi ni wachukuaji. Kweli yetu ni Danganyika.
   
 7. e

  emalau JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba we wazawa don't think big, kila mbongo sasa hivi anafikiria kwenda china kuchukua bidhaa fake ili apate faida ya haraka. Sasa kama wabongo fursa hamzioni wanaotoka nje wanaziona wawasubiri?

  Kingine ni kwamba nchi hii viongozi wana tabia ya kuwanyima taarifa raia wake, kiongozi akishaona fursa anamwita mtu wa nje wanaigia dili vijisenti vyake anawekewa nje ya nchi. Ndo maana sasa hivi viongozi wana mamilioni nje ya nchi ni kwa mtindo huu.

  Anayebisha kama tunanyimana taarifa aniambie ni lini aliwahi kuona scholarship ya kwenda UK, USA, CANADA imetangazwa gazetini.
   
 8. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  hapo kwenye red kaka hauko sahihi, ila nashukuru majibu umeyatoa tena hapo chini kwenye blue. nionavyo mimi ni matokeo ya wenye mamlaka kukosa uzalendo na kuamini kuwa uwekezaji ni kwa ajiri ya wageni tu na sio wazawa. wazawa tunaangaliwa kama maadui vile. SERIKALI YENYEWE IKO WAPI?????? HII YA MAFISADI CCM????? TUTANGOJA SANA????? TUIONDOENI HARAKA SANA.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna sehemu nakubalina sana na huyo jamaa, hususan kwenye Ardhi (na ndio ute wa mgongo wa uchumi mwingine wote uliotajwa) maana Ardhi ya Tanzania kubwa baada ya Serikali inahodhiwa na Kanisa. Nani asiyejuwa kuwa Kanisa ni wawekezaji wa nje ya nchi?

  Abdallah Majura anaona mbali.
   
 10. K

  KVM JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Kuna matatizo kama matatu makubwa yanayosababisha uchumi wa nchi yetu kuwa mikononi mwa wageni. Serikali imewathamini zaidi watu wanaotoka nje kuliko wazalendo. Hii inaonekana jinsi serikali iavyowabana sana watanzania kwenye ulipaji wa kodi lakini wawekezaji kutoka nje wanapata ahueni kubwa hata kama wanapata faida. Kwa mfano, Vodacom inasemekana mapato kutoka Tanzania ndiyo yanayowapa faida zaidi kuliko nchi nyingine zote walikowekeza.

  Lakini baya zaidi ninaloliona mimi ni kuwa makampuni mengi makubwa kama Vodacom yana wanahisa Watanzania ambao hawataki kabisa kulipa kodi na serikali inakubaliana nao. Hili ni tatizo la ufisadi. Sijui ni wangapi wanakumbuka Watanzania hawa (wale wa Vodacom) walitaka kuuza hisa zao lakini wakakataa katakata kuziuza Tanzania ili wananchi wa kawaida wanufaike.

  Tatu, Watanzania wengi ni wababaishaji sana kiasi cha kwamba hatuwezi kuaminika. Mabenki mengi yamelizwa na Watanzania. Hata mimi ningekuwa benki nisingewakopesha kirahisi Watanzania. Wakati fursa za uwekezaji zipo nyingi Tanzania tunashindwa kupata mikopo kutokana na tabia yetu.

  Nini kifanyike? Kwanza kabisa inabidi tupate mkuu wa nchi ambaye atachukia madudu yaliyopo sasa hivi. Dawa siyo kuwafukuza wageni. Kwa kiasi kikubwa wageni wametusaidia sana kuimarisha uchumi wetu. Tunachohitaji Tanzania ni utawala bora. Utawala wa sheria. Utawala unaotaka wananchi wake kutii sheria na kutendewa haki. Kuna watu wanasifia uchumi uliokuwepo enzi za JKN. Ukweli ni kuwa JKN alikuwa hajui kabisa mambo ya uchumi. Nchi iliyumba sana kiuchumi.
   
Loading...